Yesu alikuwa mfanyabiashara, Mohammed alikuwa mfanyabiashara: Kwanini wafanyabiashara wakristo na waislam wengi sio waaminifu?

Yesu alikuwa mfanyabiashara, Mohammed alikuwa mfanyabiashara: Kwanini wafanyabiashara wakristo na waislam wengi sio waaminifu?

Ninachotaka kusema ni kuwa alikuwa selemala mtoto wa selemala. Hayo mengine siyajui ndio naomba uniletee mstari unaosema alifanya biashara. Sasa kwa mfano kama alichonga kumsaidia baba yake anakuwaje mfanyabiashara?

Kumbuka akiwa mdogo alikutwa hekaluni. So unaona interest yake haikuwa biashara unayodai. Na hili linathibitishwa na Yeye tena akiwa mtu mzima.

Luke 2:41-49
Now his parents went to Jerusalem every year at the feast of the passover. And when he was twelve years old, they went up to Jerusalem after the custom of the feast. And when they had fulfilled the days, as they returned, the child Jesus tarried behind in Jerusalem; and Joseph and his mother knew not of it.

But they, supposing him to have been in the company, went a day's journey; and they sought him among their kinsfolk and acquaintance. And when they found him not, they turned back again to Jerusalem, seeking him.
And it came to pass, that after three days they found him in the temple, sitting in the midst of the doctors, both hearing them, and asking them questions. And all that heard him were astonished at his understanding and answers.

And when they saw him, they were amazed: and his mother said unto him, Son, why hast thou thus dealt with us? behold, thy father and I have sought thee sorrowing. And he said unto them, How is it that ye sought me? wist ye not that I must be about my Father's business?

John 4:34 "Jesus saith unto them, My meat is to do the will of him that sent me, and to finish his work."

Sasa hiyo ndiyo biashara ya Bwana Yesu. Sasa na wewe leta verse za kupiga biashara ya samani na ma marketingi, nini sijui?
Yesu alikuwa anafanya Biashara.
Mtoto mzalishaji wa samani (kwa mujibu wa Mathayo) ambaye baadae jamii nzima ilimtambua wa taaluma ya uselemala(Marko).

Kwanza Hakukuwa na hekalu Nazareti aliokulia. Hekalu kilikuwa Yerusalem. Kama dar mwanzakama Israel ingekuwa Tanzania.

Kuse.a Yesu alikuwa anashinda hekaluni ni uongo.

Ilikuwa ni tukio la siku moja tu.

Hayo mengine aliyasema alipoianza mazi yake Mya ya urabbi na ukombozj wa mwanafamu.
Ila kabla ya hao alikuwa akiafanya Biashara ya vitu alivyokuwa anabuni na kufyatua.
 
Hata hakuna haja ya kumjadili YESU. Kwani ametenda maajabu mengi sana. Tumwabudu, na kumpenda tu kwa wale tunaomwamini. Msikilize Ananias Ediga kama unapenda kufahamu habari zake zaidi.
Kwa nini unasema tusimjadili Ila tukamsikilize mtu flani mkuu.

Yesu kasema lazima tumjua.

Uzima wa milele ndo huu, wakujue wewe Mungu wa Kweli na wa pekee na Yesu uliyemtuma.

Sasa utamjuaje usipojadili mkuu.

Lazima tumjue na shughuli zake zot
 
Hata wakati wao kulikuwa na walaghai na walikuwa wanaktazwa kufanya dhuluma kwenye mizani maana wengine walikuwa wanamwagia maji chini ili nafaka iwe nzito

Hii tumekatazwa na pia mizani iwe haki bila kuwa na utapeli
Sio wafanyabiashara wote washirikina au waizi
Mimi nimeuza bidhaa sana na nimeisharudisha hela za ziada mara kibao kwa wateja wangu

Kuna siku niliuza vocha za jumla za 1.5m kwa mteja wangu akanipigia simu na kusema pitia hela zako
Alipotoa hela tu nikajua ni nyingi sana nikamuambia hizi sio 1.5m ni zaidi ya hizo

Kuja kuzingalia zilikuwa 3M
Akanishukuru nikasepa
Siku nyingine kaja mtu na hela zake kununua aliponipa hela nilizomtajia akawa kaongeza Laki nikamrudishia daa jamaa hakuamini kuwa nimerudisha laki alibaki kaduwaa kama dakika nzima ameshangaa

Sio wote waizi
Mkuu kula tano.

Hizi ndio sababu ilibidi Yesu apitie kwenye Biashara ilina sisi tumuige kuwa waaminifu.

Umeuongezea Uzi damu.
 
Hujielewi ww pole.ni vema ukae kimya ujifunze.yosef ndo alikua fundi seremala.usichanganye mafail
Unasoma biblia kwa uoga kwa kuofautiana na mapokeo.

Angalia fungu nimeweka hapo Marko.

Wateja au wanakijiji wa nazareti wanasa huyu kijana ninselemala. Hawajasema ni volunteer wa uselemala wa kuchonga viti vya sinagogini.

Maana yake alikuwa anapiga bizness
 
Yesu kafanya Sana Biashara ya furniture. Maana hata kazi za kiroho alianza akiwa na takribani miaka27.

Nazareti nzima walimjua Kama fundi. Alikuwa atengenezi vya kutumia. Alikuwa anauza.

Kwa sasa tuseme angekuwa ni wamiliki maduka makubwa ya furniture.
Huyo no Yosefu (Yusuf) Baba Mlezi wa Yesu.
 
Mtume alikuwa amenyooka?una uhakika?Yesu pekee ndo alikuwa mkamilifu mwanakondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu
Nadhani kuna vitu viwili mnavichanganya kwenye huu uzi ambavyo ni imani pamoja na maisha ya kawaida.

Mkiachana na mambo ya imani mkajikita kwenye maisha ya kawaida na halisi basi mtamuelewa vizuri mleta mada.

Hao kina Yesu na Mohammed walizaliwa na kulelewa kama wototo wengine tu, kazi za utume na unabii wamezianza wakiwa watu wazima above 25yrs. Hivo basi kabla ya kuanza kutekeleza majukumu mama waliyo pangiwa na Mungu toka wakiwa tumboni, walikuwa wanajishughulisha na shughuli zingine kwajili ya kujipatia kipato na chakula ili waweze kuishi na kujikimu.

Hebu Jaribuni kuweka kando mambo ya imani zenu mjikite kwenye maisha halisi, Mtume Muhammad na Yesu mwana wa adam hawakuzaliwa katika familia za kitajiri au kifalme bali walizaliwa katika familia masikini zinazo tegemea kupambana kufanya kazi mbalimbali ili zipate kukidhi mahitaji. Sasa bila kufanya kazi wangeweza je kuishi? Au mlitaka maisha yao kabla ya kuanza majukumu yao mama nayo yawekwe kwenye maandiko? Kama mnaona ni dhihaka mtu kusema Yesu na Muhammad walifanya kazi na biashara je siku akifufuka jamaa yeyote alie cheza nao utotoni akaanza kuwapa story zao za utotoni si mtamuua kabisa.

Nadhani tuelewe tu kuwa, mtu akisema walifanya biashara au walifanya kazi flani asichukuliwe kama kadhihaki au katukana, maana hata wanafunzi wa yesu kabla hawajaanza kazi ya Mungu walikuwa na kazi zao, wengine walikuwa wavuvi, wengine wafugaji, wengine wahunzi na n.k

Ila kama mkitaka mtoe mapovu yasiyokuwa na maana kwa mleta mada basi endeleeni na mawazo yenu hayo ya kufikiri kama Yesu na Muhammad hawakupitia maisha ya kawaida ya mwanadamu. Na sijui ninani aliwakaririsha kufanya kazi au biashara ni dhihaka au dhambi hadi mtoe mapovu.

Yangu ni hayo tu, na lengo la bandiko hili nikujaribu kuweka tu mambo sawa, nasi kubadili mitazamo na imani binafsi ya kila mtu juu ya manabii hao.
 
Yesu hakuwa mfanyabiashara, alikuwa anajishughulisha na fenicha kwa sababu mzee wake alikuwa fundi, kwa hiyo ni kama kazi za nyumbani tu. Kwanza hata useremara wenyewe alikuwa anazuga tu ili miaka isogee aanze kuchapa injili watu watubu dhambi zao wamrudie Mungu.
 
Mleta uzi alitaka kutumia mifano iyo miwili ila kuonyesha kwa nn hao mitume tunaowafuata walikuwa waaminifu ila sisi tunaendekeza utapeli kwa sana

Je kwa huu mwenendo wetu wa utapeli ,ufisadi, uwizi ni dhahiri hatuwafuati tumebaki maneno tu

Ila vijana wa ovyo wala nguruwe ,wezi, madhulumatii ,walevi , wazinzi wanaleta point hazipo
Kama wote walio Comment na kupitia huu uzi wangekuwa waelewa kama wewe, hakika wasingefanya mada rahisi kama hii kuwa complicated na hao ndo wanafanya dini ionekane kama ugonjwa wa akili wakati akili zao ndo tatizo.

Wakuu nadhani inatakiwa mjikite kwenye hili swali kujenga hoja zenu; kama mitume na manabii tunao wafuata katika imani, hawakuwa na skendo zozote katika biashara na kazi zao, kwanini sisi wafuasi wao tumejaa skendo kwenye kazi na biashara zetu??
Mfano wa skendo ni, dhuruma, utapeli, uchawi, wivu, wizi, ufisadi, nongwa, kuuwana na uovu wote mnaoujua.
 
Kama wote walio Comment na kupitia huu uzi wangekuwa waelewa kama wewe, hakika wasingefanya mada rahisi kama hii kuwa complicated na hao ndo wanafanya dini ionekane kama ugonjwa wa akili wakati akili zao ndo tatizo.

Wakuu nadhani inatakiwa mjikite kwenye hili swali kujenga hoja zenu; kama mitume na manabii tunao wafuata katika imani, hawakuwa na skendo zozote katika biashara na kazi zao, kwanini sisi wafuasi wao tumejaa skendo kwenye kazi na biashara zetu??
Mfano wa skendo ni, dhuruma, utapeli, uchawi, wivu, wizi, ufisadi, nongwa, kuuwana na uovu wote mnaoujua.
Ndo tulivyo kupenda kukwepesha mambo ya maana
 
Kama wote walio Comment na kupitia huu uzi wangekuwa waelewa kama wewe, hakika wasingefanya mada rahisi kama hii kuwa complicated na hao ndo wanafanya dini ionekane kama ugonjwa wa akili wakati akili zao ndo tatizo.

Wakuu nadhani inatakiwa mjikite kwenye hili swali kujenga hoja zenu; kama mitume na manabii tunao wafuata katika imani, hawakuwa na skendo zozote katika biashara na kazi zao, kwanini sisi wafuasi wao tumejaa skendo kwenye kazi na biashara zetu??
Mfano wa skendo ni, dhuruma, utapeli, uchawi, wivu, wizi, ufisadi, nongwa, kuuwana na uovu wote mnaoujua.
Huku ndio nilikuwa nataka kwenda.

Maana hata mitume hawakuwahi kwenda mabarabarani kuhubiri na kukusanya sadaka. Walienda sokoni Kama wafanyabiashara. Mafano Paulo na kushare gospel huku na wao walifanya Biashara halali bila Kuomba Sadaka zamtu.


Mambo ya Sadaka yalifanyikia makanisani.

Kuna vitu wengi wako gizani sana
 
Mkuu Yesu alikuuzia samani gani? wapi? Lini? Sh ngapi?
Kwahiyo alikuwa anachonga alafu anazivundika products zake.?

Daa!!!

Lazima alikuwaana business plan
Marketing na sales stratergy zake
Anatunzahesabu.

Huwezikunielewa Hadi ujifunze mafundisho yake alioanza kufundisha.zile zilikuwa ni lekcha zamtu mwenye uzoefu mkubwa wa industry karibu zote.

Mfano Luka 14:28
Huwezi kutoa hii kauli Kama Hauna uzoefu wa Projects Management.

Na atakuwa amejifunza katika family Business aliyoachiwa na mzee wake kabla hajajikita katika ministry yake.


Yesu ukimuelewa kiupana ni mtamu Sana.
 
Yesu hakuwa mfanyabiashara, alikuwa anajishughulisha na fenicha kwa sababu mzee wake alikuwa fundi, kwa hiyo ni kama kazi za nyumbani tu. Kwanza hata useremara wenyewe alikuwa anazuga tu ili miaka isogee aanze kuchapa injili watu watubu dhambi zao wamrudie Mungu.
Biashara ni nini?
Wanakijiji wamesema Yesu ni Fundi wanamjua maana alikuwa anawatengenezea vitu.

Kwa wayahudi Biashara ilikuwa ni wewe kuuza bidhaa yako, na mnunuzi kutoa pesa. Na inakuwa biashara ilikamilika kwa Yule mpokea fedha kurithika na alichopokea na na alipokea fedha ameridhika.

Win win situation.

Haya Yesu akifanya Sana. Has Mtume akifanya. Ila hakuwa na kashfa.


Hii ni wito kwa wachungaji wasipende Sadaka wakasahau kuwaadibisha waumini Kama Yesu
 
Tujadili kidogo.

Wafanyabiashara wengi Kama sio waislam ni wakristo.

Lakini wengi sio waaminifu. Wanatumia juju na uchawi, wanaforce kupata faida isivyo halali,kukwepa Kodi na kukwepa taratibu rasmi

TATIZO linatoka wapi ikiwa Yesu alikuwa mfanyabiashara wa samani(furniture)lakini hakutenda dhambi?

Mtume Mohammad SAW alikuwa mfanyabiashara muaminifu Sana chini ya Khadija. Akifanya Biashara Kati ya saudia na Syria. Alikuwa amenyooka.

Tunafeli wapi wakuu.

Karibuni
Yesu hakuwahi kuwa mfanyabiashara.
 
Hapana. Yesu asingemkabidhi mama yake kwa jirani yake Familia ya Yohana wakati mume wake alikuwepo.

Inaonekana yeye ndiye alikuwa analisha na kuendesha familia.

Soma kabla hajafa. Mama yake alimtafutia pa kumuacha.
Shida yako una kashifu tu!
 
Ualimu na urabi alianza baadae Sana.

Ukienda mtaani kwao wanamjua ni fundi na mfanya Biashara mkubwa wa furniture.

Hata Paulo alikuwa mfanya Biashara mkubwa wa kujenga mahoteli. / Tents zile kwa sasa ni Kama nyumba za kulala wageni.


Pamoja na wakina Pricilla


🤣🤣🤣

Kisa Yusuph Baba yake alikuwa seremala
 
Hao jamaa sijui wanabisha nini, mbona ni akili ya kawaida tu hapo.

Sasa mtu akiwa seremala si ni mfanyabiashara tayari, ni sawa na ubishe kua wale wavuvi sio wafanyabiashara.

Hapo ni vile tu hatujaoneshwa maisha yake ya biashara yalikuaje, labda wangeandika walau kidogo watu wangejifunza kwa matendo na kupunguza dhulma, uchawi na unafiki kwenye biashara.
 
Back
Top Bottom