Kwa haya yanayojiri katika kipindi cha miezi mitatu hivi hadi Watanzania waingie kwenye vyumba vya kupiga kura sio mambo mazuri kwa CCM na uongzi uliopo.
Vitendo vingi sana vya unyanyasaji wa wana siasa vinaendelea wakati huu. Mnaojua ukweli ni kwamba vitendo hivi vitazidi kuongezeka hasa wakati wa kampeni na kufanya watu wengi kuzidi kuchukizwa na hali ya haki na usalama wa watu ambayo tayari imeshakuwa mbaya.
Uongozi mbaya mara zote huleta mwisho wake wenyewe. Uongozi uliopo sasa unaweza kufikiri kuwa kwa kuwabana wananchi na kutumia nguvu ndio vitawasafishia njia, lakini ukweli ni kwamba hali ndio inazidi kuwa mbaya zaidi.
Ukiwasikiliza watu wengi utagundua wamechoka na hawana imani tena na uongozi uliopo. Machache mazuri hayawezi kuficha mengi mabaya.