Yesu akirudi leo atasali wapi? Kwa Wayahudi, RC /Wasabato au Kwa Walokole? Au Mashahidi wa Yehova? Naomba majibu

Yesu akirudi leo atasali wapi? Kwa Wayahudi, RC /Wasabato au Kwa Walokole? Au Mashahidi wa Yehova? Naomba majibu

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
Nawasalimu wote.

Kumekuwepo na mjadala kuhusu ipi dini ya Kweli, huu ni mjadala wa siku nyingine. Leo nataka tumuongelee YESU KRISTU.

Wakati akiwa hapa duniani, Yesu alionekana hekaluni akihubiri injili, Wayahudi hawakupendezwa sana wakisema anakufuru na kupelekea kumsulubisha msalabani.

Baada ya kifo na ufufuo wake (Kama ilivyoandikwa) ndipo lilianza vuguvugu la kanisa la kwanza!

Ukiwauliza RC watakwambia, Papa wa Kwanza ni Mt Petro na alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Ukiwauliza Walokole nao watakwambia wao ndio wapo sahihi, Vivyo Hivyo kwa Wasabato au Mashahidi wa Yehova!

Kama biblia inayotumika ni moja inakuwaje kuna mgongano huu mkubwa?

Je, ni kitu gani hawatuambii?
 
IMG_20240604_163318.jpg
 
Atapenda kujua Kama kazi alizowaachia wanafunzi wake zinatekelezwa ikumbukwe aliwaagiza akisema. "Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili... "

Kuihubiri injili hakuna maana ya watu kuanzisha makanisa...

Imeandikwa hivi:

Marko 16
15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Lengo la kwenda kuihubiri injili imelenga kuwe na matokeo mawili ambayo yametajwa hapo kwenye rangi nyekundu, na endapo kutakuwa kuna ukaidi basi hatma imetajwa pia...
 
wenye Afya hawana haja na tabibu.. uwo ndio msimamo wake.. isipokuwa walio hawawezi.. yeye marazote ana deal na wenye dhambi tu na wala sio kusali wapi.
 
Umeuliza ili ujue lakini ikitokea amekuja leo haji kusali popote. Anakuja kufuata wale ambae waliweza kumsubiria Kwa unyenyekevu.

Akiwachukua tu anawapeleka Kwa Baba yake mahali alipowaandalia. Kwa sasa yeye ni Bwana wa wale wanaomwamini na kumfuata vema.
 
Dini Gani wanaoingia msikitini?
Luka 4:16
Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi kama ilivyokuwa desturi yake.
Lakini walimlalamikia hashiki sabato akawaambia Sabato iliumbwa kwa ajili ya mwanadamu na Siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato
 
Umeuliza ili ujue lakini ikitokea amekuja leo haji kusali popote. Anakuja kufuata wale ambae waliweza kumsubiria Kwa unyenyekevu. Akiwachukua tu anawapeleka Kwa Baba yake mahali alipowaandalia. Kwa sasa yeye ni Bwana wa wale wanaomwamini na kumfuata vema.
Watu hao wanyenyekevu atakaowachukua wanasali wapi?
 
wenye Afya hawana haja na tabibu.. uwo ndio msimamo wake.. isipokuwa walio hawawezi.. yeye marazote ana deal na wenye dhambi tu na wala sio kusali wapi.
Kwanini, umekuwepo msisitizo wa dini yaani ukiwaambia watu namwamini Mungu watakuuliza unasali dini ipi? Ukiwaambia Mkristo watakuuliza dhehebu!!
 
Back
Top Bottom