Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini

Watu mko vizuri bwana kwenye kutetea hoja... asante mkuu.
 
King Octavian

Dini ni siasa ya zamani, siasa ni dini ya mbeleni.

Siasa na dini ni pande mbili za sarafu moja.

Ukiona siasa na dini ni vitu tofauti utapata maswali yasiyo msingi.

ukijua siasa ni dini na dini ni siasa wala huwezi kujiuliza kwamba Yesu aliuawa kwa sababu za dini au siasa.

Siasa ni dini.

Ndiyo maana mkuu wa Wakatoliki ni Mkuu wa nchi ya Vatican.

Ndiyo maana ISIS wanapigania caliphate.
 
Kiranga, nilikua najiuliza upo wapi kiongozi, kumbe tupo pamoja, nashukuru kwa hili, Kwa hiyo kwa tafsir ya haraka haraka ya kiimani Siasa na dhambi ni kitu kimoja?
 
Maana yake, Ukiwa Mkristo tu hutokuwa na dhambi tena hata ukizini au kulewa au kuuwa??..ila pia, siye Huyu Yesu alisema kila mtu atabeba furushi lake mwenyewe? na pia kutakuwa na hukumu kutokana na matendo yetu?. Npata kizunguzungu kila nikifkiria dhana ya sisi kukombolowa na kifo cha yesu na kauli zake Yesu kuwa tutabeba mafurushi yetu wenyewe
 
Ok!ninavyojua mimi,Yesu aliuawa c kwasababu ya kisiasa wala kidini bali KUTIMIZA KUSUDI LA MUNGU ambalo ni kumwokoa mwanadam na dhambi kwa hyo yote hayo yaliyotendka ni njia ya kutimiza ANIKO TAKATIFU.
huko kuokolewa na dhambi kukoje? Maana si Mwislam, si Mkristo.... wote wanafanya madhambi mpaka sasa...vipi huko kuokolewa? Pia Yesu mwenyewe anasema tutahukumiwa kutokana na matendo yetu....tumeokolewaje sasa kwa kifo chake? Na wale waliofanya madhambi kabla Yesu hajaja kuokoa na tukamfuata tukawa Wakristo, wale wataokolewaje sasa au kifo cha Yesu hakimuhusu? Maana walikuwa hawamjui na hawakuwa wakristo kama sisi leo
 
Hii nilishawahi kusikia zaidi nikasema nitapata wapi vitabu au nakala za mambo haya ya kale.
Kitu kimoja,mambo yanayotokea siku hizi za leo hayatofautiani sana na mambo ya miaka 2000 iliyopita.
Its the same human being we talking about.
Dah! Nakusoma Sana mkuu
 
Kiranga, nilikua najiuliza upo wapi kiongozi, kumbe tupo pamoja, nashukuru kwa hili, Kwa hiyo kwa tafsir ya haraka haraka ya kiimani Siasa na dhambi ni kitu kimoja?
Unaipataje tafsiri hiyo?

Siasa si kitu kibaya (kama tafsiri yako ya "dhambi" ni kitu kibaya). Kinacholeta ubaya katika siasa ni complexity ya maisha ya leo.

Huko zamani jamii ilikuwa haina complexity na watu waliweza kufanya siasa za maana, wadogo waliheshimu wakubwa, wakubwa walijiheshimu.

Kadiri siku zinavyoendelea, kwa kufuata "The Second Law of thermodynamics", mambo yana move kutoka kuwa simple na kuwa complex, uongozi unageuka uongo, siasa inageuka si hasa.

Kuna watu wanaona siasa yote mbaya. Si kweli. Ni mambo ya nyakati zetu hayo.

Kuna siasa nzuri bado. Waziri Mkuu wa Uingereza kashindwa kuongoza, kajiuzulu Uwaziri Mkuu na sasa anajiuzulu ubunge. Hakuna mtu aliyeuawa wala kupinduliwa wala kung'ang'ania madaraka.
 
wafia dini utawajua tu
 
Somo zuri asante kwakuniongezea maharifa Leo kichwani mwangu
Ila majibu ya yesu kwann yalikuwa sio ya Moja kwa Moja?
Yaani ukimuuliza swali anakujibu kwa swali!!!!
Mfano kwenye kutoa ushuru,
Katika hili la kujibu swali kwa swali inaonyesha watawala wa kipind kile walikuwa wavumulivu kias flan. maana alikuwa anakera mno hasa kwa kiongoz wa juu vile. Ndo maana alikufa akiwa kijana labda. Ambacho sielew ni ilikuwaje wafuasi wa Yesu wakaongezeka dunia nzima kirahis ilihali warumi kwa mamlaka yao wangeweza kuidhibiti hali ya uasi? Au masuala ya unaabuduje hayakuwa na uzito kama hayaathiri ukusanyaj kodi na utiifu kwa huyo mkoloni!
 
Mtoa mada asante sana kwa kuwa objective...jambo ambalo ni gumu sana kwa wafia dini...naomba nipendekeze kwa wale wanaopenda kujua habari hizi kihistoria zaidi.....

Ingia you tube...seach...misquoting jesus by Bart Ehrman. Sikiliza lecture yake....na nyingine nyingi...hakika hautotoka bure!

Angalizo: this is historical approach...so be open minded.
 
Very interesting story, nineipenda.. Hata hivyo Nina maswali mengi ya kuuliza.

He hii dola ya rum ilipindukiwa na nani, mwaka gn

Maswali mengine tayafata.....

Hata hivyo nimrkutana na maneno mawili ya kigeni.


SANHEDRIN السنهدرين majlis kwa maana ya baraza, mahakama

CAIPHAS - linakaribiana na neno CALIPHATE - kwa maana ya kiiongozi wa dini na mtawala.
 
U know absolute nothing dude

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana Yesu alipanda punda badala ya Farasi alipokuwa anaenda Jerusalem
 
so?
mkuu Kwani aliyekuambia Yesu aliuawa kwa sababu za kidini ni nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…