Yesu anaweza kuizuia El Niño. Ukweli huu hapa!

Yesu anaweza kuizuia El Niño. Ukweli huu hapa!

Nionapo haya, najua YESU ANAKUJA! umejiandaje ndio swali la kila mtu kujihoji.....
 
Hapo nakubaliana na wewe. Kama WMO na NOAA wametoa tahadhari hizo, basi msingi wa kusema kuna uwezekano wa El Niño kuimarika upo kwenye taarifa za kisayansi, si kwenye hisia.

Na kuhusu hoja yako ya maombi, nimekusoma tena. Uko wazi kabisa kwamba husemi maombi yachukue nafasi ya maandalizi; unasema tufanye maandalizi yote yanayowezekana huku pia tukimwomba Mungu atulinde. Hilo ni jambo tofauti kabisa na kupuuza tahadhari za wataalamu.

Kwa hiyo tofauti yetu ilikuwa zaidi kwenye namna ya kuwasilisha hoja, si kwenye umuhimu wa maandalizi. Sayansi itusaidie kujua tunachokabiliana nacho, maandalizi yatupunguzie madhara, na kwa mwenye imani, maombi yaende sambamba na yote hayo.
Amen, tuko pamoja
 
Chukulia mfano sasa mtu ndio kajenga nyumba yake sehemu ambayo ina mkondo wa maji mwingine kapanga sehemu yenye mkondo wa maji. Unataka huyo mtu aende kuishi wapi na pesa ya kuhama hana. Kuna wakati tunahitaji kumtegemea Mungu na kumwomba msaada wake kwa mambo ambayo yapo juu ya upeo wa akili zetu.
Umetoa mfano mzuri sana.
 
Unasema hivyo kwa sababu labda hujajua nguvu ya maombi. Mimi, Mungu amenifanyia mambo mengi sana baada ya kumuomba. Soma nyuzi zangu za nyuma utathibitisha hilo.
Mimi ni muumini wa Ku take responsibility. Mimi pia nimethibitisha binafsi kuwa maombi hayasaidii chochote, lazima uwe mtu wa kutenda Kwa usahihi ndio unafanikiwa...Hakuna namna yoyote Ile jamii inaweza kutoboa Kwa kufanya maombi, kinachofanya ionekana maombi yamejibiwa ni Ile Imani tu mtu aliyokuwa nayo.
 
Mimi ni muumini wa Ku take responsibility. Mimi pia nimethibitisha binafsi kuwa maombi hayasaidii chochote, lazima uwe mtu wa kutenda Kwa usahihi ndio unafanikiwa...Hakuna namna yoyote Ile jamii inaweza kutoboa Kwa kufanya maombi, kinachofanya ionekana maombi yamejibiwa ni Ile Imani tu mtu aliyokuwa nayo.
Hiyo husababishwa na tatizo la imani. Ila wengine tunaishi kwa maombi. Na tunaona Mungu akitutendea miujiza mikubwa kupitia maombi. Yapo mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyatatua kwa kutumia akili zake za kawaida za darasani. Hizo biology, chemistry, physics, na geography zilianzishwa zilikuta watu wanaishi kwa maombi. Zilianzishwa ili kuweka kumbukumbu za hatua za kufuata na ili kukumbusha hatua jinsi muujiza ulivyofanywa.
 
.
 

Attachments

  • Screenshot_20260906_205959_Gallery.jpg
    Screenshot_20260906_205959_Gallery.jpg
    180.9 KB · Views: 8
Tumeishasikia wataalamu wa hali ya hewa wakisema El Niño kali yaja. Na wameonya tayari kwamba El Niño ya mwaka 2026 imeimarika na inatarajiwa kuwa na nguvu sana. Hali hiyo inaweza kusababisha mafuriko makubwa na kuharibu makazi, barabara nk.

Tunashukuru wenye mamlaka wameishaanza maandalizi ya kukabiliana na El Niño.

Wewe binafsi umejiandaa vipi kukabiliana na El Niño?
Katika maandalizi yote unayofanya, nakushauri uanze sasa kumuomba Mungu aizuie El Niño isije au hata ikija iwe ya kawaida tu, isilete uharibifu katika eneo lako na la majirani zako na nchi yako kwa ujumla.

Ili uone umuhimu wa kuomba, ngoja nikukumbushe habari moja katika Biblia. Imeandikwa katika Marko 4:35-41. Biblia inasema siku moja Yesu alipokuwa ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, dhoruba kubwa ilitokea. Mawimbi yakaanza kuipiga mashua kiasi cha kuhatarisha maisha yao. Wakati huo Yesu alikuwa amelala. Wanafunzi wakamwamsha na kumwambia: "Mwalimu hujali kuona tunazama?" Yesu akainuka, akaukemea upepo na kuiambia bahari: “Nyamaza, utulie.” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

Ni raha sana tukiwa na Yesu na kutambua uwezo alio nao wa kuzuia hata majanga ya asili.

Kwahiyo, pamoja na kwamba wataalamu wameishasema El Niño kali inakuja, bado Yesu anaweza kuuamuru upepo wa El Niño utulie usitudhuru. Yesu hajabadilika. Ni Yeye yule jana na leo na hata milele. Na ameahidi akisema tukiomba neno lolote kwa Jina lake atalifanya (Yohana 14:13). Amesema pia katika Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa.”

Nakukumbusha tena: fanya maandalizi yote unayoweza kufanya ya kukabiliana na El Niño, lakini usisahau pia kuomba na kumwamini Mungu kuwa anaweza kuizuia El Niño isitupige.

Mungu akusaidie kulifanya hilo na akulinde daima. Amen
Asante sana Mkuu. Hapa nimepata mawili
1. Maandalizi ya kujihami dhidi ya Elnino
2. Kufanya maombi kwa Mungu ili kuzuia kabisa au pengine maandalizi yetu yakifeli tusipate madhara.
 
Ikitokea hii betting imekubali Atheists watanyanyaswa sana hapa Jukwaani
 
Asante sana Mkuu. Hapa nimepata mawili
1. Maandalizi ya kujihami dhidi ya Elnino
2. Kufanya maombi kwa Mungu ili kuzuia kabisa au pengine maandalizi yetu yakifeli tusipate madhara.
Sawa kabisa, tuko pamoja
 
Back
Top Bottom