Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini

Mkuu hapo umeandika pumba tupu..is better kama hujui bible ukakaa kimya...unatakiwa usome agano la kale vizur ndo utaelewa agano jipya..hapo utajua kuwa Yesu alikufa kwa sababu za kidini na siasa ilikuwa kama passing code...na hata Leo machafuko yote ya kisiasa yanaongozwa na mapambano ya kidini kat ya Yesu na Shetani ila
siasa ndo battle ground
 
Nimeelewa na nimefundishika,naona na wanafunzi wenzangu mpaka sasa tuko pamoja na mwalimu.

Yaani ukiichukulia biblia kama kitabu kingine na si kitakatifu,kuna mengi sana utajifunza maana unakuwa na uwezo wa kukataa vitu kadhaa na hivyo kukupelekea kutafuta zaidi.

Kila atafutaye ataona.
 
Kuna kitu... Nimejifunza ktk somo la imani..... Sio suala la kupinga kwa utashi wa kiimani bora kuleta hoja.. Inayokwenda sambamba na uzi uliopo.... [emoji19][emoji19]
 
ivi kurudi kwa ukawa bungeni kuna weza kuongeza joto la kisiasa bungeni
 
Hakuuuawa kwa sababu za kisiasa bali za kidini.Na ieleweke wazi kuwa waliomwua Yesu SIO WAYAHUDI ni warumi.Askari wa Kirumi (ROMA) ndio waliomwua YesU sio wayahudi.Kitendo cha kuua kilifanywa na warumi

Kisa cha Yesu kuuawa ni kuwa Kulikuwa na wivu mkubwa wa kidini kati yake na viongozi wa dini alizozikuta.Walilalamika kuwa watu wengi wanamfuata yeye na kumsikiliza yeye kuliko wao.Alikuwa na wafuasi wengi kuliko mafarisayo na masadukayo.Wivu huo wa kidini ambao uko hadi leo ambapo dini mbali mbali hupigania kuwa na wafuasi wengi na dini moja ikichukua wafuasi wa dini ingine viongozi hutangaziana vita kama wakati ule wa Yesu na kusulubiana kwa maneno,kejeli,matusi nk

Kesi ya YESU ni aibu kwa fani ya Sheria

Kesi ya Yesu kuuawa ilivinja sheria zote.

Kwa mfano ukisoma Biblia utashangaa Yesu alikamatwa usiku akisali kanisani kwake porini kwenye milima ya mizeituni akiomba na wanafunzi wake ambao kwa sababu ya usingizi walikuwa wakilalala hawasali.Walimshika ndani ya kanisa lake porini ambako akitekeleza ibada yake na wanafunzi wake akitumia uhuru nwake wa kuabudu.Usiku haukuwa muda wa kazi.Kwa hiyo kisheria haikuwa sahihi kwao.Pia haikuwa sahihi kumshika akiwa ibadani kwenye chaka ambalo ndio lilikuwa hekalu lake la kuabudia

Pili aliburuzwa kwenye mahakama zao usiku.Katika historia ya sheria hakuna popote mahakama iliwahi fanya vikao vyao usiku mida isiyo ya kazi na majaji wakaendesha kesi

Tatu Kazi ya askari ni kumlinda mtuhumiwa anapopelekwa kwenye mashtaka lakini Yesu alipokuwa akipelekwa mahakamani watu walikuwa wakimzonga ,kumpiga na kumtemea mate mbele ya macho ya askari wa kirumi bila askari hao kuchukua hatua zozote

Nne alipokuwa mahakamani Askari walifanya kitendo cha kihuni alipokuwa akihojiwa na Jaji Alipokuwa akijibizana na jaji askari alimzaba kibao Yesu NDANI YA mahakama kazi ambayo si yake.Huyo askari alivunja sheria ya mahakama mbele ya jaji na jaji hakumchukulia hatua wala jeshi lake halikumchukulia hatua.

Tano,hukumu aliyotoa jaji mrumi Ponsio PILATO ilikuwa ya kihuni na haikubaliki kisheria.Alipohukumu aliuliza umati uliokuwepo mahakamani nimfanyie nini Yesu huyu? Umati ukajibu asulubiwe ,asulubiwe na akakubali na kumhukumu.Kisheria Jaji anatakiwa aangalie sheria zinasemaje kwenye vitabu vyake sio aulize waliohudhuria kusikiliza kesi mahakamani.Katika majaji wajinga waliowahi tokea duniani Ponsio pilato ndio jaji mjinga nambari wani

Sita,aliposulubiwa na kufa Askari maruhuni wa Kirumi WALIGAWANA mavazi yake.Mavazi ni mali ya mtu.Akifa mirathi huwa inatangazwa ili wapatikane warithi kisheria wachukue hizo mali.Lakini za Yesu baada ya kukata roho tu askari wa kirumi waligawiana mirathi pale pale bila kibali cha kisheria.

Nini cha kufanya??? Wakristo waliburuze serikali ya Italia (Waitaliano) iwalipe fidia kwa kumwua mtu wao na wadai mali zile walizogawana bila kibali cha mahakama wazirudishe na riba juu.

Pia waidai serikali ya Italia ambayo ndio iliyoteua ponsio Pilato ilipe fidia wakristo na waiombe ifukue maiti ya Ponsio Pilato ihukumiwe upya na jopo la majaji

Yesu alihukumiwa kufa na jaji mrumi Ponsio Pilato NA akauawa na askari wa Kirumi kwa hiyo warumi wana kesi ya kujibu kuhusiana na kifo cha Yesu
 
Mkuu umekosea hapo uliposema kwa sababu ya siasa na wala sio dini.

Dini maana yake ni njia ya maisha (way of life) humo kuna kila kitu kuna elimu, afya,siasa,uchumi, sheria n.k

Siasa maana yake ni kusimamia watu hapa tunasema utawala. Siasa neno la kiarabu lililotokana na neno siyasiya.
Hivyo unapotofautisha siasa na dini utakuwa unalisha watu matango pori.
 
Mkuu hapo umeandika pumba tupu..is better kama hujui bible ukakaa kimya...unatakiwa usome agano la kale vizur ndo utaelewa agano jipya..hapo utajua kuwa Yesu alikufa kwa sababu za kidini na siasa ilikuwa kama passing code...na hata Leo machafuko yote ya kisiasa yanaongozwa na mapambano ya kidini kat ya Yesu na Shetani ila
siasa ndo battle ground
Nakushukuru kwa kuuelezea uelewa wako katika hili, lakini pia nasikitika kwa vile umetumia uelewa wako kuukandamiza uelewa wangu tena kwa lugha kali, rejea aya ya kwanza kabisa ya uchambuzi wangu mkuu.
 
Heshima kwako mleta uzi,mie nafarijika sana kwenye maisha yangu ninapokutana na "Great thinker" kama wewe... hakika umeni boost ubongo wangu! mie niruhusu nikuite BUDDHA.
Hahaha mkuu, tuendelee kusoma na kujifunza kwa kutafakari.
 
Hakuuuawa kwa sababu za kisiasa bali za kidini.Na ieleweke wazi kuwa waliomwua Yesu SIO WAYAHUDI ni warumi.Askari wa Kirumi (ROMA) ndio waliomwua YesU sio wayahudi.Kitendo cha kuua kilifanywa na warumi

Kisa cha Yesu kuuawa ni kuwa Kulikuwa na wivu mkubwa wa kidini kati yake na viongozi wa dini alizozikuta.Walilalamika kuwa watu wengi wanamfuata yeye na kumsikiliza yeye kuliko wao.Alikuwa na wafuasi wengi kuliko mafarisayo na masadukayo.Wivu huo wa kidini ambao uko hadi leo ambapo dini mbali mbali hupigania kuwa na wafuasi wengi na dini moja ikichukua wafuasi wa dini ingine viongozi hutangaziana vita kama wakati ule wa Yesu na kusulubiana kwa maneno,kejeli,matusi nk

Kesi ya YESU ni aibu kwa fani ya Sheria

Ukiangalia hata mashtaka yake yalianzia ndani ya dini na yalivunja sheria zote.
Kwa mfano ukisoma utashangaa Yesu alikamatwa usiku akiwa akisali kanisani kwake porini akiomba na wanafunzi wake.Walimshika ndani ya kanisa lake na akitekeleza ibada yake na wanafunzi wake.Usiku haukuwa muda wa kazi.Kwa hiyo kisheria haikuwa sahihi kwao.

Pili aliburuzwa kwenye mahakama zao usiku.Katika historia ya sheria hakuna popote mahakama iliwahi fanya vikao vyao usiku mida isiyo ya kazi na majaji wakaendesha kesi

Tatu Kazi ya askari ni kumlinda mtuhumiwa anapopelekwa kwenye mashtaka lakini Yesu alipokuwa akipelekwa mahakamani watu walikuwa wakimzonga ,kumpiga na kumtemea mate mbele ya macho ya askari bila kuchukua hatua zozote

Nne alipokuwa mahakamani Askari walifanya kitendo cha kihuni alipokuwa akihojiwa na Jaji Alipokuwa akijibizana na jaji askari alimzaba kibao Yesu NDANI YA mahakama kazi ambayo si yake.Huyo askari alivunja sheria ya mahakama mbele ya jaji na jaji hakumchukulia hatua wala jeshi lake halikumchukulia hatua.

Tano,hukumu aliyotoa jaji mrumi Ponsio PILATO ilikuwa ya kihuni na haikubaliki kisheria.Alipohukumu aliuliza umati uliokuwepo mahakamani nimfanyie nini Yesu huyu? Umati ukajibu asulubiwe ,asulubiwe na akakubali na kumhukumu.Kisheria Jaji anatakiwa aangalie sheria zinasemaje sio aulize waliohudhuria mahakamani.Katika majaji wajinga waliowahi tokea duniani Ponsio pilato ndio jaji mjinga nambari wani

Sita,aliposulubiwa na kufa Askari maruhuni wa Kirumi WALIGAWANA mavazi yake.Mavazi ni mali ya mtu.Akifa mirathi huwa inatangazwa ili wapatikane warithi kisheria wachukue hizo mali.Lakini za Yesu baada ya kukata roho tu askari wa kirumi waligawiana mirathi pale pale bila kibali cha kisheria.

Nini cha kufanya??? Wakristo waliburuze serikali ya Italia (Waitaliano) iwalipe fidia kwa kumwua mtu wao na wadai mali zile walizogawana bila kibali cha mahakama wazirudishe na riba juu.

Pia waidai serikali ya Italia ambayo ndio iliyoteua ponsio Pilato iilipe fidia wakristo na waiombe ifukue maiti ya Ponsio Pilato ihukumiwe upya na jopo la majaji

Yesu alihukumiwa kufa na jaji mrumi Ponsio Pilato NA akauawa na askari wa Kirumi kwa hiyo warumi wana kesi ya kujibu kuhusiana na kifo cha Yesu
1. Serikali iliyotoa hukumu ya Yesu leo hii haipo na hakuna mamlaka yake hapa duniani, ilianguka na kufutika miaka mingi iliyopita, rejea historia ( The fall of Roman Empire), Italia kama ulivyowatuhumu hawahusiki katika hili.

2. Swala la Tuhuma za nani hasa wa kumlaumu kuhusiana na kifo cha Yesu kati ya wayahudi na Warumi bado Ni DEBATE, kuna wanaowatuhumu wayahudi kwa 80℅ na wapo wengine ikiwa pamoja na wewe mkuu mnaowatuhumu warumi.

3. Kuhusu uvunjwaji wa sheria katika hukumu ya Yesu pamoja na muda hukumu yake ilipotolewa, waliovunja sheria sio warumi bali ni wayahudi ndiyo walivunja sheria zao(JEWS LAW) kwa kumuhukumu Yesu usiku kwa usiku, ila kwa Pilato walimpeleka Asubuhi.
 
Hakuuuawa kwa sababu za kisiasa bali za kidini.Na ieleweke wazi kuwa waliomwua Yesu SIO WAYAHUDI ni warumi.Askari wa Kirumi (ROMA) ndio waliomwua YesU sio wayahudi.Kitendo cha kuua kilifanywa na warumi

Kisa cha Yesu kuuawa ni kuwa Kulikuwa na wivu mkubwa wa kidini kati yake na viongozi wa dini alizozikuta.Walilalamika kuwa watu wengi wanamfuata yeye na kumsikiliza yeye kuliko wao.Alikuwa na wafuasi wengi kuliko mafarisayo na masadukayo.Wivu huo wa kidini ambao uko hadi leo ambapo dini mbali mbali hupigania kuwa na wafuasi wengi na dini moja ikichukua wafuasi wa dini ingine viongozi hutangaziana vita kama wakati ule wa Yesu na kusulubiana kwa maneno,kejeli,matusi nk

Kesi ya YESU ni aibu kwa fani ya Sheria

Ukiangalia hata mashtaka yake yalianzia ndani ya dini na yalivunja sheria zote.
Kwa mfano ukisoma utashangaa Yesu alikamatwa usiku akiwa akisali kanisani kwake porini akiomba na wanafunzi wake.Walimshika ndani ya kanisa lake na akitekeleza ibada yake na wanafunzi wake.Usiku haukuwa muda wa kazi.Kwa hiyo kisheria haikuwa sahihi kwao.

Pili aliburuzwa kwenye mahakama zao usiku.Katika historia ya sheria hakuna popote mahakama iliwahi fanya vikao vyao usiku mida isiyo ya kazi na majaji wakaendesha kesi

Tatu Kazi ya askari ni kumlinda mtuhumiwa anapopelekwa kwenye mashtaka lakini Yesu alipokuwa akipelekwa mahakamani watu walikuwa wakimzonga ,kumpiga na kumtemea mate mbele ya macho ya askari bila kuchukua hatua zozote

Nne alipokuwa mahakamani Askari walifanya kitendo cha kihuni alipokuwa akihojiwa na Jaji Alipokuwa akijibizana na jaji askari alimzaba kibao Yesu NDANI YA mahakama kazi ambayo si yake.Huyo askari alivunja sheria ya mahakama mbele ya jaji na jaji hakumchukulia hatua wala jeshi lake halikumchukulia hatua.

Tano,hukumu aliyotoa jaji mrumi Ponsio PILATO ilikuwa ya kihuni na haikubaliki kisheria.Alipohukumu aliuliza umati uliokuwepo mahakamani nimfanyie nini Yesu huyu? Umati ukajibu asulubiwe ,asulubiwe na akakubali na kumhukumu.Kisheria Jaji anatakiwa aangalie sheria zinasemaje sio aulize waliohudhuria mahakamani.Katika majaji wajinga waliowahi tokea duniani Ponsio pilato ndio jaji mjinga nambari wani

Sita,aliposulubiwa na kufa Askari maruhuni wa Kirumi WALIGAWANA mavazi yake.Mavazi ni mali ya mtu.Akifa mirathi huwa inatangazwa ili wapatikane warithi kisheria wachukue hizo mali.Lakini za Yesu baada ya kukata roho tu askari wa kirumi waligawiana mirathi pale pale bila kibali cha kisheria.

Nini cha kufanya??? Wakristo waliburuze serikali ya Italia (Waitaliano) iwalipe fidia kwa kumwua mtu wao na wadai mali zile walizogawana bila kibali cha mahakama wazirudishe na riba juu.

Pia waidai serikali ya Italia ambayo ndio iliyoteua ponsio Pilato iilipe fidia wakristo na waiombe ifukue maiti ya Ponsio Pilato ihukumiwe upya na jopo la majaji

Yesu alihukumiwa kufa na jaji mrumi Ponsio Pilato NA akauawa na askari wa Kirumi kwa hiyo warumi wana kesi ya kujibu kuhusiana na kifo cha Yesu

Hili la kutaka watu ndio watoe hukumu hadi leo lingalipo.Hata hapa kwetu.Unakumbuka baada ya Makonda kuwasilisha mashitaka kwa "Jaji(Magu)" mintarafu tuhuma za Kabwe "Jaji" alitoa hukumu ya aina gani? Aliwauliza wananchi wa Kigamboni amfanye nini. Ni afadhali hata Yesu kuna mahali alipewa haki ya kujitetea lakini kwa Kabwe yule rafiki yako "Jaji" hakujali kabisa kutoa haki hiyo.Unasemaje sasa ndugu zake Kabwe nao wafungue kesi ya madai?
 
Ahsante mkuu kwa majibu yako. lakini umenifanya nikuulize tena hii namba 2 na 4.
1 Ikiwa Wayahudi wanamjua Mussa tu mbona kwenye vitabu vya dini vinasema manabii wengi ni Wayahudi?
2 Unasema wametumia adhabu ya msalaba kutokana hio ndio adhabu ya Kirumi, kwahio msalaba ni alama ya Kirumi na sio ya kikristo? ikiwa ndio kwanini sasa iwe alama kuu inayotumika kwenye dini ya kikristo?
 
Back
Top Bottom