Seth saint
JF-Expert Member
- Oct 27, 2020
- 2,262
- 5,885
Kwamba El nino inakuja kwa watenda zambi sio? Unadhani El nino ikifika inachagua familia za watakatifu tu au wadhambi tu.Usichanganye masomo.
Unakumbuka ghadhabu ya Mungu juu ya Sodoma? Ibrahimu alifanya nini? Aliomba au alifanya toba?
Soma vizuri Mwanzo 18:22–33
Halafu ukumbuke maombi yanayoleta matokeo ni ya mtu asiyewaza maovu. Ni ya mtu ambaye tayari ametubu. Kwa maneno mengine, wito huu wa maombi ni kwa watu wanaoishi maisha matakatifu. Wanaofanya dhambi ndio wanaopaswa kutubu kwanza kisha ndio waombe.
Yakobo 5:16
“Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.”
1 Petro 3:12
“Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao; bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.”
1 Yohana 3:21–22
“Wapenzi, mioyo yetu isipokuwa na hatia, tuna ujasiri kwa Mungu; na lo lote tuombalo twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.”
Kama ambavyo jua uwaka kwa watu wote bila kujali usafi au uchafu wako ndivyo itakavyokuwa El nino.Ghazabu ya Mungu ni juu ya ardhi sio familia ya mtu.Kama unadai huko msafi basi unaweza kuwa salama lakini ardhi ikiwa chafu wewe usafi unatoa wapi?
Ukitoa mfano wa Ibrahim inabidi ukumbuke Ibrahim kwa Mungu alionekana vipi,rafiki sio ndio?kuna mtu hapa chini ya jua wakati huu wakuweza kujilinganisha na Ibrahim katika imani na matendo?Hayupo hilo ndio jibu sahihi