Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
Ndugu zangu Watanzania salama? Kila ninapofuatilia mijadala ya kisiasa nchini kwetu, ninashangazwa sana na ukosefu wa hoja za msingi kuhusu namna ya kuendeleza Tanzania yetu na hatma yetu kama Taifa!
Sote tunakubaliana kwamba tunahitaji kuishi ktk Taifa linalofuata misingi ya utu na haki, aliyotuachia Baba wa Taifa, Mwl. Julius. K. Nyerere na Abeid Amani Karume.
Hatuhitaji Taifa la watu wanaotukanana muda wote au wanaotekana na kudhalilishana! Vitendo hivyo huwa haviwi na mwisho mwema! Vinajenga chuki na visasi! Ni watu wajinga tu wasioweza kutambua hilo!
Tunahitaji Taifa la watu wamoja, wanaojadiliana kwa uwazi, kwa heshima na kuona tofauti zao kama ni njia ya kupata suluhu kwenye changamoto zao!
Tunahitaji watu wanaojiuliza ni kwa nini Afrika - pamoja na rasilmali zake zote - imebaki kuwa bara la nchi za chini kabisa duniani, zinazoelekezwa na mabeberu nini cha kufanya na kunyonywa tu siku zote?
Ni kwa nini hata uamuzi wa demokrasia ya vyama vingi - ambao ungeweza kusaidia demokrasia kwa kiwango kikubwa - bado haujaleta matokeo kama ya wengine, wakiwamo Wachina, ambao walibuni mfumo wao wa kipekee tofauti na uliberali, unaowasaidia?
Nimeiuliza Chatgpt kwamba kwani Waafrika ni binadamu wajinga zaidi kuliko wote duniani kwa sababu ndio wanebaki wakiitwa nchi maskini wakati wana rasilmali zote? Chat inanieleza kuwa hakuna ushahidi huo.
Lakini, Chat hainisaidii kujua ni kwa nini sisi baada ya uhuru, tumeendelea kuuana vita vya wao kwa wao, kuwa na mapinduzi ya kijeshi, kupigana tu fitna, kuingia mikataba ya kijinga na mataifa mengine kuhusu rasilmali zetu na wakati leo tuko huru!
Nikamuuliza Chat kuhusu mataifa ya Asia ambayo yalifanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na viwanda, baada ya uhuru wao. Akasema, wale walijitambua na kujua wanataka nini! Wakaweka sera sahihi, mikakati sahihi ya kujikomboa kisiasa, kijamii na kiuchumi!
Nilipomuuliza kuhusu kwa nini Waafrika hawafanyi hivyo? Jibu lake limenitafakarisha sana! Anasema, Waafrika hawajaweka sera sahihi na mikakati sahihi ya kujikomboa kwa sababu viongozi wanawaza zaidi namna ya kubaki madarakani na kuyashikilia kuliko kesho bora ya mataifa yao!
Nilipomuuliza ni kwa nini hali iko hivyo kwa Afrika pekee na siyo kwa mataifa mengine, yakiwamo ya Asia? Akasema kitu nilichohitimisha kama kwamba: 'Waafrika hawajajitambua,'.
Ninatoa wito kwa CCM na vyama vya ushindani. Kaeni pamoja mjadili maslahi ya Taifa ambayo ninyi nyote mnapaswa kuyasimamia na kuyapigania!
Demokrasia ya kugombania madaraka Afrika haijatusaidia na haitatusaidia kamwe! Inawasaidia zaidi wale wanaotaka tufarakane ili wapenyeze hoja zao!
Nimeuliza mara kadhaa, ni kwa nini Waafrika tunaendelea kushuhudia madhila mengi kwa watu wetu, wakati tuna rasilmali kama zote, ambazo leo wanazifaidi wengine?
Nimesisitiza, ni kwa nini hata nchi za Afrika zilizobadilisha sana vyama madarakani bado zina matatizo makubwa ukilinganisha na Tanzania?
Kuna watu wameniuliza ni kwa nini kila post yangu ninarudia hoja hii ya nchi zilizobadilisha vyama madarakani kuwa na changamoto!
Lengo langu ni kuruhusu fikra tunduizi iongoze namna tunavyofikiri! Kwamba katiba mpya ni muhimu sana, lakini haina majibu yote kwa changamoto za Waafrika. Kwa sababu zipo nchi zinaongozwa kwa katiba mpya na zina changamoto kubwa zaidi kuliko Tanzania!
Je, tunapojadili kuwa na katiba mpya, tunapaswa kuzingaria masuala gani muhimu kwa maisha yetu binafsi na kwa mustakabali wa Taifa letu na Afrika kwa ujumla?
Je vijana wetu (Gen-Z) wanafahamu kuwa tunaweza kuwa na katiba mpya na bado wakaendelea kuishi kwa shida zile zile, kama wale wa Kenya au Afrika Kusini?
Hoja yangu - pamoja na kukubali wito wa katiba mpya - ni kwamba ni lazima Waafrika waje pamoja, wahoji mifumo ya kinyonyaji ya kidunia na watake kuwapo kwa mageuzi ya mifumo hii ili kuweka uwanja sawa ktk ushindani!
Bila mabadiliko haya, Afrika itaendelea kuishi kwa taabu saba!/
*******
*******
#Copiedfrom_TheIntelegencyOne!