Kuna kipindi Russia ilionya kitendo cha kuwapa Ukraine silaha za masafa marefu na data za intelijensia waweze kupiga eneo la mbali ndani ya Russia.
Ikaonya juu ya tukio la Ukraine kushambulia ndege muhimu ya kimkakati wa nukilia ( strategic nuclear defense system ) iliyo kuwa ndani kabisa ya Russia mbali na war front line.
Hiki kinachotokea sasa kwa Marekani na Iran ndicho kisasi alicho ahidi Putin. Playbook Iran kalipua ndege za ulinzi za surveillance hewani zilizo kuwa zimepaki mbali.
Iran kalipua mifumo ya radar na Patriots muhimu. Jiulize teknolojia ile wametoa wapi na satellites za precision kubwa hivyo wametoa wapi Kama siyo China na Russia wanawapa hivyo vitu?
Watu walidhani Russia atalipa kisasi kwa kushambulia nchi ya NATO moja kwa moja. Vita ni akili.
US ana aibishwa na Iran..
Ili kuepuka hio aibu anasema Iran inapewa assist na hizo nchi..
Ukweli ni kwamba Iran pekee ina huo uwezo wa kupiga target yeyote ya adui iliyopo hapo miidle east. Nashangaa jinsi watu wana underestimate uwezo wa Iran.
Iran wana makombora yanatumia inertia navigation system/INS , huo mfumo hawategemei mfumo wa uendeshaji wa Russia/glonass ama China/beidou achilia gps ya US ambayo hawaitumii kabisa..
Huo mfumo missile ikirushwa inakwenda yenyewe haitegemei mawasiliano yeyote kutoka nje, kama kombora likitumwa kutoka Dar kwenda Dodoma linakadiria speed, umbali , uelekeo na hata altitude, hivyo hata kama adui ana mitambo ya kufanya jamming haitoweza kupoteza hilo kombora maana linakwenda kwa kujitegemea, hata Tehran kwenyewe wanakuwa hawana tena uwezo wa kuliensesha. Sasa Iran missiles zake za INS z sasa amezifanya kuwa za kidijitali.
Ndio maana jamming, electronics warfare tactics zimeshindwa kabisa kuzuia missiles za Iran.
Hivyo Iran hata pasipo Beidou wala Glonass bado wanaweza kuitumia INS na wakapiga mahala kwa usahihi wa kutisha.
Iran wana makombora pia yana camera, wana makombora yana sensors za mawimbi ya radio na joto...
Likifika eneo husika likahisi kuna mawimbi ya patriot yanatokea mahala flani, basi kombora linakwenda huko huko patriot ilipo.
Iran pia wana mifumo ya kufanya jamming na spoofing kwenye gps.. hivyo missiles inapokwenda eneo husika , radars za ulinzi inakuwa ngumu kufahamu kama missile inakuja.