Yeriko Nyerere: CIA waliamini Mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka ni Mangi Thomas Mariale!

Yeriko Nyerere: CIA waliamini Mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka ni Mangi Thomas Mariale!

Wengi mnabisha bisha kipumbavu bila kuwa na hoja. Hizo smartphone zenu mnatumia kufanyia nini badala ya kujisomea mambo mbalimbali? Maandiko mengi ya Yericko ni copy & paste kutoka kwa waandishi wengine. Kabla ya social media nilikuwa nikisoma sana gazeti la Rai na baadae Raia mwema. Kule kulikuwa na waandishi nguli tupu. Na makala nyingi za Rai na Raia mwema zipo kwenye kitabu cha Yericko.
 
Thomas Marealle alitaka Uhuru ucheleweshwe angalau miaka 10 baada ya 1961. Ni kweli kuwa Nyerere njia yake haikuwa nyepesi hasa kipindi cha utawala wa Gavana Edward Twinning.

Pia Machifu wa Tanganyika kipindi hicho walikuwa washirika wa Utawala wa Kikoloni kwa njia ya Indirect Rule na walikuwa na baraza lao(Chiefs Council)

Uwezekano wa Mangi Marealle kuwa chaguo la kuachia nchi ulikuwa mkubwa kwa sababu alikuwa kwenye mfumo na pia alikiwa msomi.
 
Mjumbe wa mikutano mkuu wa CHADEMA Yeriko Nyerere amesema Taarifa za Siri za Shirika la Ujasusi la Marekani CIA za mwaka 1953 zinaonyesha CIA waliamini mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika basda ya wakoloni wa Kiingereza kuondoka ni Kiongozi wa Wachagga Mangi Thomas Mariale

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄
Yericko Nyerere tangu adanganye kuwa hawa wamama wa kariakoo ni masista wa shirika la maryknol ndipo nilipomuona tapeli.
images (3).jpeg

Cc Mohamed Said
 
Burito kambarage Nyerere aliebatizwa hapo tabora na kuitwa julius akiwa chini ya majesuits wa kanisa katoliki akashinda bid hiyo,dhidi ya chief kidaha wa usukumani na thomas Mareale akiwa chini ya fabian society!!

Hiyo ni kweli kabisa Wala hajaongopa huyu mkulima wa Bamia!
 
Mjumbe wa mikutano mkuu wa CHADEMA Yeriko Nyerere amesema Taarifa za Siri za Shirika la Ujasusi la Marekani CIA za mwaka 1953 zinaonyesha CIA waliamini mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika basda ya wakoloni wa Kiingereza kuondoka ni Kiongozi wa Wachagga Mangi Thomas Mariale

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄
Aisee aisee aisee, kumbe babu yangu alidhulumiwa eeeh?! Ngoja...
 
Nyerere akawazidi akili kina mangi.
plus babaake na mbowe walishawishi machief tz
Thomas Marealle alitaka Uhuru ucheleweshwe angalau miaka 10 baada ya 1961. Ni kweli kuwa Nyerere njia yake haikuwa nyepesi hasa kipindi cha utawala wa Gavana Edward Twinning.

Pia Machifu wa Tanganyika kipindi hicho walikuwa washirika wa Utawala wa Kikoloni kwa njia ya Indirect Rule na walikuwa na baraza lao(Chiefs Council)

Uwezekano wa Mangi Marealle kuwa chaguo la kuachia nchi ulikuwa mkubwa kwa sababu alikuwa kwenye mfumo na pia alikiwa msomi.
kuna watu walikuwa wakorogaji kuna bwana mmoja toka pande kwa wameru alienda dai uhuru wa kaskazini ya arusha watu walishikwa na hasira ushawishi wa mzee aikaeli(rafiki mkubwa wa nyerere) kwa kina mariale na machief wengine wa tz ndo wakakubali nyerere aongoze jahazi wengi mnamsema mariale ila hawakua na huo mpango at the time sababu alikuwa kwenye memorundum of understanding. na wazungu ila pia kuna wazee wakiswahili ndo waliompokea. nyerere mjini na kumuongezea ushawishi(Sykes,said,mohaaa, nk....haikuwa safari ndogo
 
Yeriko anawadanganya wajinga. Kipindi hicho cha ukoloni Uingereza alikuwa na nguvu za kijasusi kuliko hata hao marekani. Waingereza waliijua nguvu ya Nyerere ndo maana wakampa nchi bila kumwaga damu kama kwingine. Julius K Nyerere alikuwa ni akili-kubwa aliwazidi akili machifu wote akiwemo huyo mareale.

.. CIA documents kama ziko declassified zinaweza kutoa ukweli wa madai ya Yericko.

..Tanganyika haikuwa koloni, sisi tulikabidhiwa kwa Waingereza watulee kwa niaba ya UN. Baada ya Mjerumani kushindwa vita kuu makoloni yake yaliwekwa chini ya UN.

..Kila mara wakati wa utawala wa Waingereza kuna timu ya makoloni kutoka UN ilikuwa inakuja kuangalia na kukagua kinachoendelea. Timu hiyo ilikuwa inachukua wasaa wa kuzungumza na wazawa katika makoloni hayo.

..Machifu walimsaidia Mwalimu Nyerere na Tanu katika harakati za kudai uhuru. Halikuwa suala la Mwalimu Nyerere kuwazidi akili na Machifu. Hata Mangi Thomas Marealle alikuwa ni mmoja wa Machifu walikwenda UN kudai na kuunga mkono madai ya Uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom