Yesu alikuwa mfanyabiashara, Mohammed alikuwa mfanyabiashara: Kwanini wafanyabiashara wakristo na waislam wengi sio waaminifu?

Yesu alikuwa anafanya Biashara.
Mtoto mzalishaji wa samani (kwa mujibu wa Mathayo) ambaye baadae jamii nzima ilimtambua wa taaluma ya uselemala(Marko).

Kwanza Hakukuwa na hekalu Nazareti aliokulia. Hekalu kilikuwa Yerusalem. Kama dar mwanzakama Israel ingekuwa Tanzania.

Kuse.a Yesu alikuwa anashinda hekaluni ni uongo.

Ilikuwa ni tukio la siku moja tu.

Hayo mengine aliyasema alipoianza mazi yake Mya ya urabbi na ukombozj wa mwanafamu.
Ila kabla ya hao alikuwa akiafanya Biashara ya vitu alivyokuwa anabuni na kufyatua.
 
Hata hakuna haja ya kumjadili YESU. Kwani ametenda maajabu mengi sana. Tumwabudu, na kumpenda tu kwa wale tunaomwamini. Msikilize Ananias Ediga kama unapenda kufahamu habari zake zaidi.
Kwa nini unasema tusimjadili Ila tukamsikilize mtu flani mkuu.

Yesu kasema lazima tumjua.

Uzima wa milele ndo huu, wakujue wewe Mungu wa Kweli na wa pekee na Yesu uliyemtuma.

Sasa utamjuaje usipojadili mkuu.

Lazima tumjue na shughuli zake zot
 
Mkuu kula tano.

Hizi ndio sababu ilibidi Yesu apitie kwenye Biashara ilina sisi tumuige kuwa waaminifu.

Umeuongezea Uzi damu.
 
Hujielewi ww pole.ni vema ukae kimya ujifunze.yosef ndo alikua fundi seremala.usichanganye mafail
Unasoma biblia kwa uoga kwa kuofautiana na mapokeo.

Angalia fungu nimeweka hapo Marko.

Wateja au wanakijiji wa nazareti wanasa huyu kijana ninselemala. Hawajasema ni volunteer wa uselemala wa kuchonga viti vya sinagogini.

Maana yake alikuwa anapiga bizness
 
Huyo no Yosefu (Yusuf) Baba Mlezi wa Yesu.
 
Mtume alikuwa amenyooka?una uhakika?Yesu pekee ndo alikuwa mkamilifu mwanakondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu
Nadhani kuna vitu viwili mnavichanganya kwenye huu uzi ambavyo ni imani pamoja na maisha ya kawaida.

Mkiachana na mambo ya imani mkajikita kwenye maisha ya kawaida na halisi basi mtamuelewa vizuri mleta mada.

Hao kina Yesu na Mohammed walizaliwa na kulelewa kama wototo wengine tu, kazi za utume na unabii wamezianza wakiwa watu wazima above 25yrs. Hivo basi kabla ya kuanza kutekeleza majukumu mama waliyo pangiwa na Mungu toka wakiwa tumboni, walikuwa wanajishughulisha na shughuli zingine kwajili ya kujipatia kipato na chakula ili waweze kuishi na kujikimu.

Hebu Jaribuni kuweka kando mambo ya imani zenu mjikite kwenye maisha halisi, Mtume Muhammad na Yesu mwana wa adam hawakuzaliwa katika familia za kitajiri au kifalme bali walizaliwa katika familia masikini zinazo tegemea kupambana kufanya kazi mbalimbali ili zipate kukidhi mahitaji. Sasa bila kufanya kazi wangeweza je kuishi? Au mlitaka maisha yao kabla ya kuanza majukumu yao mama nayo yawekwe kwenye maandiko? Kama mnaona ni dhihaka mtu kusema Yesu na Muhammad walifanya kazi na biashara je siku akifufuka jamaa yeyote alie cheza nao utotoni akaanza kuwapa story zao za utotoni si mtamuua kabisa.

Nadhani tuelewe tu kuwa, mtu akisema walifanya biashara au walifanya kazi flani asichukuliwe kama kadhihaki au katukana, maana hata wanafunzi wa yesu kabla hawajaanza kazi ya Mungu walikuwa na kazi zao, wengine walikuwa wavuvi, wengine wafugaji, wengine wahunzi na n.k

Ila kama mkitaka mtoe mapovu yasiyokuwa na maana kwa mleta mada basi endeleeni na mawazo yenu hayo ya kufikiri kama Yesu na Muhammad hawakupitia maisha ya kawaida ya mwanadamu. Na sijui ninani aliwakaririsha kufanya kazi au biashara ni dhihaka au dhambi hadi mtoe mapovu.

Yangu ni hayo tu, na lengo la bandiko hili nikujaribu kuweka tu mambo sawa, nasi kubadili mitazamo na imani binafsi ya kila mtu juu ya manabii hao.
 
Yesu hakuwa mfanyabiashara, alikuwa anajishughulisha na fenicha kwa sababu mzee wake alikuwa fundi, kwa hiyo ni kama kazi za nyumbani tu. Kwanza hata useremara wenyewe alikuwa anazuga tu ili miaka isogee aanze kuchapa injili watu watubu dhambi zao wamrudie Mungu.
 
Kama wote walio Comment na kupitia huu uzi wangekuwa waelewa kama wewe, hakika wasingefanya mada rahisi kama hii kuwa complicated na hao ndo wanafanya dini ionekane kama ugonjwa wa akili wakati akili zao ndo tatizo.

Wakuu nadhani inatakiwa mjikite kwenye hili swali kujenga hoja zenu; kama mitume na manabii tunao wafuata katika imani, hawakuwa na skendo zozote katika biashara na kazi zao, kwanini sisi wafuasi wao tumejaa skendo kwenye kazi na biashara zetu??
Mfano wa skendo ni, dhuruma, utapeli, uchawi, wivu, wizi, ufisadi, nongwa, kuuwana na uovu wote mnaoujua.
 
Ndo tulivyo kupenda kukwepesha mambo ya maana
 
Huku ndio nilikuwa nataka kwenda.

Maana hata mitume hawakuwahi kwenda mabarabarani kuhubiri na kukusanya sadaka. Walienda sokoni Kama wafanyabiashara. Mafano Paulo na kushare gospel huku na wao walifanya Biashara halali bila Kuomba Sadaka zamtu.


Mambo ya Sadaka yalifanyikia makanisani.

Kuna vitu wengi wako gizani sana
 
Mkuu Yesu alikuuzia samani gani? wapi? Lini? Sh ngapi?
Kwahiyo alikuwa anachonga alafu anazivundika products zake.?

Daa!!!

Lazima alikuwaana business plan
Marketing na sales stratergy zake
Anatunzahesabu.

Huwezikunielewa Hadi ujifunze mafundisho yake alioanza kufundisha.zile zilikuwa ni lekcha zamtu mwenye uzoefu mkubwa wa industry karibu zote.

Mfano Luka 14:28
Huwezi kutoa hii kauli Kama Hauna uzoefu wa Projects Management.

Na atakuwa amejifunza katika family Business aliyoachiwa na mzee wake kabla hajajikita katika ministry yake.


Yesu ukimuelewa kiupana ni mtamu Sana.
 
Biashara ni nini?
Wanakijiji wamesema Yesu ni Fundi wanamjua maana alikuwa anawatengenezea vitu.

Kwa wayahudi Biashara ilikuwa ni wewe kuuza bidhaa yako, na mnunuzi kutoa pesa. Na inakuwa biashara ilikamilika kwa Yule mpokea fedha kurithika na alichopokea na na alipokea fedha ameridhika.

Win win situation.

Haya Yesu akifanya Sana. Has Mtume akifanya. Ila hakuwa na kashfa.


Hii ni wito kwa wachungaji wasipende Sadaka wakasahau kuwaadibisha waumini Kama Yesu
 
Yesu hakuwahi kuwa mfanyabiashara.
 
Hapana. Yesu asingemkabidhi mama yake kwa jirani yake Familia ya Yohana wakati mume wake alikuwepo.

Inaonekana yeye ndiye alikuwa analisha na kuendesha familia.

Soma kabla hajafa. Mama yake alimtafutia pa kumuacha.
Shida yako una kashifu tu!
 


🀣🀣🀣

Kisa Yusuph Baba yake alikuwa seremala
 
Hao jamaa sijui wanabisha nini, mbona ni akili ya kawaida tu hapo.

Sasa mtu akiwa seremala si ni mfanyabiashara tayari, ni sawa na ubishe kua wale wavuvi sio wafanyabiashara.

Hapo ni vile tu hatujaoneshwa maisha yake ya biashara yalikuaje, labda wangeandika walau kidogo watu wangejifunza kwa matendo na kupunguza dhulma, uchawi na unafiki kwenye biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…