Yawezekana Tanzania ikawa ya MwiSho kukombolewa, hata Burundi watatutangulia

Inawezekana lakini kama walitumia hio mbinu basi hao jamaa kwenye masuala ya kijasusi wameshindikana, maana captain alichokuwa anakisema hakikuwa na afya kwao, na wananchi walipokea maneno ya captain ambayo yalikuwa ni ya kutengeneza chuki dhidi yao , kama walifikia hatua ya kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe ili kumpata HP, basi hao watu si mchezo.

Mi naona ratiba ilikuwa inaendelea vyema, hadi ile siku captain anatoka kuzungumza pale ndipo mambo yakatokea.

Hapo kuna mawili kugeukana ama uvujaji wa taarifa but the question is kwanini matukio yafuatane siku ya kukamatwa na siku ya captain kuzungumza mtandaoni?

Kwenye uvujaji wa taarifa ni either waliuzana au mambo ya 'trust chain' na mistakes ndogo ndogo...

Kama waliuzana hopefully waliomuuza walishapotelea kwa usalama wao, maana hawatoaminika tena... na mpango umeharibika wote.

Kama ni uvujaji wa taarifa basi wapo wanajipanga, kwa mujibu wa mdogo mtu anasema siku zao zinahesabika.
 
U
Binafsi nilikuwa nilimsikiliza polepole kwa makini mnoo.
Plan A : Kutumia ushawishi wake na kutoa taarifa za ndani kupitia uzoefu wake ndani ya CCM, na kupata uungwaji mkono ndani ya ccm ili mchakato urudiwe, na kwakuwa ana kipawa hicho aliamini CCM mtandao wangesita na kurudi kwenye mchakato. Mission failed: alisema pia hata yeye hakutegemea, ila ameplay part yake)

Plan B: ilikuwa sasa kuwajaza hasira wananchi kupitia uchambuzi wake wa mambo yanayoendelea ( ahadi za kampeni, utekaji., n.k) ili wananchi na baadhi ya watu kwenye vyombo waungane kuukataa huu uchaguzi ikiwemo maandamano. ( hii siwez kusema ni failed mission ingawa aliondoka too soon, tusubiri 29 Oct)

Plan C: Hii sifahamu walipanga nn kwenye kupambana na mtandao ikiwa watapenya.
 
Wananchi ndio wamebaki wanasikilizwa wafanye maamuzi ya mwisho na kuwapatia wazee wa kazi uhalali wa kuingia kazini...


Ndio maana mtandao nao wanatumia nguvu zao zote kuzuia lisitokee, maana wanaelewa nini kitafuatia, HP alisema watu watanyongwa, wengine watakimbia nchi, wengine watafungwa...

Hawa wengine wanasema ole wao watakaowagusa wananchi...

Tusubiri mwamba alisema atarudi... lakini ndani ya siku hizi chache kuna tamko lingine litatokea nadhani kutoka upande wa wananchi.
 
 
Inasikitisha Sana....inahitajika msaada wa Gen Z wa 254.
 
Priorities mkuu. As long as unapata tsh 100 ya kula, kulala na bando la JF, who cares about "corrupted leadership"? Hathari direct ni ndogo sana they become negligible.

Vijana watajali muda ukifika. Kwa sasa wako bize kuangalia Etugul na Breaking Bad kujipoza na harakati za maisha magumu.
 
Mwamba hawezi kurudi, wamemuweka sehemu, ni ngumu kurudi, labda alikuwa anawachezea akili akimaanishi kuna mwengine kwenye kundi lao waliokubaliana ndo atarudi kutoa neno, hivyo hawa watatumia nguvu kubwa kumyima nafasi uyu kurudi kumbe kuna mwamba mwengine anakuja kuruka hewani.
 
Polepole alikuwa anatetea tumbo, baada ya kuacha kazi alitakiwa akikache chama na aje atuelezee mabaya ya Magu. Na kwa nini Samia kaiga mabaya ya Magu. Alitakiwa aje na ajenda ya kusogeza uchaguzi mbele na tukazanie mchakato wa katiba. Kitendo cha yeye kutaka uchaguzi ufanyike katika mfumo huu huu uliopo, unaridhia kwamba huyu jamaa alikuwa anataka arudi kwenye system. Hata kumuua ni rahisi maana wanajua hakuna upinzani utamtetea na kumkumbuka. Na walio CCM wao ni matumbo tu na hawafungamani na mtu.
 
Mageuzi yapi ndugu wakati Jamaa alitaka Samia aachie ngazi CCM ipate mgombea mwingine waingie kwenye uchaguzi. Jamaa alikuja na ngojera za Samia ndio tatizo. Tatizo sio mtu wala kikundi cha watu tatizo ni mfumo. Huyu jamaa hotuba yake ya kwanza ilitakiwa kuwa kusogeza uchaguzi na kutetea mchakato wa katiba mpya.
 
Ndicho nilikuwa namaanisha, upande wa wananchi anaweza tokea mwingine, maana team wananchi wanategemea wananchi wafanye kweli na hawataki kuona wananchi wanatishwa na kupewa hofu.

Hapo anaweza jitokeza kiongozi wa dini, mtu fulani kutoka vyombo vya ulinzi na usalama ama mwanasiasa kuhamasisha tena watu kutoka.

Ndio maana mtandao wanawatia nguvuni wapinzani na wahamasishaji wa kutoka 29 oct kwa speed ya 5G pasipo sababu za msingi, kule mahakamani shahidi hakufika makusudi na kesi imerushwa hadi November.

Mtandao wapo kwenye surviving mode, wapo kwenye shock, ndio maana badala ya kuzima moto wanaongeza petrol, wanatumia either nguvu ama pesa. Katika hali hio mtu uwa anashindwa kutumia akili vyema bali anafanya lolote kujiponya.
 
Mwongozo umeshatolewa kwa vitendo na Wananchi wa Songwe
 
Bri kaishiwa pawa ๐Ÿ˜ƒ
Kaona vitu haviendi, anaona ubashiri wake unakutana na ukuta.. Atulie alipo ishia yeye Gen Z ndio wanaanzia.. Hawa Majasusi wa Tz na vyombo vingine vya usalama walisha prove fail toka kitambo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ