Yesu anaweza kuizuia El Niño. Ukweli huu hapa!

Umeuma kwa picha kisha ukapuliza kwa signature!
My friend, you may only be responsible for what you say, but you are not exempt from the meaning your images/words clearly convey in context.
 
Hiyo husababishwa na tatizo la imani. Ila wengine tunaishi kwa maombi. Na tunaona Mungu akitutendea miujiza mikubwa kupitia maombi. Yapo mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyatatua kwa kutumia akili zake za kawaida za darasani. Hizo biology, chemistry, physics, na geography zilianzishwa zilikuta watu wanaishi kwa maombi. Zilianzishwa ili kuweka kumbukumbu za hatua za kufuata na ili kukumbusha hatua jinsi muujiza ulivyofanywa.
Mkuu Kusema kwamba wengi mnaishi Kwa maombi sio Jambo sahihi au halina ukweli thabiti...Maombi hayasaidii chochote, Imani thabiti yenye utekelezaji ndio Mkombozi wa Kila kitu. Dunia ina Siri moja ambayo wengi hawaifahamu.
 
Hii kauli yako inajichanganya. Unakataa maombi halafu unakubali imani.
Sisi tunaomba halafu tunaamini kuwa Mungu anasikia tunayoomba na atatupatia haja zetu. Maombi na imani vinaenda pamoja
"Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:24)
 
Chukulia mfano sasa mtu ndio kajenga nyumba yake sehemu ambayo ina mkondo wa maji mwingine kapanga sehemu yenye mkondo wa maji. Unataka huyo mtu aende kuishi wapi na pesa ya kuhama hana. Kuna wakati tunahitaji kumtegemea Mungu na kumwomba msaada wake kwa mambo ambayo yapo juu ya upeo wa akili zetu.
Omba kama kila kitu kinategemea Mungu, lakini chukua hatua kama vile Mungu amekupa akili ili uitumie.
 
Yes, Mungu ametupa akili, lakini ameonya tusizitegemee akili zetu wenyewe.
“Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe.” (Mithali 3:5)
 
Hakuna sehemu nimesema tegemea akili zako pekee.
 
Hii kauli yako inajichanganya. Unakataa maombi halafu unakubali imani.
Sisi tunaomba halafu tunaamini kuwa Mungu anasikia tunayoomba na atatupatia haja zetu. Maombi na imani vinaenda pamoja
"Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:24)
Simaanishi Imani hiyo ya kuamini kuwa mungu atajibu, Imani ninayoisemea ni Ile ya utekelezaji wa Jambo, mfano unataka kufanikiwa Jambo kwenye fikra lazima uwe Una uhakika au ujasiri wa kuona kwamba Hapa Mimi nitafanikiwa ni suala la muda Tu, hii ndio Imani ninayosemea Mimi, na hii Imani ndio ufunguo wa Milango yote duniani, ukiwa Huna doubt na unachokifanya basi kufanikiwa ni nje nje....Hakuna Jamii yyte ile iliyofanikiwa bila kuwa responsible....
 
Hakuna sehemu nimesema tegemea akili zako pekee.
We umesema: "Omba kama kila kitu kinategemea Mungu..."
Nilivyoielewa hiyo kauli yako ni kwamba unamaanisha kuna mambo ya kuomba na mengine sio ya kuomba ni ya kutumia akili tu. If so, hili andiko unalielewaje?
“Msijisumbue kwa neno lo lote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” (Wafilipi 4:6)
 
Simaanishi Imani hiyo ya kuamini kuwa mungu atajibu, Imani ninayoisemea ni Ile ya utekelezaji wa Jambo, mfano unataka kufanikiwa Jambo kwenye fikra lazima uwe Una uhakika au ujasiri wa kuona kwamba Hapa Mimi nitafanikiwa ni suala la muda Tu, hii ndio Imani ninayosemea Mimi, na hii Imani ndio ufunguo wa Milango yote duniani, ukiwa Huna doubt na unachokifanya basi kufanikiwa ni nje nje....Hakuna Jamii yyte ile iliyofanikiwa bila kuwa responsible....
Reference yako ni kitabu gani? Labda tuanzie hapo kwanza
 
We umesema: "Omba kama kila kitu kinategemea Mungu..."
Nilivyoielewa hiyo kauli yako ni kwamba unamaanisha kuna mambo ya kuomba na mengine sio ya kuomba ni ya kutumia akili tu. If so, hili andiko unalielewaje?
“Msijisumbue kwa neno lo lote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” (Wafilipi 4:6)
Hapana, hujanielewa vizuri.
Sikusema kuna mambo ambayo hayaruhusiwi kuombewa. Nilichosema ni kwamba kuomba hakumwondolei mwanadamu wajibu wa kutumia akili na kuchukua hatua.

Je, Biblia inaposema tuombe, inamaanisha tusifanye chochote baada ya kuomba?

Yakobo 2:17 inasema, “Imani isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.”

Nehemia 4:9 inasema: “Tukamwomba Mungu wetu, tena tukaweka walinzi…”

Angalia hapo, waliomba Mungu, lakini pia wakaweka walinzi. Hawakusema, “Kwa kuwa tumeomba, basi hatuhitaji tahadhari.

Ukiishi kwenye nyumba iliyo kwenye mkondo wa maji, omba Mungu akulinde lakini pia tafuta namna ya kujikinga na mafuriko. Ukiona hatari, kuchukua hatua si kukosa imani.

Maombi si mbadala wa hekima; maombi na hekima vinaweza kwenda pamoja.

Na kama tunataka kutumia Wafilipi 4:6 kwa maana kwamba kila jambo tumuombe Mungu na hivyo tusihitaji kufanya juhudi yoyote, basi tutakuwa tunapuuza maandiko mengine mengi yanayotutaka tufanye kazi, tutumie hekima, tujilinde na kuchukua hatua.
 
Ije tuheshimiane
Lol, ni nani tena amekuvunjia heshima? Hiyo avatar yako tu inaonesha unastahili heshima kubwa, kwakuwa hizo ndevu nyeupe hazipatikani kirahisi, ni mpaka mtu uwe umekula chumvi nyingi sana.
Mimi Biblia yangu inaniambia hivi:
Rum 13:7
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
 
Hapana, hujanielewa vizuri.
Sikusema kuna mambo ambayo hayaruhusiwi kuombewa. Nilichosema ni kwamba kuomba hakumwondolei mwanadamu wajibu wa kutumia akili na kuchukua hatua.

Je, Biblia inaposema tuombe, inamaanisha tusifanye chochote baada ya kuomba?

Yakobo 2:17 inasema, “Imani isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.”

Nehemia 4:9 inasema: “Tukamwomba Mungu wetu, tena tukaweka walinzi…”

Angalia hapo, waliomba Mungu, lakini pia wakaweka walinzi. Hawakusema, “Kwa kuwa tumeomba, basi hatuhitaji tahadhari.

Ukiishi kwenye nyumba iliyo kwenye mkondo wa maji, omba Mungu akulinde lakini pia tafuta namna ya kujikinga na mafuriko. Ukiona hatari, kuchukua hatua si kukosa imani.

Maombi si mbadala wa hekima; maombi na hekima vinaweza kwenda pamoja.

Na kama tunataka kutumia Wafilipi 4:6 kwa maana kwamba kila jambo tumuombe Mungu na hivyo tusihitaji kufanya juhudi yoyote, basi tutakuwa tunapuuza maandiko mengine mengi yanayotutaka tufanye kazi, tutumie hekima, tujilinde na kuchukua hatua.
Nilishindwa kukuelewa kwa sababu ya matumizi ya neno "kama" kwenye kauli yako ya mwanzo. Vinginevyo tuko pamoja. Tuombe na tuchukue tahadhari.
 
Kama ni ghazabu ya Mwenyezi Mungu maombi hayawezi kusaidia labda toba ya kweli.Mind you toba sio maombi bali ni kukubali makosa yenu na kubadili mienendo yenu na huruma ya Mwenyezi Mungu inaweza kuwa juu yenu.

Kama ni majanga na mabadiliko ya tabia ya nchi kama wasemavyo wanamazingira na watu wasayansi basi kuweni wapole.

Kabla ya kuombea majanga yasitokee kumbuka ilikubidi kuombea haki itamalaki na dhuluma ziishe tofauti na hapo sala zenu zinaweza geuzwa kelele na mkaangamizwa.
 
Reference yako ni kitabu gani? Labda tuanzie hapo kwanza
Kitabu ni maandishi tu ambayo hata ww unaweza kuandika na watu wakafuata...Sina Haja ya kitabu Kwani uzoefu wangu abroad ni kitabu tosha.
 
Kama ni ghazabu ya Mwenyezi Mungu maombi hayawezi kusaidia labda toba ya kweli.
Usichanganye masomo.
Unakumbuka ghadhabu ya Mungu juu ya Sodoma? Ibrahimu alifanya nini? Aliomba au alifanya toba?
Soma vizuri Mwanzo 18:22–33
Halafu ukumbuke maombi yanayoleta matokeo ni ya mtu asiyewaza maovu. Ni ya mtu ambaye tayari ametubu. Kwa maneno mengine, wito huu wa maombi ni kwa watu wanaoishi maisha matakatifu. Wanaofanya dhambi ndio wanaopaswa kutubu kwanza kisha ndio waombe.
Yakobo 5:16
“Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.”

1 Petro 3:12
“Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao; bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.”

1 Yohana 3:21–22
“Wapenzi, mioyo yetu isipokuwa na hatia, tuna ujasiri kwa Mungu; na lo lote tuombalo twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.”
 
Kitabu ni maandishi tu ambayo hata ww unaweza kuandika na watu wakafuata...Sina Haja ya kitabu Kwani uzoefu wangu abroad ni kitabu tosha.
Nope. Kuna maandishi na Maandishi yenye pumzi ya Mungu. Mimi reference yangu ni Maandishi yenye pumzi ya Mungu. Yaani yaliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu mwenyewe.
“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.” (2 Timotheo 3:16)
 
Back
Top Bottom