Yawezekana kama Mwanadamu Idi Amin alikuwa na Mapungufu yake ila nimegundua Afrika ya leo iliwahitaji akina Amin wengi ili kupiga hatua

Yawezekana kama Mwanadamu Idi Amin alikuwa na Mapungufu yake ila nimegundua Afrika ya leo iliwahitaji akina Amin wengi ili kupiga hatua

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Marehemu Idi Amin Dada....

1. Alichukia Upuuzi (Upumbavu)

2. Alichukia Uonevu na Dharau

3. Aliwapenda sana Wananchi wake

4. Hakuwa Mnafiki na wa Kujipendekeza

5. Hakuwa Muoga kuipigania nchi yake

6. Hakuwa Fisadi (Mwizi) hata kidogo

7. Alikuwa Mbabe ili Kulinda nchi yake

Sasa wakati umefika kwa Waafrika Kukiri kuwa tulikosea au tulilazimishwa tu na 'Mabeberu' katika Kumchukia Idi Amin Dada hivyo tuombe Radhi kwa Familia yake na hata kwa Mwenyezi Mungu ikiwezekana.

Kwa mtazamo mfupi tu ni kwamba kama nikisema niyapime Madhambi ya Marehemu Idi Amin Dada kipndi chake na hawa Viongozi wa sasa wa Afrika tulionao Mzani wangu utalalia hasa kwa Viongozi wa sasa kwani 90% yao wanafanya (wanatenda) maradufu ya aliyokuwa akiyafanya Idi Amin Dada ila Waafrika wengi ama kwa Unafiki wetu au kuwa Kwetu Mapopoma (Majuha) au kwa Kushikiwa kwa muda Akili zetu na Mabeberu (Wazungu) tunaogopa Kukemea, Kukosoa na hata Kusema Ukweli juu ya Masuala Mtambuka katika nchi zetu nyingi (kama si zote) za Kiafrika.

R.I.P sana tu Marehemu Idi Amin Dada.
 
tutajie maendeleo yeyote aliyoyafanay idi amini kwa kipindi chote alichotawala, zaidi ya kufukuza wahindi na kunyangánya/kuua biashara zao, kutupa vilema mto kagera, kula nyama za watu na kulala na wanawake.
Kula nyama za watu mi uwa naamini ni uongo walikuwa wanamchafua ili aonekane wa hovyo. Imagine Magu hapa alijaribu kutupeleka kibabe kidogo na maendeleo tuliyaone tena kwa kasi sana but ni mangapi mabaya amesemwa na mabeberu na sisi wenyewe? Hivi tungelipata kina Magu km watano wakiongoza kwa kufululiza kwa style ya kibabe unadhani hii nchi ingefika wapi kimaendeleo!

Tulingelifika mbali. Nakwambia nchi zetu bado zinahitaji viongozi wababe ili zisonge, naunga mkono mada kwani bado tunawihataji kina Idd Amin,kina Gaddaf, kina Magu ili tusonge mbele, wabongo sie tukiongozwa kwa kubembelezwa hatuwezekani tena.
 
Angewapenda wananchi wake wangempigania sio kunsaliti kama walivyokuja kumsaliti Ibilisi mwenzie Gadaffi!

Ona rais wa Ukraine anavyopiganiwa na wananchi wake, rais ukiwa mwovu vita ikitokea wananchi watakusaliti tu
 
Kula nyama za watu mi uwa naamini ni uongo walikuwa wanamchafua ili aonekane wa hovyo.Imagine Magu hapa alijaribu kutupeleka kibabe kidogo na maendeleo tuliyaone tena kwa kasi sana but ni mangapi mabaya amesemwa na mabeberu na sisi wenyewe?Hivi tungelipata kina Magu km watano wakiongoza kwa kufululiza kwa style ya kibabe unadhani hii nchi ingefika wapi kimaendeleo!Tulingelifika mbali.Nakwambia nchi zetu bado zinahitaji viongozi wababe ili zisonge,naunga mkono mada kwani bado tunawihataji kina Idd Amin,kina Gaddaf,kina Magu ili tusonge mbele,wabongo sie tukiongozwa kwa kubembelezwa hatuwezekani tena.
Maendeleo ya kuandika kwa kuunganisha maneno kama ulivyofanya?

Kama unaona Magu alileta maendeleo unamatatizo makubwa ya kufikiri nyie ndio mnaweza hata kumwabudu shetani
 
tutajie maendeleo yeyote aliyoyafanay idi amini kwa kipindi chote alichotawala, zaidi ya kufukuza wahindi na kunyangánya/kuua biashara zao, kutupa vilema mto kagera, kula nyama za watu na kulala na wanawake.
Hizi propaganda ndo mlilishwa na watawala wenu enzi zile mpaka tukawa tunaimba Kambona Gaidi ameolewa na ukaamini kweli.
 
Back
Top Bottom