You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

Unaweza kunielezea zaidi?
Hivi vitu 2 ni silaha kubwa sana kwako, sasa ni wewe kuchagua ikuangamize au ikupe uhai.

Kwanini nasema hivyo. Kuna kitu kinaitwa sheria. Sheria huwa haijui unajua sheria au hujui sheria, yeye kazi yake nikutia mtu hatiani. Basi ili kuwa huru ni wewe kujua sheria na inavyofanya kazi. Endelea kujifunza na kutafiti katika hayo mambo 2 yatakusaidia
 
Habari wadau wa JF,

Unavuta Kile Unachowaza na Kuamini: Akili Yako Ni Adui Au Nguvu Yako Kubwa?

Nimekuwa nikijiuliza sana hivi karibuni;

Kwa nini watu wawili wakipitia changamoto ile ile, mmoja anaona fursa na mwingine anaona mwisho wa dunia?

Nimegundua kitu kimoja Life does not give you what you WANT, it gives you what you BELIEVE.

Ukiamini pesa ni ngumu, utaona ni ngumu kweli. Ukiamini hakuna kazi Dar, hutapata. Ukiwaza kila siku "nimezimiwa, naonewa, sitaweza" ubongo wako utatafuta ushahidi wa kukuthibitishia kuwa uko sahihi.

Mifano
•Ukianza siku ukisema "leo itakuwa mbaya", hata daladala ikichelewa kidogo unasema "nilijua tu".
•Ukiamini "watu hawapendi kununua online", hautajitahidi kuuza vizuri.

Swali langu kwenu wadau;

1. Je, umewahi kubadilisha mawazo yako na maisha yakabadilika kweli? Toa mfano.
2. Unafanyaje ku-control mawazo hasi hasa ukiwa kwenye pressure ya pesa/kazi?
3. Unadhani ni kweli "Positive thinking" inafanya kazi au ni porojo za motivational speakers?

Natoa mwaliko tujadili kwa hekima,

Karibuni.

​
Hii ni kweli ila shida watu wanachanganya kati ya mawazo (ambayo mostly huwa yanakuja randomly na ni ngumu kuyacontrol) na hisia zinazopelekea kufocus kwenye jambo husika kwa muda mrefu.

Kiuhalisia, kuwaza mambo mabaya au mambo mazuri hakuwezi kukufanya uangukie huko, coz unaweza kuwaza kufa na usife na unaweza kuwaza kuwa tajiri na usiwe.

Ila effect ya hicho unachowaza huwa inaenda kwenye uhalisia pale ambapo mitetemo yako inatetema kwenye eneo sawia na kile unachokiamini ndani yako (kwahiyo sio mawazo ila mostly ni Imani)

Na infact Imani huwa haziji tu kwenye Kila jambo ila Imani huwa inakuja kwenye yale yote ambayo ni hakika kwa mtu husika coz universe hainaga bahati mbaya wala nzuri ila Kila kitu kipo kwenye mpangilio wake, so Kila kitu ambacho mtu anakutana nacho hakijawahi kuwa coincidence.

Ndio maana kitu ambacho wewe unakiogopa na kinaweza kukufanya mapigo yako ya moyo yaende mbio once kikitokea sio kitu ambacho kinaweza kikadundisha mapigo ya moyo ya Kila mmoja.

Ni sawa na mitetemo pia.
 
Hapa nimeelewa kwamba una msimamo mkali hauwezi kuyumbishwa kirahisi kwasababu tu kuna jambo umekumbana nalo!

Hii no 2. Ni mimi.. kutoa uchungu niongee au nilieee hata masaa matatu😅

Positive thinking haisolve matatizo yote! Kuna mtu nimechagua kumuleza jambo langu moja, kila nikikwama nikimueleza ananjibu nijitahidi kuwa positive.. sasa nashindwa kuelewa..🤔

Mimi naweza kupitia jambo gumu lakini mbele za watu nikaact kama hamna kitu, nikipata nafasi ya kuwa mwenyewe ndo maombolezo yanaanza 🤦‍♀️

Nilishawahi kuwa na boss alikuwa anasema hajawahi kuona nimekasirika hata aniseme vipi lakini alishaniona kwenye camera amenisema weeee nilivyoondoka akaniona kwenye camera nimeingia chumba fulani nikaanza kulia 😂

Positive thinking kusolve mambo yote hii ni kwa motivation tu, practically mambo sio marahisi namna hii
 
Huwa inafanya kazi baada ya muda gani? Huenda wengine wana haraka sana!
Sijawahi kufanya hiyo tathmini lakini Kuna wakati naweza kusubiri hadi miezi 6

Ukiwa in hurry, tegemea disappointment kwenye hili

Sipendi mtu wa kulalamika, Kuna mtu kwa Kila analopitia huwa ni mtu wa kutoa lawama tu

Hajipi nafasi kuweza kuvumilia na kutafakari kwamba pengine anakomazwa kupitia hilo

Mimi wakati naanza kazi, nilikaa miaka 2 tu kazini, then nikakabidhiwa niongoze Idara iliyokuwa na ma-seniors zaidi ya 6

Kumbe ilikuwa ni kipimo watu wamekaa mahali wananipima nacho

Can't write more....lakini it was a big test for the big position
 
Manadharia mengine haya yanafanya kazi vizuri kwa wazungu huko ambako mifumo imenyoka. Huku kwetu cha muhimu uwe na connections nzuri tu na bidii kidogo basi kazi kwisha. Unachokitaka unaweza ukakifanikisha kirahisi tu.

Sasa wewe eti jidanganye kwamba uta-attract what you want wakati uko nje ya mfumo na huna connections. Kila kitu kinakuwa kigumu na uwezekano wa kushindwa ni mkubwa. Mwishowe mtu unaishia kuwa negative!

Hivyo manadharia haya ya kinafsiya yanaathiriwa sana na mazingira (nurture) hata kama asili ya binadamu na misingi yake (nature) ni ya kimajumui (universal). Ukiyachukua manadharia ve tu bila saba haya kutoka huko yalikotoka na kuyaleta huku kwetu bila kuyapitisha kwenye chujio la mazingira na mikatale ya jamii (social constraints ) unaweza ukaishia kutoa boko tu - tamu sana kinadharia lakini chungu kama shubiri kiuhalisia!
Asante!! Hiki ndicho ninachokiongelea pia! Haiwezekani uwe positive na huku unapambana kumbe unajiweka kwneye position ambayo bila connection hutoboi!

Ni sawasawa na kufanya maombi kwa bidii juu ya jambo fulani na usione matokeo wakati umeliomba hilo jambo na kuhakikisha hujakosea katika kufanya hayo maombi! Kumbe vitu vingine vinahitaji matendo na sio big expections tu!

bila kuyapitisha kwenye chujio la mazingira na mikatale ya jamii (social constraints ) unaweza ukaishia kutoa boko tu - tamu sana kinadharia lakini chungu kama shubiri kiuhalisia!
 
Hivi vitu 2 ni silaha kubwa sana kwako, sasa ni wewe kuchagua ikuangamize au ikupe uhai.

Kwanini nasema hivyo. Kuna kitu kinaitwa sheria. Sheria huwa haijui unajua sheria au hujui sheria, yeye kazi yake nikutia mtu hatiani. Basi ili kuwa huru ni wewe kujua sheria na inavyofanya kazi. Endelea kujifunza na kutafiti katika hayo mambo 2 yatakusaidia
Shukrani sana!!
 
Hii ni kweli ila shida watu wanachanganya kati ya mawazo (ambayo mostly huwa yanakuja randomly na ni ngumu kuyacontrol) na hisia zinazopelekea kufocus kwenye jambo husika kwa muda mrefu.

Kiuhalisia, kuwaza mambo mabaya au mambo mazuri hakuwezi kukufanya uangukie huko, coz unaweza kuwaza kufa na usife na unaweza kuwaza kuwa tajiri na usiwe.

Ila effect ya hicho unachowaza huwa inaenda kwenye uhalisia pale ambapo mitetemo yako inatetema kwenye eneo sawia na kile unachokiamini ndani yako (kwahiyo sio mawazo ila mostly ni Imani)

Na infact Imani huwa haziji tu kwenye Kila jambo ila Imani huwa inakuja kwenye yale yote ambayo ni hakika kwa mtu husika coz universe hainaga bahati mbaya wala nzuri ila Kila kitu kipo kwenye mpangilio wake, so Kila kitu ambacho mtu anakutana nacho hakijawahi kuwa coincidence.

Ndio maana kitu ambacho wewe unakiogopa na kinaweza kukufanya mapigo yako ya moyo yaende mbio once kikitokea sio kitu ambacho kinaweza kikadundisha mapigo ya moyo ya Kila mmoja.

Ni sawa na mitetemo pia.
Kwahiyo hii nadharia ya kusema you attract what you are ni misemo tu au inafanya kazi ila sio kwa kila mtu? Kwa hivyo unaweza kutarajia jambo kwa ukubwa na kwa uhakika bila kuwaza unaweza ukalikosa pia lakini ukaanguka vibaya tu!

Hii ya kusema kwamba ukiwaza jambo zuri halitatokea ni kweli halitatokea, lakini ukiwaza jambo baya hata kwa probability tu litatokea ni nadharia!

Nilifikiri imani ina nguvu kuliko kitu chochote kile kumbe haiji tu bila mpangilio kama kitu hakikuwa kwenye mfumo!

Umenifundiaha kitu kipya kuwa hakunaga coincidence! Kuna sehemu niliona watu wa imani wanabishana sana humu kujusu imani na matokeo yake wakasema hakuna kitu kama hicho hiyo ni coincidence tu, wewe hapa umesema hakuna coincidence kila kitu kipo kwenye mpangilio 🤔
 
Mimi naweza kupitia jambo gumu lakini mbele za watu nikaact kama hamna kitu, nikipata nafasi ya kuwa mwenyewe ndo maombolezo yanaanza 🤦‍♀️
Mimi mpaka huwa napenda kuwa mwenyew muda mwingi coz sijui kufake yani huwa niko mbwai mbwai, siwezi kabisa hata nyumbani wananisema sana juu ya hili kwamba siwezi kujikaza hata kiunafiki tu! Nikiwa siko sawa ntajitahidi nisikae na watu kabisaaa!! Nikizuia kulia uchungu unakuwa mkali sana na huwa siongei nakaa kimya muda wote!!
Nilishawahi kuwa na boss alikuwa anasema hajawahi kuona nimekasirika hata aniseme vipi lakini alishaniona kwenye camera amenisema weeee nilivyoondoka akaniona kwenye camera nimeingia chumba fulani nikaanza kulia 😂
😂😂😂😂😂😂 duhh ulijiskiaje alipokueleza? Jamani🙆🏽‍♀️
Positive thinking kusolve mambo yote hii ni kwa motivation tu, practically mambo sio marahisi namna hii
Mambo ni magumu jamani tuwe wakweli tu!
 
Sijawahi kufanya hiyo tathmini lakini Kuna wakati naweza kusubiri hadi miezi 6

Ukiwa in hurry, tegemea disappointment kwenye hili

Sipendi mtu wa kulalamika, Kuna mtu kwa Kila analopitia huwa ni mtu wa kutoa lawama tu

Hajipi nafasi kuweza kuvumilia na kutafakari kwamba pengine anakomazwa kupitia hilo

Mimi wakati naanza kazi, nilikaa miaka 2 tu kazini, then nikakabidhiwa niongoze Idara iliyokuwa na ma-seniors zaidi ya 6
Kuna watu wanapambana hata miaka mitano haoni mwanga, unataka aendelee kuamini tu kuwa hili jambo kitatokea wacha niendelee kusubiri? Unakuta mtu amejaribu kila njia matokeo ni yaleyale kwanini asinung’unike?
Kumbe ilikuwa ni kipimo watu wamekaa mahali wananipima nacho

Can't write more....lakini it was a big test for the big position
Congrats!
 
Kuna watu wanapambana hata miaka mitano haoni mwanga, unataka aendelee kuamini tu kuwa hili jambo kitatokea wacha niendelee kusubiri? Unakuta mtu amejaribu kila njia matokeo ni yaleyale kwanini asinung’unike?
Kila jambo huwa na sababu zake, Kuna wengine wangepewa wanachokiomba kwa wakati huenda wange- mis-use na kupata athari hasi mapema

Kwahiyo pengine wanaachwa hapo waliopo ili wakue kimwili na fikra
Congrats!
Asante mjukuu

Ila ni mwaka 47 huo, sasa tumejizeekea 🤪
 
Kila jambo huwa na sababu zake, Kuna wengine wangepewa wanachokiomba kwa wakati huenda wange- mis-use na kupata athari hasi mapema

Kwahiyo pengine wanaachwa hapo waliopo ili wakue kimwili na fikra
Hmm wengine hawapati kabisa matokeo haijalishi ukuaji!
Asante mjukuu

Ila ni mwaka 47 huo, sasa tumejizeekea 🤪
Poleni..
 
Hmm wengine hawapati kabisa matokeo haijalishi ukuaji!
Hapana, matokeo wanapata ila sio kwa kiwango walichotegemea.

Mathalani uliomba kazi yenye mshahara wa milioni 2, lakini ukapata kazi yenye mshahara wa laki 8

Kumbe wenzio wanakupa muda wa kukuangalia performance yako na namna unavyoweza kuwa productive kwenye Taasisi yao
Asante
 
Okay umeeleweka mzee!
 
Mimi naweza kupitia jambo gumu lakini mbele za watu nikaact kama hamna kitu, nikipata nafasi ya kuwa mwenyewe ndo maombolezo yanaanza
Hapa kuna kipengele ambacho kinaendana na cha kwangu, mimi naweza kupitia mambo magumu ila hakuna mtu ambae anaweza kujua kua napitia hali hiyo ila upande mwingine hata kama napitia hayo kulia ni ngumu kwangu
 
Back
Top Bottom