Yemi Alade afunguka; Zuchu kamfunika Davido na Wanaija wengine

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
Baada ya Zuchu kufanya show kwenye jukwaa la kimataifa kwenye African Day ambayo host alikuwa Idris Elba.

Zuchu alifanya show ya kukata na mundu kiasi crowd yote ikabaki na butwaa hapo mjini Lagos kwa wapopo.

Akaibuka yemi Alade akaongea na media za kimataifa akasema ameshangazwa na show ya Zuchu kwani ni ya kiwango cha kustaajabisha akasema ndio show bora kwenye usiku huo.

Zuchu alifanya show nzuri kushinda Davido na wasanii wengine wa Nigeria waliopanda kwenye stage hiyo.

 
Nimeiyona hiyo performance aisee bidada katisha katuwakilisha vizuri hivyo ndio mnatakiwa mfanye sio masuala yakuangaika na makiki
Siku hizi watu wameshazoea mambo ya kiki watu wanataka kuona unakua sio insta stories kila asubuhi. Zuchu ni big thing
 
Huyo yemi alade ni Mungu? Akisema jambo ndio inakua hitimisho?

Yeye katoa mtazamo wake kama yeye,kila mtu ana mtazamo wake na uhuru wake wakuelezea jinsi alivyo vutiwa na jambo fulani,hatufanani,

Juma Lokole unakwama wapi?
Sawa mtazamo wake ndio huo Zuchu kamfunika Davido
 
ila zuchu kawa star kiajabu sana hapo ndio utaijua nguvu ya Diamond
Hamna maajabu bali kupeana muda na kuwekeza. WCB msanii wanamtizama kama bidhaa na ndio maana wanaipa thamani na wana ipromoti.

Hapo ndipo wanapozipiga bao label nyingi za East Africa, kuna wasanii wengine wapo kwenye label ambazo hata wao wenyewe hawajui zinahusiana na nini.

Diamond ndiye msanii pekee yupo tayari kusimamisha projects zake binafsi kwa ajili ya kumpromoti na kumpush msanii wake,wasanii wengine wameanzisha label kama kufuata mkumbo, ila wana wapotezea mda wasanii walio wasaini kwani muda haumsubiri mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…