Vita ya Iran haiwezi sababisha vita ya tatu ya Dunia.
Marekani anachofanya sasa hivi anarudisha nyuma Iran kutoka kwenye fukwe, anachochea ni kuifanya Iran ishindwe kuuza wala kunafika na mafuta yake, ikishakuwa hivi Iran haitakuwa na uwezo wa kuendesha vita kwa muda mrefu.
Kingine Israel na Marekani hadi sasa wamefocus na IRGC na kuliacha Jeshi la Taifa la Iran, kisiasa wanatengeneza fursa kwa jeshi la Iran kuweza kuwa na nguvu sawa na IRGC, hii inaweza kuwa kama case ya Sudan nchi moja ina majeshi mawili ambayo yana mtazamo/Ideology tofauti.
Iran tayari iko kwenye mtikisiko wa uchumi, kuharibiwa kwa bandari, madaraja na vituo vya umeme vinachochea hali ya uchumi kuendelea kudorora, kwa wananchi Uchumi kwanza ubabe wako wa kivita baadaye, hapa Marekani na Israel wanachochea Wairan watoke barabarani.
Kingine Israel na Marekani katika mashambulizi yao mawekuawa wakishambulia vituo vya polisi, ofisi na uwezo wa nchi kusimamia usalama wa ndani, yakitokea maandamano mengine Israel na Marekani wakijaza Silaha na moto kwa waandamanaji, nchi inakuwa Somalia au Syria