Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini

Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini

Si lengo wala dhamira yangu kupinga wala kupindisha Imani ya mtu yeyote, bali ni wajibu wangu kama binadamu mwenye akili na upeo wa kudadisi, kuchanganua na kuyaelewa mambo mbalimbali katika namna tofauti tofauti.

Biblia ni kitabu kama vilivyo vitabu vingine vyenye maarifa, tamaduni na vinavyoelezea hisia za jamii za watu wake, isipokua Biblia ni kitabu maarufu kuliko kitabu chochote kilichowahi kuandikwa katika taaluma ya uandishi hapa Duniani.

Uchambuzi wangu utajikita zaidi katika kuelezea kifo cha Yesu Kristo ambaye historia kupitia vitabu mbalimbali vinavyounda kitabu kikuu cha biblia inatueleza kuwa ndiye chanzo cha Dini ya kikisto au kwa lugha ya kigeni dini hiyo inajulikana kama CHRISTIAN yenye tafsiri ya Wafuasi wa Yesu Kristo.

Historia kutoka katika vitabu vya MATHAYO na LUKA inatuambia kua Yesu Kristo alikua MYAHUDI na alizaliwa sehemu ijulikanayo kama BETHLEHEM katika jimbo la JUDEA. Wakati huo sehem kubwa ya Dunia ilikua inatawaliwa na kumilikiwa na UTAWALA WA FALME YA KIRUMI (ROMAN EMPIRE).

Warumi au Waroma walitawala Kwa muda mrefu sana karibu sehem yote ya dunia chini ya wafalme mbalimbali waliofahamika kama KAISARI (CAESAR).

Katika kila jimbo la utawala wa kirumi, likiwemo jimbo alimozaliwa Yesu la JUDEA aliwekwa mtawala na msimamizi mkuu wa serikali ya kirumi, aliyefahamika kwa cheo cha GAVANA. Kipindi cha Yesu Kristo, Gavana wa JUDEA alijulikana kwa jina la PONTIAS PILATE (PONSIO PILATO)', na alikua chini ya Mfalme wa Roma aliyejulikana kama (TIBERIUS CAESAR).

Kazi kubwa ya kwanza ya Gavana wa Roma katika jimbo ilikua ni kulilinda jimbo na utawala wa kiroma kwa nguvu za kijeshi, na ndio maana kila gavana alipewa wanajeshi wasiopungua 3000 kwa kazi hiyo. Kama mwakilishi wa utawala wa kiroma kazi yake nyingine ilikua ni kuhakikisha anakusanya KODI pamoja na kutoa hukumu(mahakama) katika makosa mbalimbali kwa mujibu wa sheria za kiroma.

utawala wa kiroma pia uliwatumia wenyeji wa maeneo wanayoyashikilia katika utawala, hasa katika utawala wa ngazi za chini au serikali za mitaa, waliyatumia makabila mbalimbali, au viongozi wa Dini inayotawala sehemu hiyo. Mfano katika jimbo la Judea na Jerusalem lilikuwepo baraza la Makuhani au Walimu na Viongozi wa dini, baraza hilo lilijulikana kama SANHEDRIN Kwa lugha ya kiyahudi.

SANHEDRIN ni nini?
Historia inatuambia kuwa Waislael waliamriwa na Mungu kuanzisha mahakama ya majaji na mahakimu ambao walipewa mamlaka ya kuwahukumu waisrael wanapokwenda kinyume na matakwa ya Mungu wao kwa mujibu wa sheria walizopewa na Mungu wao. Majaji hao wote walikua ni wale Viongozi wa Dini pamoja na Walimu wa Dini.

Kiongozi mkuu wa kidini (KUHANI MKUU) au kiongozi wa baraza la SANHEDRIN katika jimbo la Judea aliitwa CAIPHAS (KAYAFA). Viongozi wote hawa wa kiyahudi kama historia inavyotuambia walikua chini ya utawala wa Kiroma na walifanya shughuli zao kwa umakini na uwoga pasipo kuitilafiana na watawala wao WARUMI. Na moja ya jukumu lao ilikua ni kuhakikisha haitokei vurugu ya aina yoyote miongoni mwa WAYAHUDI wala mtu anayepingana na utawala wa kirumi, ama sivyo PILATO aliwatishia kuwa atalifunga hekalu lao la kuabudia.

Utawala wa warumi ulikuwa ni wa kibabe na kimabavu sana kiasi kwamba watu walikua wameuchoka na walikua wakisubir siku moja atokee mtu awaokoe katika utawala huo, kwani walichoka kulipa kodi, kuuliwa hovyo na pia kutumikishwa kwa kazi ngumu na utawala huo warumi, kifupi ni kwamba walichoka kutawaliwa.

Yesu Kristo alipoingia Jerusalem, alifanya matukio ambayo yaliwashtua watawala wa mji huo hasa MAFARISAYO au Makuhani, na kuona kua ujio wake unatishia utawala wao na vilevile waliogopa kwamba Yesu Kristo anaweza kuwa chanzo cha vurugu zilizokatazwa na PONSIO PILATO.

Moja ya tukio alilolifanya Yesu lilikua lile la kuvamia hekalu na kuanza kumwaga mwaga bidhaa pamoja na fedha za wafanyabiashara waliokuwemo humo, kitendo hicho kiliamsha shangwe na vigelegele miongoni mwa wayahudi wakimuona kama mkombozi wao katika utumwa huo wa kiroma. Pia Yesu aliongea maneno yaliyoamsha maswali, maneno yaliyoashiria Mapinduzi ya kiutawala. Yesu alisema; mathayo 24:2.

"Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa."

Wafarisayo hao waliona kua huo ni mpango wa kuangusha utawala wao na hivyo wakakubaliana kua Yesu lazima adhibitiwe haraka iwezekanavyo. Na ndio maana hata CIAPHAS (KAYAFA) aliamuru kuwa Yesu akamatwe na ahukumiwe haraka usiku kwa usiku, tena usiku wa manane jambo lililovunja sheria za kiyahudi (JEWISH LAWS) zilizoelekeza hukumu zote kutolewa mchana kweupe tena mbele ya umati wa watu.

Yesu alipokamtwa mwanzoni alituhumiwa kwa kosa la Kupotosha imani ya Dini na Mungu wao kwa maana nyingine alikua ANAKUFURU (BLASPHEMY) kitendo cha Yesu kujitangaza kua.yeye ni mwana wa Mungu na Tayari Maandiko yote waliyoyasubir wayahudi hao kayatimiza ilionekana kua KUFURU kwao, hivyo viongozi hao wa dini waliona wamuadabishe yesu.

Lakini kutokana na kwamba wao hawana mamlaka ya kutoa hukumu bali mwenye mamlaka hayo alikua ni PONTIAS PILATE, iliwaradhimu wampeleke Yesu kwa Pilato. Lakini wazee hao wa baraza la SANHEDRIN walipofika kwa Pilato Walizibadirisha tuhuma na wakamtuhumu Yesu kwamba anachochea mapinduzi ya serikali ya kirumi kwa kuwakataza watu wasilipe kodi kwa KAIZARI na vile vile anajiita MFALME, Jambo ambalo kwa mujibu wa sheria za Roma ilikua ni Uhaini (TREASON). Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha LUKA.

Yesu alimshawishi ZACCHAEUS (ZAKAYO MTOZA USHURU)wa mji wa YERICHO ambae alikua Mkuu wa Watoza ushuru, aache kazi ya kutoza ushuru na amfuate, Yericho, ni mji uliokua ndani ya eneo la ukusanyaji kodi la Pilato. (Luka 19:2-19)

KWA NINI PONTIAS PILATE (PONSIO PILATO) ALIMUHUKUMU YESU JAPO HAKUMKUTA NA KOSA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA KIROMA?

Historia inatuambia kua Pilato alipingana na maelezo ya makuhani na kuyaona kuwa hayana uzito wa adhabu wanayopendekeza Yesu apewe. Alitaka kulithibitisha hilo kwa kumuuliza Yesu maswali ambayo lengo lake ni kuona kama kweli Yesu ni Tishio kwa utawala wa Kirumi. Pilato alimuuliza Yesu,

"Wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamjibu hayo umetamka wewe.
Pilato aliwarudia makuhani na kuwawmbia

Simuoni mtu huyu kua na tuhuma. Makuhani wakamjibu, lakini amevunja sheria, pilato akawaambia, amevunja sheria zenu sio sheria za kaisari.

Pilato alitoa hukumu ya yesu kuteswa mpaka kufa kwa woga wa kutokea vurugu zitakazompelekea kushindwa kutawala, kwani Aliwaza kua kama hatatoa hukumu hiyo kwa Yesu CAIPHAS atampa lawama zote endapo yatatokea machafuko na vurugu ndani ya jimbo lake la utawala. Vile vile aliogopa kuwajibishwa na KAIZARI endapo vurugu zingetokea, angeonekana ameshindwa kutawala.

Yesu alihukumia Kifo (Death Penalty).
Ukichunguza uchambuzi katika maelezo hayo utaona kuwa kulikua na mvutano wa kisiasa katika uongozi wa nani anakubalika zaidi na nani anataka kumpindua nani. Makuhani pamoja na Wazee wa baraza walitishwa kuwa Yesu kaja kuharibu utawala wao na labda walikua wanapata maslahi zaidi kutoka katika utawala wa kirumi hivyo ujio wa Yesu ulikuja kutiachanga katika kitumbua chao.

Upande wa Pilato japo alidai kua hausiki na mauaji ya Yesu kwa kunawa mikono kwa maji kuashiria kua Umwagaji Damu wa Yesu hausiki nao, alisema

"Sina hatia na damu ya mtu huyu, jambo hili ni juu yenu ""

lakini tamaa ya Madaraka ilimsukuma kutoa hukumu hiyo, uwezekano wa yeye kupinga tuhumu na kuamuru Yesu aachiwe huru ulikua mkubwa na ulikua ndani ya uwezo wake kwa sababu Gavana wa kirume kwa kipindi chao alikua yeye ndiye sheria na yeye ndiye mahakama muamuzi wa mwisho. Lakini alihisi kama angefanya hivyo ingekua mwisho wa utawala wake.

Asanteni kwa Kusoma maandishi haya.
(sept.2016)
Mkuu umeeleweka sana...Kifo chake kilikuwa cha kisiasa zaidi...aliponena habari za ukombozi watu walielewa ni ukombozi wa kisiasa kutoka kwa dola la kirumi.Ndio maana alipata wafuasi wengi kenye mikutano yake, watu walimchukulia kama vile kina Nyerere na Mandela walivyowaahidi waafrika uhuru kutoka kwa wakoloni.Ndio maana baada ya kukamatwa na kuteswa kwake, watu wengi walimzomea na kumcheka kwa kushindwa kwenye harakati za kupata uhuru kutoka kwa waroma.

Kama kifo chake kingekuwa cha kidini basi Israel ingekuwa na wakristo wengi zaidi.Kwa ule wingi wa watu waliomfuta kwenye mikutano yake, wangeendeleza dini ya ukristo huko Israel na matokeo yake Israel ingekuwa na wakristo wengi sana.Lakini haipo hivyo kwani Israel wanafuata dini ya kiyaudi na kuna wengine hata Yesu hawamjui zaid ya kumsikia tu.

Baada ya Yesu kufa, hakuonekana hadharani baada ya kufufuka lakini wanafunzi wake walidai kwamba amefufuka na wamemuona.Wale waliomfuata kwenye mikutano wakajiuliza, kama alifia hadharani, kwanini asingejionesha hadharani baada ya kufufuka? wakagoma kuamini.Watu wakahoji je uko wapi ukombozi aliotuahidi? wanafunzi wakajibu kwamba ukombozi ulikuwa wa kiroho na sii wa kisiasa.

Wanafunzi wake walipoanza kuhubiri habari za kufufuka kwa Yesu, walikamatwa na kuteswa kwa sababu waliashiria mapinduzi ya kiutawala na kwa hasira za kukosa ukombozi wakati wa Yesu.
 
Safi sana ndugu... inaonekana ni kweli Yesu aliuliwa kwasababu za kisiasa zaidi,kuliko kidini kama tulivyolishwa tango pori... kwasababu hata mie hua najiulizaga iweje israel iwe na wakristo wachache zaidii kuliko Mbeya?
 
Jibu ni rahisi sana, Israeli wanahoji kitu kwanza kabla ya kukipokea,...wale ni wasomi/wanasayansi so anything without proof does not appeal to them....Ila wabongo wanafuata sana vitu bila kuuliza na kutafakari, hasa kitu kikiwa cha mzungu mbongo atakiona kama kitu kamili kilichojitosheleza kisicho hitaji kuhoji.

Mfano, madhehebu ya kikrosto kama Anglikana, Katoliki na Lutheran yanaheshimiwa na kufuatwa na wengi sababu yalianzishwa na wazungu.Lakini yale ya wabongo kama makanisa ya Lusekelo na Mama Lwakatare yanadharaulika sana na kufuatwa na wachache.Ni rahisi kusikia kanisa la Lwakatare au Lusekelo ya kiitwa ya freemason kuliko kusikia Lutherani au Anglikana wanaitwa hivyo.Hii ni kwa sababu wazungu waliwaaminisha wabongo kwamba kila kinachotoka Africa(KAMA MILA ZA KIAFRIKA) ni cha Shetani na kwamba Mungu anawatumia wao kueleza jinsi gani ya kutekeleza sheria zake.
 
Target nikufika arusha lakini tutafikaje lazima kuwe na sababu.

Lengo kuu ilikuwa ni Yesu asulubiwe .

Vijisababu vitakuwa vingi. Tamaa, uchu wa madaraka nk lakini lengo limetimia tumepata wokovu.

Hakuna mistake kubwa ambayo shetani amewai kuifanya kama kuruusu yesu asulubiwe.

Hiyoo ni strength inatufanya wakristo kudunda.
 
Umeongea vyema
 
Me swali langu je uyahudi ni dini au kabila?
Na pia yesu aliuliwa na wayahudi,waisrael au warumi?
Nini tofauti ya jews na israel?
 
Naomba ufafanuzi kwa mujibu wa hii stori
1 Warumi walikuwa na dini gani kabla ya kuja Yesu?
2 Wayahudi dini waliokuwa wakiifata ililetwa na nabii yupi?
3 Ikiwa Yesu alikwenda kumwaga pesa ya sadaka kwenye HEKALU na WAYAHUDI waliingiwa na wasiwasi wa utawala wa dini yao kwanini isiwe shutuma ya dini na iwe siasa?
4 Mahakama ilio mhukumu Yesu ilikuwa ya dini ya (Wayahudi) au ya siasa(Kirumi)
3. Yesu hakumwaga pesa ya sadaka hekaluni. Alimwaga pesa na bidhaa za wafanyabiashara. kifupi, wajasiriamali walikuwa wamegeuza hekalu kuwa Kariakoo au Tandale. Walikuwa wanafugia hadi mifugo humo kama unavyoona wafuga kuku pale soko la Kisutu (hivi lile soko bado lipo?) na Shekilango.
 
Me swali langu je uyahudi ni dini au kabila?
Na pia yesu aliuliwa na wayahudi,waisrael au warumi?
Nini tofauti ya jews na israel?
Nitaongelea kipengele kimoja cha wayahudi na waisrael kwa sasa.
katika historia ya makabila yale kumi na mbili (au kumi na tatu) maana kabila la Yusufu liliwakilishwa na wanae wawili, Manase na Efraim, yaligawanyika na kuunda falme mbili. Ufalme wa kusini uliitwa Yudea (Judah) na uliundwa na makabila mawili: Kabila la Yuda na kabila la Benjamin. Nadhani hawa ndio Jews (I stand to be 'collected', sorry..to be corrected).

Makabila mengine kama Asheri, Dani, Gadi, Naftali, Zebuloni, Simeoni, Rubeni, Isakari, Efraimu na Manase yaliunda Ufalme wa Kaskazini ulioitwa Waisrael (Israelites). Inasemekana kabila la Lewi (Walawi) halikuwa na makao maalum, lilisambaa kote kote miongoni mwa makabile yale mengine hivyo halikuwa na mji wake.

Hayo makabila yaliyounda ufalme wa kaskazini ndiyo yalishambuliwa na mnamo karne kama ya nane BC na kuangushwa na watu wote kuchukuliwa mateka na baadaye kuwa integrated kwenye miji mingine ya ufalme wa Ashuru (Assyria) 2Wafalme 17. Hayo ndiyo makabila ya Israel ambayo inasemekana yamepotea maana hawakurudi tena kwenye nchi yao. Kwa maana hiyo, hata wale ambao walikumbana na panga la Hitler, walikuwa wayuda/Jews/Judah people maana wale wengine hawakupata kusikika tena. Nasikia siku hizi kuna juhudi za kutafuta The Lost Tribes of Israel, sijui kama zitafanikiwa.
 
Kwa uelewa wako na huyu Herode tunamsikia na kumsoma yeye alikuwa nani katika utawala wa kirumi, na jeeh alihusika vipi katika hukumu ya Yesu Kristo King Octavian
 
It is true. Wala haikuwa kitu cha kusema ilitabiriwa au ilikuwa ni tukio la ajabu. Kusulubishwa ilikuwa kawaida kwa walioonekana wanapinga ukoloni wa kirumi katika Israel.

Pia warumi hawakuamini alikufa. Hata watu waliposema alifufuka na kuonekana katika baadhi ya miji watu ilijulikana kuwa alisaidiwa kupona kile kifo na watu wachache ambao walipanga hiyo plan. Akiwemo Joseph mwenye tomb na mke wa Pilato na baadhi ya mitume na sio wote. Tatizo waliokuja na kusambaza imani waliyoiita imani mpya ndio wakaja na lies ambazo hawakujua facts zake na kusahau siasa iliyokuwa inaendelea na kuchochea sababu za kidini.
 
Si unajua ya kuwa kuna imani sahihi na isiyo sahihi.Katika imani hizi moja ya kweli na nyingine ni kinyume chake.

Sasa ni vyema kama una imani ya kweli umsaidie yule mwenye imani potofu.Huo ndio uninadamu au una wasi wasi na imani yako nini?
Unajua kuna watu wamekua na imani zao hata uwaambie nini hawakulewi, mfano mtu anaabudu ng'ombe na anaamini ni mungu wake
Ni Kazi sana mpaka abadilike
 
Target nikufika arusha lakini tutafikaje lazima kuwe na sababu.

Lengo kuu ilikuwa ni Yesu asulubiwe .

Vijisababu vitakuwa vingi. Tamaa, uchu wa madaraka nk lakini lengo limetimia tumepata wokovu.

Hakuna mistake kubwa ambayo shetani amewai kuifanya kama kuruusu yesu asulubiwe.

Hiyoo ni strength inatufanya wakristo kudunda.
Ni kweli kabisa, Wa kristo tutaendelea kudunda sana tena sana tu. Lengo la Yesu ilikua kumkomboa mwanadamu kutoka ktk utumwa Wa shetani.
Hallelujah!
 
Back
Top Bottom