Yesu anaweza kuizuia El Niño. Ukweli huu hapa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Tumeishasikia wataalamu wa hali ya hewa wakisema El Niño kali yaja. Na wameonya tayari kwamba El Niño ya mwaka 2026 imeimarika na inatarajiwa kuwa na nguvu sana. Hali hiyo inaweza kusababisha mafuriko makubwa na kuharibu makazi, barabara nk.

Tunashukuru wenye mamlaka wameishaanza maandalizi ya kukabiliana na El Niño.

Wewe binafsi umejiandaa vipi kukabiliana na El Niño?
Katika maandalizi yote unayofanya, nakushauri uanze sasa kumuomba Mungu aizuie El Niño isije au hata ikija iwe ya kawaida tu, isilete uharibifu katika eneo lako na la majirani zako na nchi yako kwa ujumla.

Ili uone umuhimu wa kuomba, ngoja nikukumbushe habari moja katika Biblia. Imeandikwa katika Marko 4:35-41. Biblia inasema siku moja Yesu alipokuwa ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, dhoruba kubwa ilitokea. Mawimbi yakaanza kuipiga mashua kiasi cha kuhatarisha maisha yao. Wakati huo Yesu alikuwa amelala. Wanafunzi wakamwamsha na kumwambia: "Mwalimu hujali kuona tunazama?" Yesu akainuka, akaukemea upepo na kuiambia bahari: “Nyamaza, utulie.” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

Ni raha sana tukiwa na Yesu na kutambua uwezo alio nao wa kuzuia hata majanga ya asili.

Kwahiyo, pamoja na kwamba wataalamu wameishasema El Niño kali inakuja, bado Yesu anaweza kuuamuru upepo wa El Niño utulie usitudhuru. Yesu hajabadilika. Ni Yeye yule jana na leo na hata milele. Na ameahidi akisema tukiomba neno lolote kwa Jina lake atalifanya (Yohana 14:13). Amesema pia katika Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa.”

Nakukumbusha tena: fanya maandalizi yote unayoweza kufanya ya kukabiliana na El Niño, lakini usisahau pia kuomba na kumwamini Mungu kuwa anaweza kuizuia El Niño isitupige.

Mungu akusaidie kulifanya hilo na akulinde daima. Amen
 
Hakuna tatizo kuomba kwa mtu anayeamini, maombi ni sehemu ya maisha. Lakini kuna tofauti kati ya imani ya kidini na utabiri wa kisayansi. El Niño ni hali ya mfumo wa bahari na anga unaoweza kutabirika kwa kutumia data za kisayansi; si sahihi kusema kwa uhakika kwamba “El Niño kali ya 2026 inakuja” bila kuangalia taarifa rasmi za mamlaka za hali ya hewa.

Na kuhusu Yesu kuizuia, hilo ni suala la imani, hivyo kila mtu ana uhuru wa kuliamini. Lakini maombi hayapaswi kuwa mbadala wa maandalizi. Kama kuna hatari ya mafuriko, tunapaswa kusafisha mifereji, kuepuka kujenga maeneo hatarishi, kulinda chakula na mali, kufuatilia tahadhari za hali ya hewa na kuwa na mpango wa uokoaji.

Kwa kifupi: Omba kama unaamini, lakini pia fanya maandalizi kama unavyoamini kwamba maisha yako yana thamani. Imani na tahadhari vinaweza kwenda pamoja.
 
Super reply
 
Naunga mkono hoja
 
Attachments

  • 1785576123048.jpg
    1785576123048.jpg
    81.3 KB · Views: 19

Chukulia mfano sasa mtu ndio kajenga nyumba yake sehemu ambayo ina mkondo wa maji mwingine kapanga sehemu yenye mkondo wa maji. Unataka huyo mtu aende kuishi wapi na pesa ya kuhama hana. Kuna wakati tunahitaji kumtegemea Mungu na kumwomba msaada wake kwa mambo ambayo yapo juu ya upeo wa akili zetu.
 
si sahihi kusema kwa uhakika kwamba “El Niño kali ya 2026 inakuja” bila kuangalia taarifa rasmi za mamlaka za hali ya hewa.
Sijakurupuka kuandika mada hii kabla ya kuangalia taarifa rasmi za mamlaka ya hali ya hewa. Taarifa ya hivi karibuni ya World Meteorological Organization (WMO), iliyotolewa Septemba 3, 2026, inasema El Niño “is firmly established.” Taarifa hiyo imesema pia El Niño inatarajiwa kuimarika katika miezi ijayo na kuwa “very strong." Hata NOAA Climate Prediction Center ya Marekani, imetoa taarifa kama hiyo hiyo
Lakini maombi hayapaswi kuwa mbadala wa maandalizi. Kama kuna hatari ya mafuriko, tunapaswa kusafisha mifereji, kuepuka kujenga maeneo hatarishi, kulinda chakula na mali, kufuatilia tahadhari za hali ya hewa na kuwa na mpango wa uokoaji.
Soma tena hitimisho la mada yangu, sijasema maombi ni mbadala wa maandalizi, na wala sijasema usifanye maandalizi uliyoyataja. Nimesema: "fanya maandalizi yote unayoweza kufanya ya kukabiliana na El Niño, lakini usisahau pia kuomba na kumwamini Mungu kuwa anaweza kuizuia El Niño isitupige.
 
Kwa mawazo yangu hakuna maombi yatakayosaidia kwenye Hilo kama likiamua kutokea...
 
Naunga mkono hoja
Mkuu elewa hivi, YESU alikuja duniani karne ya kwanza!,mtume alikuja karne ya saba,wakati huo hakukuwa na teknolojia ya kamera,bali huadithiwa tu jinsi watakatifu hawa walivyokuwa wakifanania, mfano mtume wanaeleza alikuwa mrefu,mwenye kifua kipana,mwenye sura ya kupendeza na nywele nyeusi,na ndevu nyingi zilizojaa,alikadhalika YESU naye alihadithiwa hivyo pia,watafiti walijarimu kua assume tu,au kufananisha,but ukweli sura halisi bado kujulikana za watakatifu wote hawa wawili.
 
Chukulia mfano sasa mtu ndio kajenga nyumba yake sehemu ambayo ina mkondo wa maji mwingine kapanga sehemu yenye mkondo wa maji. Unataka huyo mtu aende kuishi wapi na pesa ya kuhama hana. Kuna wakati tunahitaji kumtegemea Mungu na kumwomba msaada wake kwa mambo ambayo yapo juu ya upeo wa akili zetu.
Nakubaliana na wewe kwamba kuna mazingira ambayo mtu hana uwezo wa kuyatatua kwa nguvu zake mwenyewe, na hapo imani na maombi vina nafasi yake. Mtu aliyekwisha jenga au kupanga sehemu yenye mkondo wa maji hawezi kuambiwa tu “hama” wakati hana uwezo huo.

Lakini hapo ndipo tunapopaswa kutofautisha kumtegemea Mungu na kuacha kuchukua tahadhari. Anaweza kuomba Mungu amlinde, huku akitafuta njia yoyote ya kupunguza hatari, kufuatilia tahadhari za mafuriko, kuhamisha vitu muhimu sehemu salama, kuwa na mpango wa dharura na kushirikiana na majirani.

Kwa hiyo hoja si kwamba “usiombe, chukua hatua.” Hoja ni omba na chukua hatua pale unapoweza; na pale jambo likiwa nje ya uwezo wako, ndipo unamwachia Mungu.
 
Tumeishasikia wataalamu wa hali ya hewa wakisema El Niño kali yaja. Na wameonya tayari kwamba El Niño ya mwaka 2026 imeimarika na inatarajiwa kuwa na nguvu sana. Hali hiyo inaweza kusababisha mafuriko makubwa na kuharibu makazi, barabara nk.

Tunashukuru wenye mamlaka wameishaanza maandalizi ya kukabiliana na El Niño.

Wewe binafsi umejiandaa vipi kukabiliana na El Niño?
Katika maandalizi yote unayofanya, nakushauri uanze sasa kumuomba Mungu aizuie El Niño isije au hata ikija iwe ya kawaida tu, isilete uharibifu katika eneo lako na la majirani zako na nchi yako kwa ujumla.

Ili uone umuhimu wa kuomba, ngoja nikukumbushe habari moja katika Biblia. Imeandikwa katika Marko 4:35-41. Biblia inasema siku moja Yesu alipokuwa ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, dhoruba kubwa ilitokea. Mawimbi yakaanza kuipiga mashua kiasi cha kuhatarisha maisha yao. Wakati huo Yesu alikuwa amelala. Wanafunzi wakamwamsha na kumwambia: "Mwalimu hujali kuona tunazama?" Yesu akainuka, akaukemea upepo na kuiambia bahari: “Nyamaza, utulie.” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

Ni raha sana tukiwa na Yesu na kutambua uwezo alio nao wa kuzuia hata majanga ya asili.

Kwahiyo, pamoja na kwamba wataalamu wameishasema El Niño kali inakuja, bado Yesu anaweza kuuamuru upepo wa El Niño utulie usitudhuru. Yesu hajabadilika. Ni Yeye yule jana na leo na hata milele. Na ameahidi akisema tukiomba neno lolote kwa Jina lake atalifanya (Yohana 14:13). Amesema pia katika Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa.”

Nakukumbusha tena: fanya maandalizi yote unayoweza kufanya ya kukabiliana na El Niño, lakini usisahau pia kuomba na kumwamini Mungu kuwa anaweza kuizuia El Niño isitupige.

Mungu akusaidie kulifanya hilo na akulinde daima. Amen
Kwani el nino inaletwa na nani
? Nashauri badala ya kuanza maombi ebu Tu deal na mleta El nino.
 
Sijakurupuka kuandika mada hii kabla ya kuangalia taarifa rasmi za mamlaka ya hali ya hewa. Taarifa ya hivi karibuni ya World Meteorological Organization (WMO), iliyotolewa Septemba 3, 2026, inasema El Niño “is firmly established.” Taarifa hiyo imesema pia El Niño inatarajiwa kuimarika katika miezi ijayo na kuwa “very strong." Hata NOAA Climate Prediction Center ya Marekani, imetoa taarifa kama hiyo hiyo

Soma tena hitimisho la mada yangu, sijasema maombi ni mbadala wa maandalizi, na wala sijasema usifanye maandalizi uliyoyataja. Nimesema: "fanya maandalizi yote unayoweza kufanya ya kukabiliana na El Niño, lakini usisahau pia kuomba na kumwamini Mungu kuwa anaweza kuizuia El Niño isitupige.
Hapo nakubaliana na wewe. Kama WMO na NOAA wametoa tahadhari hizo, basi msingi wa kusema kuna uwezekano wa El Niño kuimarika upo kwenye taarifa za kisayansi, si kwenye hisia.

Na kuhusu hoja yako ya maombi, nimekusoma tena. Uko wazi kabisa kwamba husemi maombi yachukue nafasi ya maandalizi; unasema tufanye maandalizi yote yanayowezekana huku pia tukimwomba Mungu atulinde. Hilo ni jambo tofauti kabisa na kupuuza tahadhari za wataalamu.

Kwa hiyo tofauti yetu ilikuwa zaidi kwenye namna ya kuwasilisha hoja, si kwenye umuhimu wa maandalizi. Sayansi itusaidie kujua tunachokabiliana nacho, maandalizi yatupunguzie madhara, na kwa mwenye imani, maombi yaende sambamba na yote hayo.
 
Kwa mawazo yangu hakuna maombi yatakayosaidia kwenye Hilo kama likiamua kutokea...
Unasema hivyo kwa sababu labda hujajua nguvu ya maombi. Mimi, Mungu amenifanyia mambo mengi sana baada ya kumuomba. Soma nyuzi zangu za nyuma utathibitisha hilo.
 
Back
Top Bottom