Yericko Nyerere aandika Kitabu Kipya cha MOSCOW: Operesheni Ukraine

Yericko Nyerere aandika Kitabu Kipya cha MOSCOW: Operesheni Ukraine

SANGAPIPI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
206
Reaction score
301
Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi bora wa vitabu barani Afrika na mdau wa JamiiForums ndugu Yericko Nyerere ametangaza leo kuachia kitabu kipya kinachoelezea vita vya Urusi kinachapishwa,

Katika utangulizi wa Kitabu hicho, Yericko Nyerere anasema, Kitabu cha MOSCOW: Operesheni ya Ukraine, ni mahsusi juu ya Oparesheni Maalumu ya Kijeshi ya Urusi nchini Ukraine ya 22 Februari 2022 hadi Octoba 2023, hasa eneo la Mashariki mwa nchi hiyo maarufu kama DONBASS lenye Majimbo ya Donetsk na Luhansk, na Mikoa ya Kherson na Zapolozhye. Kitabu kinaeleza chanzo halisi cha mgogoro wa Ukraine na Urusi kwa ushahidi wa kinyaraka. Kitabu kinaeleza hatua kadha wa kadha zilizochukuliwa na Moscow kabla, wakati na baada ya operesheni hiyo.

Kitabu kinaeleza mtiririko wa mwenendo na matukio halisi kutoka katika uwanja wa mapigano huko Donbass, kutoka ndani na nje ya Ikulu ya Urusi ya Kremlin, kutoka ndani na nje ya Ikulu ya Ukraine, kutoka ndani na nje ya Ikulu ya Marekani ya "White House," na kutoka katika viunga vya Umoja wa Ulaya na NATO ambao kwa PAMOJA Walishirikiana na Ukraine kupambana na Moscow dhidi ya Operesheni hiyo.

Kitabu kina Kurasa 1,400
Sura 1-14,
Marejeo 389
Bei kinauzwa kwa 150,000/=

IMG_1332.jpeg

2dd53a9f-30fd-47a8-bc8d-5cda63086083.jpeg

28a20873-d3a2-4347-9f2f-07264218101b.jpeg
 
Hivi ni sahihi kitabu kuachiwa kabla ya vita kuisha?

I mean hapa katikati hakuna matukio muhimu ambayo yanaweza kujitokeza na kuwa potential zaidi kwenye kitabu chake?
Operesheni ilikamilika tangu Octobar 2023, kwasasa kilichopo ni offensive ya Ukraine kujaribu kurejesha Ardhi iliyotwaliwa na wanashindwa hadi leo
 
Kifanyiwe book review katka online TV, Yericko Nyerere atupe kwa ujumla tutegemee nini kutoka book hili la kurasa 1,400.

Je kinapatikana pia Amazon, Mkuki Na Nyota n.k au toka katika hivyo vyanzo tu vya simu zilizowekwa.

Mwandishi Yericko Nyerere kusoma kwake katika Chuo kilchokuwa katika iiiyokuwa Shirikisho la Urusi iliyovunjika inampa nafasi ya kipekee kuandika antropolojia ya mawazo ya jamii ya Russia na Ukraine....
Antropojia ni kujiuliza maswali na kutafuta majibu ya jinsi Putin Russia Ukraine wanavyofikiri hili ni eneo ukiishi wa wenyeji inakupa utambuzi Antropojia ya Kijamii( Social Anthropology) ya mataifa hayo mawili na raia zake kwa undani

TOKA MAKTABA:
Vitabu zilivyochapishwa awali na kupitiwa na mchambuzi binafsi

View: https://m.youtube.com/watch?v=nSnxcJ40ynA
 
Hicho kitabu lazima kitakuwa kimebase kuitetea urusi tu maana tokea mwanzo Yeriko alikuwa ni mpenzi wa putin so hiki kitabu hakina jipya maana inajulikana mtuzi yupo upande gani utasoma na mifugo yako kigamboni huko
 
Kifanyiwe book review katka online TV, Yericko Nyerere atupe kwa ujumla tutegemee nini kutoka book hili la kurasa 1,400.

Je kinapatikana pia Amazon, Mkuki Na Nyota n.k au toka katika hivyo vyanzo tu vya simu zilizowekwa.

Mwandishi Yericko Nyerere kusoma kwake katika Chuo kilchokuwa katika iiiyokuwa Shirikisho la Urusi iliyovunjika inampa nafasi ya kipekee kuandika antropolojia ya mawazo ya jamii ya Russia na Ukraine....

TOKA MAKTABA:
Vitabu zilivyochapishwa awali na kupitiwa na mchambuzi binafsi

View: https://m.youtube.com/watch?v=nSnxcJ40ynA

Jamaa kasoma nchi za usoviet?
 
Hivi ni sahihi kitabu kuachiwa kabla ya vita kuisha?

I mean hapa katikati hakuna matukio muhimu ambayo yanaweza kujitokeza na kuwa potential zaidi kwenye kitabu chake?
Kitabu mwendokasi au vodafasta.
 
Hicho kitabu lazima kitakuwa kimebase kuitetea urusi tu maana tokea mwanzo Yeriko alikuwa ni mpenzi wa putin so hiki kitabu hakina jipya maana inajulikana mtuzi yupo upande gani utasoma na mifugo yako kigamboni huko
Halafu kitajaa uongo mwingi sana kama ilivyo ada ya Putin mwenyewe. Ukiona mtu anatetea sera za Putin na Urusi yake ujue kabisa mtu huyo ana mapungufu makubwa sana kwenye kifuu chake au labda anafanya makusudi tu kuvutia wajinga ilihali yeye mwenyewe akijua kuwa anachotetea siyo cha kweli.
 
Sema vitabu vya Yericko bei kinoma. Kile ujasusi anauza 80,000!! Hiki 150,000.
Kuna wanajeshi na watu wengi wanaguswa moja kwa moja na hiyo vita,nina hakika hawa watakuja kuandika habari za vita hii,sio kwa kuperuzi mitandaoni kwa kile walichoona kwa macho,Sidhan hata kama bei itafika huko.
 
Back
Top Bottom