Yericko Nyerere ashinda Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Afrika

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Taasisi ya Tuzo za Zikomo Africa Award ya yenye makao makuu nchini Zambia zimefanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili, Novemba 19, 2023 nchini humo.

Mara baada ya kutangazwa mshindi kwa kuwashinda washindani wenzake nane kutoka Botswana, Uganda, Zambia na Zimbabwe, Nyerere amewashukuru Watanzania wote waliompigia kura.

"Asanteni sana Watanzania wote mlionipigia kura, Tanzania imeshinda," amesema Nyerere

Baada ya kutwaa Tuzo hiyo, Nyerere ameikabidhi kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule aliyekuwapo ukumbini kama ishara ya Itifaki ya Ki-nchi na Balozi akatoa neno la ki-nchi la kumpongeza na kuhamasisha Watanzania wasome na waandike vitabu.

Baadhi ya vitabu alivyoandika ni cha Ujasusi wa Kidola na Kichumi, toleo la 2016, Kitabu cha Mapambano ya Madaraka, toleo la 2017, Kitabu cha Strategy The Road to Power, toleo la 2018 na Kitabu cha Mtu Baada ya Mtu, toleo la 2020.
IMG_20231019_210735_191.jpg
 
Hahaaaa Nyerere Licha ya kuwa mwandishi nguli hapa JF anatambulika pia kama Mwanachama wa Chadema. Hilo lina shida gani?
Halina shida ila mbona mnapiga kelele Taifa 🌟 kuhusihwa na CCM?

Kama Yericko (Mtanzania) ni CHADEMA basi usikatae kwamba Taifa 🌟 (Tanzania) ni CCM kwa kuwa CCM na Serikali yake ndiyo iliyoanzisha hii timu.
 
Hongera sana kwake,waliokua wanamchukulia poa,labda kwasababu za kichama,kwamba kwasababu yu CHADEMA,hivyo wakawa wanambeza wakijua kaandika mambo ya kuponda labda CCM,ndo wasome sasa,jamaa kaandika nondo,hadi nje ya mipaka,waka-appreciate na kumuweka kwenye list,nasasa ni mshindi.
 
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Taasisi ya Tuzo za Zikomo Africa Award ya yenye makao makuu nchini Zambia zimefanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili, Novemba 19, 2023 nchini humo.

Mara baada ya kutangazwa mshindi kwa kuwashinda washindani wenzake nane kutoka Botswana, Uganda, Zambia na Zimbabwe, Nyerere amewashukuru Watanzania wote waliompigia kura.

"Asanteni sana Watanzania wote mlionipigia kura, Tanzania imeshinda," amesema Nyerere

Baada ya kutwaa Tuzo hiyo, Nyerere ameikabidhi kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule aliyekuwapo ukumbini kama ishara ya Itifaki ya Ki-nchi na Balozi akatoa neno la ki-nchi la kumpongeza na kuhamasisha Watanzania wasome na waandike vitabu.

Baadhi ya vitabu alivyoandika ni cha Ujasusi wa Kidola na Kichumi, toleo la 2016, Kitabu cha Mapambano ya Madaraka, toleo la 2017, Kitabu cha Strategy The Road to Power, toleo la 2018 na Kitabu cha Mtu Baada ya Mtu, toleo la 2020.
Jamaa anajua.
 
Back
Top Bottom