TANZIA Yona Fares Maro (MwanaJF na Muasisi wa Wanabidii) Afariki Dunia

TANZIA Yona Fares Maro (MwanaJF na Muasisi wa Wanabidii) Afariki Dunia

Huo uamuzi ni mgumu mnoo, kwa nini hakuwaza watoto wake, mama anarudi usiku nani atawaangalia!!!

Apumzike kwa amani....
Mwanaume na mwanamke wako tofauti. Mwanamke huwa kitu cha kwanza anawaza mtoto; sisi wanaume kwa vile tuna vichwa viwili huwa tunawaza kwanza K na watoto baadaye. Usimlaumu marehemu ndivyo tulivyo
 
Doris Liundi alikumbwa na kisa kama hiki.

Alijaribu kujiua na watoto wote.

Ila alisalimika huku baadhi ya watoto wakasalimika.

Kesi ilienda High Court na Court of Appeal.

Daktari alithibitisha kuwa Doris alipata ugonjwa wa akili kwa hiyo alipojaribu kujiua na watoto, haikuwa akili timamu.

Ila majaji, kulingana na ushahidi na sheria, akajiuliza kama sawa alikuwa karukwa na akili, iweje alikataza watoto wasipewe maziwa, na pia kwanini akajifungia ndani na watoto; kama hakua na nia ya kuua, na hivyo alikuwa timamu?

Majaji waliandika ile hukumu kwa masikitiko sana na ninakumbuka Jaji wa High Court alisema ni kweli, mshtakiwa alirukwa na akili, lakini ushahidi wa daktari hauwezi kumfunga jaji katika hukumu.

Wasomi wa sheria watanielewa vizuri hapa.

Doris alipatikana na hatia. So sad!
Huyu mamake Taji Liundi mtoto alipona peke yake kama sijakosea
 
Ukiona mwanamke ameanza kuchepuka ndugu yangu ujue huna miaka mitano mbele, Either atakuua au utakufa kutokana na msongo wa mawazo.. Ushauri ni bora ukaachana nae na kuendelea na ishu nyingine halafu kwa nini mjini wamama wenye nyumba ni wengi?
True
 
Vitu vingine unaweza usitegemee kwa mtu smart kama Yona ....sijui ndio pepo la mauti! Dah
Mkuu linapokuja suala la ''mtu kujiua'' ni kitu amabcho kipo complex sana. Tena mara nyingi watu smart ndio huingia kwenye huamua kuchukua hii njia. Zamani nakumbuka kuna dada mmoja alijiua kwa kunywa sumu ya wadudu. Ile siku ya mazishi alikuwepo kijana mmoja mcheshi na mchangamfu, jirani wa marehemu akawa anafoka na kusikitika inakuwaje mtu aamue kunywa sumu badala ya kupambana na matatizo. Haikuisha miei sita na yeye tukasikia amekunywa sumu na kufariki. Kila mtu aliyemsikia ile siku ya mazishi ya yule dada akabaki kushangaa!
 
Dah...Yona amenisikitisha sana to be true. Nimetoka naye mbali sana. Tangu 2002 tulipokua tunaanza kuhangaika na utundu wa mitandaoni. Na mambo mengune mengu ambayo siwezi kuyasema lakini kwa ufupi alikua ni kijana very bright na aliyeipenda nchi yake kwa moyo wote.
Nilitamani nijitahidi niwezavyo niweze kuhudhuria mazishi yake, ila bahati mbaya huwa sina utamaduni wa kuhudhuria mazishi ya mtu aliyejiua.
Dah...so sad. Kama bado tungekua intouch nina uhakika asingefikia maamuzi hayo.
Na huenda labda alikua mtu mkimya asieshare yanayomsibu na wengine
 
But kwa nini maamuzi kama hayo wakati unaweza kuquit kwa kutalikiana au Ku revenge kuliko kujiangamiza,sidhani kama ni sawa,alikuwa na marafiki na ndugu angewashirikisha kutafuta suluhu hata jf pia
Jamani tukikwama kutoa maamuzi wenyewe tushirikishe wengine sio kujichukulia sheria mkononi
Ndoa ni mwiba mkuu,bila ya kumshirikisha Mungu unaweza kufanya uamuzi wowote ule,hata kama utashirikisha marafiki,ndugu,wanasaikolojia,wachungaji na vitu vyote ujuavyo,usipokuwa karibu na Mungu ni kazi bure..
 
kujiua ni roho ya mauti, kama hauna ulinzi wa Mungu ikikupata hata hautajua kwanini unajiua, ila ukitaka kujiua ukapona siku Mungu akakufungua macho utajilaumu kwanini ulitaka kufanya maamuzi ya kijinga. hata yeye kama angepata nafasi ya kupona, kuna siku angejishangaa kwasababu wala sio yeye, ni roho chafu ya mauti. mkimbilieni Bwana ili awe mliinzi wenu, bila yeye hakika mtu yeyote anaweza kufanya lolote wala sio wa kumlaumu huyo Yona kwa maamuzi ya kijinga, laumuni shetani.
 
Back
Top Bottom