JaxenDL
JF-Expert Member
- May 17, 2022
- 1,118
- 2,581
wanalia mkuu, ata Jo amesema bado analia.Kwani kwenye 1 na 2 wanawake huwa hawalii...
Nimeongelea kwa upande wangu sijaona kilio muda mrefu
wanalia mkuu, ata Jo amesema bado analia.Kwani kwenye 1 na 2 wanawake huwa hawalii...
Hii no. 03 unamsaidiaje mtu ambaye muda mwingi ananung’unika na kuona hakusatahili kupitia jambo fulani? Na kwanini negativity iwe faster kuwa attracted kwa sababu tu mtu huyo haja appreciate kitu kibaya kilichomkuta?2. Kutuliza pressure au mawazo... mara nyingi hua nakaa kimya natafakali niliwezaje kuovercome changamoto zilizopita... ambazo sikuamini ningevukaje...
na hii inanipa tumaini hata this time i can....
3. Positive thinking kwangu inafanya kazi we become what we think... hata kama ni changamoto ngumu epuka sana manung'uniko na kujilaumu.... kwa sababu utaendelea kujilaumu tu bila kutafuta njia mbadala ya kufanikiwa...
Thanks mkuu
Hapa nimeelewa kwamba una msimamo mkali hauwezi kuyumbishwa kirahisi kwasababu tu kuna jambo umekumbana nalo!Mimi sio motivation speaker lakini nafikiri ni moja kati ya the strongest people i know
Nimepitia pitia mengi lakini kujua ni ngumu hadi niseme
1. Sijawahi kubadili mawazo na maisha yangu yakabadilika, lakini nimewahi kubadili mawazo yangu nikapata unafuu wa nafsi
Hii no 2. Ni mimi.. kutoa uchungu niongee au nilieee hata masaa matatu😅2. Nikiwa na mawazo ya pressure ya kazi/mahusiano huwa natoa uchungu kwa kulia( mimi ni mliaji haswaaa) kwa mahusiano na kama pressure ya kazi njia pekee ni kufanya kazi kuziba hivyo vipengele vinavyoleta pressure
3. Positive thinking ni nzuri lakini haifanyi kazi kwa kila case
Okay kwa mfano una expect jambo fulani litatokea halafu lisitokee ukaanza kujisikia vibaya ukaona kama kile kitu hukustahili unakuwa umekaribisha negativity? Na kama umeikaribisha unawezaje kurudi kule mwanzo kwenye positivity?Positive thinking inasaidia, Binafsi inaniletea energy ya kusimama tena au kufanya maamuzi.
Japo matokeo sio mara zote matokea yanaendana na matarajio. Lakini inasaidia kwa kiasi chake.
Wabheja sana! Kwahiyo kumbe ukiwa na mawazo positive unapokea positive ila ukiwa na mawazo hasi unapokea hasi, what if ukiwa positive na jambo fulani kwa muda mrefu, lets say mwaka ukapata matokeo tofauti na matarajio huruhusiwi kuwa heart broken kwenye same same situation ambayo umekuwa ukiipambania kwa muda mrefu?Umeeleweka vema sana mkuu ni kwamba mtu huwa kulingana na anavyoilisha akili yake. Ukiilisha akili yako vitu positively utakuwa hivyo na kinyume chake ni sawa. Mfano mtu anayeilisha akili yake picha za utupu atakuwa wa hivyo hivyo tu. Na mtu anayeilisha akili yake maarifa, bidii na imani ya kweli atafanikiwa
Binafsi naamini kuwa akili ya mtu na mawazo ya mtu yanaweza kuwa chanzo Cha mafanikio yake au anguko lake kwa sababu naamini mawazo yako yanaweza kukufanya ulemae kiupambanaji au kiutaftaji au ikakufanya uchakarike na upambanie maisha yako, ijapokuwa positive mind siyo guarantee ya kwamba 100 percent utafanikiwa lakini inaweza kuwa catalyst ya wewe kupambana kufikia lengo lako, kwa kuwa mawazo chanya bila juhudi nayo inaweza kuwa bure kama haihusishi juhudi na bidii
1. Siwezi kusema maisha kwangu yamebadilika sana ila mawazo ya kuamini kuwa ninaweza, nina thamani na mafanikio yapo kwenye juhudi zangu yamenifanya nipambane maradufu kwa ajili yangu na familia yangu, nashukuru Mungu mkate wa siku haunishindi na familia yangu hailali njaa, watoto wanasoma, na chenji chenji hazinisumbui in fact naishi maisha ya kawaida kwa levo zetu za kitanzania ijapokuwa familia niliyotoka ilikuwa hali tete.
2. Ninaamini katika falsalfa ya kutafuta Kuna kupata na kukosa, hivyo nisipopata Leo nitapata kesho ijapokuwa Kuna muda vyuma vinakaza na mambo hayasogei lakini naamini katika kesho iliyo bora kuliko Leo au Jana niliyokosa
3. Inafanya kazi katika kuamsha hari na munkari wa upambaniaji na utafutaji ndani yako ijapokuwa positive thinking inahitaji juhudi na uvumilivu usiomithilika katika kukabili changamoto za kila siku hasa kwa sisi watu wa hali ya kati.. So inafanya kazi kukiwa na hari
Angalia sana hivi vitu 2Habari wadau wa JF,
Unavuta Kile Unachowaza na Kuamini: Akili Yako Ni Adui Au Nguvu Yako Kubwa?
Nimekuwa nikijiuliza sana hivi karibuni;
Kwa nini watu wawili wakipitia changamoto ile ile, mmoja anaona fursa na mwingine anaona mwisho wa dunia?
Nimegundua kitu kimoja Life does not give you what you WANT, it gives you what you BELIEVE.
Ukiamini pesa ni ngumu, utaona ni ngumu kweli. Ukiamini hakuna kazi Dar, hutapata. Ukiwaza kila siku "nimezimiwa, naonewa, sitaweza" ubongo wako utatafuta ushahidi wa kukuthibitishia kuwa uko sahihi.
Mifano
•Ukianza siku ukisema "leo itakuwa mbaya", hata daladala ikichelewa kidogo unasema "nilijua tu".
•Ukiamini "watu hawapendi kununua online", hautajitahidi kuuza vizuri.
Swali langu kwenu wadau;
1. Je, umewahi kubadilisha mawazo yako na maisha yakabadilika kweli? Toa mfano.
2. Unafanyaje ku-control mawazo hasi hasa ukiwa kwenye pressure ya pesa/kazi?
3. Unadhani ni kweli "Positive thinking" inafanya kazi au ni porojo za motivational speakers?
Natoa mwaliko tujadili kwa hekima,
Karibuni.
Huwa inafanya kazi baada ya muda gani? Huenda wengine wana haraka sana!Binafsi huwa ni muumini wa positive thinking, kwa uzoefu wangu naona inafanya kazi
Huwa nina msemo wangu kwamba kila ninachopitia, naamini ni Mungu alipanga nikipitie
Iwe kwa nia ya kujifunza binafsi ama wengine wajifunze kupitia mimi
Mengine hututokea ili kupimwa na kujazwa ujasiri katika kutatua changamoto za baadaye