Yawezekana watanzania wanapenda zaidi kandanda kuliko Siasa, siyo kwa nyomi hii ya Yanga hapa Mkapa

Yawezekana watanzania wanapenda zaidi kandanda kuliko Siasa, siyo kwa nyomi hii ya Yanga hapa Mkapa

Wrong and wishful thinking!
Ni kosa kubwa ku politicise michezo.
Ikitoka michezo itaingia dini.
Mwalimu aliwahi kusema huko ni kufilisika kisiasa.
Mkuu Jidu, kuna kitu sii watu wengi wanakijua kuhusu, kitu kinachoitwa "colour therapy", watu wanachagua kitu fulani kutokana na rangi zake!.

Amini usiamini kuna watu wanaipenda timu fulani kutokana tuu na jezi yake!. Mimi nilimpenda sana Pele, hivyo nikaipenda timu ya Brazil, enzi zile za jezi yao ya stripes nyeusi na nyeupe.

Kwenye UK Premier League, nikajikuta nimeipenda New Castle kwasababu tuu ya jezi!.

Bendera zote zenye rangi nyekundu ni rangi ya damu, watu wenye allergy ya damu, wakiona tuu kitu chenye nyekundu, wanakichukia!. Hivyo amini usiamini kuna watu wanaipenda Yanga kutokana na jezi yake, na kuna watu, wanakipenda kile "Chakijani" kutokana na rangi zake!. Subiria tarehe 28 October, uone nani ataibuka mshindi kati ya Chakijani, na chenye rangi ya damu damu!.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...Vaw3NF_WZEf1JJBr5l-KI6rEZ&cshid=1598850233224
P
 
Ni sawa tu mkuu.
Lakini kwa hali halisi hapa mjini, upenzi wa Yanga au Simba, pamoja na rangi zake , upenzi huo una mizizi iliyoenda mbali sana.
Na si siasa.
Tukumbke kuwa mpira(kwa Yanga na Simba) ni upenzi na si uhalisia wa maisha .
Siasa ni uhalisia wa maisha na ni serious.
Mtu anaweza kuipenda timu yake na ikishinda anaweza tembe uchi, na mimi nimeon hilo.
Kuna wanao lia machozi club ikishindwa, na ikishinda club kuna extreme joy
Na hili linagusa sehemu ya ubongo unaohusika na passion.
Football passion inaemeenda mbali sana, kuna emotion, excitement na dedication kwa upenzi wa club.
Na football inaawaunganisha watu wa aina zote na of different background, mara nyingi isiyohusu siasa kabisa.

Lakini leo chama changu kikishinda siwezi kuona mtu akitembea uchi kuunga mkono juhudi.
Hata akishinda mbunge wangu na tukajengewa mabarabara mengi, bado nitasema huo likuwa wajibu wake.
Upenzi wa siasa ni tofauti kabisa na unahusisha the logical part of the brain.
Malengo na msimamo mliojiwekea katika siasa usipomsaidia mtu au jamii lengwa, mtu huyo anasepa.
Hata Mwalimu kipindi fulani aliwahi kusema ufuasi kwa chama, CCM , ni sera zake.
Kama sera haziendani na ninachokiamini basi chama si mama yangu, naweza kuondoka.
 
Kwa taarifa yako uchaguzi huu utakuwa na wapiga kura wachache sana. Fuatilia vizuri, hamasa ya kisiasa imeshuka sana ndani ya hii miaka mitano ya Magufuli. Tulizoea vipindi moto moto vya kampeni kwenye TV, tulikuwa tunaona mijadala moto moto inayoonyesha mafanikio na mapungufu ya miaka mitano iliyoisha, na matarajio ya miaka mitano inayofuata. Midahalo kadhaa iliyopandisha hamasa. Ila sasa hivi muandishi kama ww Paskali na ww upo kwenye mijadala ya nyomi kwenye kampeni, badala ya mijadala mizito kwenye luninga ya uchaguzi!

Yaani kama taifa tumegeuzwa tunajadili burudani zaidi, kuliko kipindi kizito cha mustakabali wa maisha yetu. Cha ajabu kuanzia wasomi mpaka wasiojua kusoma tunajadili matukio badala ya issues. Nilitarajia muandishi nguli kama ww saa hii ungekuwa hata umeaandaa vipindi maalum vya uchaguzi, hasa midahalo ya wagombea kadhaa wa uchaguzi. Waandishi nguli wa nchi nyingine, wangekuwa wanajua nini wawape wananchi wao kwa wakati nyeti wa taifa kama huu. Hali hii inasikitisha na kuumiza, lakini hapo ndio Magufuli katufukisha.
Kwenye burudani huko uzuri wake matokeo huyajui tofauti na uchaguzi wa Tz ambao hata mtoto mdogo anajua kuwa vyovyote iwavyavyo lazima ccm ishinde(iwe kihalali au si kihalali),sasa hapo kuna cha maana zaidi ya kupoteza muda tu?
 
Siasa haina mvuto kutokana na kukosa fair ground. Watu wanaona bora wakaangalie mpira tuu. Huko kwenye siasa CCM inataka kila siku yenyewe ishinde tuu hata kwa kutumia nguvu sasa kuna siasa tena hapo.
Na zaidi ni kwamba hakuna tofauti kati hao ccm na hao wapinzani,wengi washaunga juhudi wengine walipotolewa kwenye system ndio wanaona ccm haitendi haki.

Hivyo ni utapelo utapeli tu.
 
Kwenye burudani huko uzuri wake matokeo huyajui tofauti na uchaguzi wa Tz ambao hata mtoto mdogo anajua kuwa vyovyote iwavyavyo lazima ccm ishinde(iwe kihalali au si kihalali),sasa hapo kuna cha maana zaidi ya kupoteza muda tu?

Ishinde sio kihalali.
 
Back
Top Bottom