Yondani anaweza kupata pesa nyingi kuliko kipindi chote alichocheza mpira

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Kwa wale wanaofatilia Azam TV, kuna mahojiano na mashabiki kuelekea mechi ya Yanga na Simba. Katika mahojiano hayo kuna shabiki mmoja wa Yanga anatamka bila wasiwasi na Azam TV kumuweka hewani kuwa, Simba hawawezi kufunga Yanga bila makandokando na hata walipomfunga nne walimhonga Yondani.

Yondani bado anacheza mpira kama ajira yake, kitendo cha kumhusisha na hongo kitamfanya asiaminike hata pale inapotokea akafanya kosa kwa bahati mbaya. Pia kitawapa mashaka waajiri wake hata kutomuongezea mkataba.

Katika ile mechi, Yondani aliingia mwishoni wakati timu imeshafungwa, kwanini sasa wamhusishe na hongo? Kwa TV kama Azam sikutegemea kama wanaweza kukosa weledi na kurusha kipindi bila kufanya uhariri, hivyo ni muda sahihi wa Yondanj kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.
 
Hata mimi huwa najiuliza sana maana hii kauli umejaa sana humu.
Najiulizaga hivi watu wana ushahidi au wanaongea tu kujifurahisha.
 
aangalie tu na yy acje akajaa kwny mtego wakat unamshaur na una maon anaend kuvun pesa icje ikawa akatoa yy pesa
 
Ungewataja tu kwa majina yao feki hao mbulugila wanatoa malalamiko yao humu, huku wakiwa hawana ushahidi wowote ule.

Mimi naanza na huyu GENTAMYCINE! Amekuwa ni mbulugila mwenye malalamiko ya uongo sana! Mwingine ni huyu mbulugila njaakalihatari! Mbulugila wengine nimewaweka akiba. Ila kuna siku nao nitakuja kuwataja hadharani.
 
Naona upepo wa hela unamuelekea Cotton ashindwe mwenyewe tu kuzikinga. Ingekuwa mimi ndiyo ile tunaita mbuzi kafia kwa muuza supu.
 
mkuu sio kudai haki ila lzm ujue halisia na nadharia n vitu viwil tofaut kule munapoend n mahakamn sio kijiwen
Unaweza usiwe mwanasheria lakini vitu vingine vidogo ukavijua hivi Azam wanaweza kuthibitisha alipewa rushwa wapi, siku Gani, saa ngapi, kiasi gani na nani alipmpa rushwa
Naomba unijibu hata swali moja
 
Wengi wakurupukaji tu wanapenda kuropoka ropoka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…