You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

Kwahiyo kufikiri positive au negative hakuwezi kufanya mtu awe tajiri au masikini au augue ugonjwa au apone ugonjwa fulani bali fikra positive au negative zenye uwezo wa kwenda kubadili mpangilio wa mitetemo yako kutoka kwenye level fulani hadi kwenye level fulani inaweza kufanya hivyo.

Natamani ungechambua zaidi hiyo paragraph ya mwisho hapo juu kama itakupendeza.
 
Weka imani kwenye mambo yaliyo nje ya uwezo wako kwa 100% tu.

Kwenye mambo yaliyo ndani ya uwezo, fanya kinachotakiwa, ukifeli jitathmini, songa mbele.

Kama kuna anguko linakuumiza sana tafuta mzizi wake
Umeniacha hapa mwishoni! Kama kuna anguko linaniumiza nitafute mzizi wake, unaweza kueleza kwa undani?
 
Kuna kitabu kimoja nilikisoma miaka kadhaa, around 2013. Kinaitwa "Think and grow rich- Napoleon Hill. Na toka hapo ninacho hiki kitabu, na huwa sichoki kukisoma.

Kuna somo kubwa sana mle linaitwa "The power of positive thinking". Somo hilo ni kama somo hili, ulilotoa hapa.
Ni kweli kabisa; kinachotokea kwenye maisha ya binadamu ni matokeo ya fikra zake (Fikra sahihi na chanya).
Kwahiyo kwa maisha yetu ya kibongo bongo unaona inafanya kazi kwa kiasi gani maana ukiangalia maisha ya walio wengi yanafanana kwa kiasi kikubwa!
 
Kwenye hii comment yako kuna kitu muhimu sana umegusia ambacho ni exactly opposite to your thread.

Kwanini ni rahisi sana Negative thoughts kutokea kuliko positive.

Binafsi nina ushuhuda wa watu au mie mwenyewe katika mambo mengi.

If I have to rate,
1. Negative thinking: above 60% happened
2. Positive thinking: less than 5% happened
3. Mixed feelings: 20% unexpected results

Swali ambalo bado najiuliza, Kwanini ni rahisi sana kwa Negativity kutokea kuliko Positivity
Uko sahihi kabisa mkuu ni vile sikuipanua zaidi ila nililenga hiki ulichokiandika hapa! Hiyo ndio nilikuwa naitafutia majibu ngoja Thecoder atudadafulie..
 
Nafikiri hiyo theory ya positive thinking kwy huo mfano wako ndipo inapofanya kazi vizuri zaidi kwa tafsiri yangu kuliko mwanzoni.

Kwamba unapopata Negative results, usijute, kuuzunika au kukata tamaa. Badala yake fikiria kuna kitu hukukifanyia kazi vyema mwanzo hivyo fikiria namna ya kujaribu tena. Hapo ndio inakuja ule msemo "keep on trying "
Na kutokana na hiyo, ndio maana wanasema waliofanikiwa wengi walipambana hawakukata tamaa.

Mfano, wavumbuzi wengi wanapitia fall down nyingi sana hadi kuja na hizo innovative solutions.

Ukibaki kwy kujuta, kukata tamaa, huzuni, majuto. Hiyo ndio Negative thinking sasa, coz hutaendelea au kurudia kitu kilichokupa Negative results.

Maelezo hayo juu, kwa mtazamo wangu ndio maana halisi kati ya Positive and Negative thoughts.
Umenielewesha vizuri zaidi hapa! Nazidi kujifunza 🙇🏽‍♀️
 
Kwahiyo kwa maisha yetu ya kibongo bongo unaona inafanya kazi kwa kiasi gani maana ukiangalia maisha ya walio wengi yanafanana kwa kiasi kikubwa!

Inafanya kazi, watu ni matokeo ya kile wanachokiwaza na kukifanya katika maisha yao ya ila siku. Hakuna kitu kitajitokeza nje ya imagination yako. Laaima kuwe na maono sahihi yakufikishe hapo ulipo.
Kufanana kwa maisha; kuna tokana na namna ya mazingira yetu, mifumo yetu na fikra zetu ambazo kwa kiasi kikubwa zinazofanana.
 
Sawasawa nimekuelewa braza chivundu!
 
Nimekubaliana nawe 100%, positive thinking bila juhudi ni ndoto za mchana. Na wewe umeprove hiyo uliamini una thamani na ukapambana mpaka familia inapata mkate na watoto wanasoma. Hapo ndipo ukweli upo.

Na hiyo falsafa yako ya "Leo sikupata, kesho nitapata" ndio nguzo ya watu wa hali ya kati.

Shukrani kwa mchango mzito, lakini bado najiuliza hii point yako ya mwisho kwakuwa mtu anakuwa ana nia ya kufanya jambo fulani, na analipambania haswa, kisha linafeli kila anapojaribu hii inawezekana kuwa ana negativity ndani yake?
Siyo necessarily negativity, ni wakati sahihi haujafika, kuacha kujaribu na kukata tamaa ndiyo negativity lakini unapambania jambo na unaendelea bila kukata tamaa inamaanisha positivity ipo ndani yako lakini muda sahihi wa wewe kutimiza lengo lako haujafika, hivyo kama bado haja quit despite failure inamaanisha still ana mawazo chanya ila tu muda wa yeye ku harvest juhudi zake haujafika, ku quit always ndo inajenga negativity hata kwenye ubongo kuwa hili jambo sitaweza kamwe na inakuwa mbaya zaidi
 
Uko sahihi kabisa mkuu ni vile sikuipanua zaidi ila nililenga hiki ulichokiandika hapa! Hiyo ndio nilikuwa naitafutia majibu ngoja Thecoder atudadafulie..
Nadhani ni experience tu za maisha ndio hasa zinaweza mpeleka mtu kwenye kuwaza mawazo ya upande fulani zaidi ya upande mwingine, ila pia namna mtu anavyoyachukulia maisha kwa ujumla wake.
 
Siyo necessarily negativity, ni wakati sahihi haujafika, kuacha kujaribu na kukata tamaa ndiyo negativity lakini unapambania jambo na unaendelea bila kukata tamaa inamaanisha positivity ipo ndani yako lakini muda sahihi wa wewe kutimiza lengo lako haujafika, hivyo kama bado haja quit despite failure inamaanisha still ana mawazo chanya ila tu muda wa yeye ku harvest juhudi zake haujafika, ku quit always ndo inajenga negativity hata kwenye ubongo kuwa hili jambo sitaweza kamwe na inakuwa mbaya zaidi
Hapa nimekuelewa zaidi, shukran 🙏🏽
 
Natamani ungechambua zaidi hiyo paragraph ya mwisho hapo juu kama itakupendeza.
Sumaku inaweza kuattract baadhi ya vitu ila lazima kuwe na vitu kadhaa vilivyozingatiwa cha kwanza ni distance kutoka hapo sumaku ilipo na kile kitu kinachotakiwa kuvutwa na cha pili lazima hiko kitu kinachotaka kuvutwa kiwe ni miongoni mwa vitu ambavyo sumaku inayouwezo wa kukivuta.

Sasa hapo kwenye distance ndio kiini cha mada yetu, ya kwamba mawazo utakayoyakaribisha kichwani mwako yanaposibility kubwa ya kwenda kutokea lakini ukiweka udongo karibu na sumaku au mbao karibu na sumaku sikweki ya kwamba itavutwa ndio maana Mimi nikaandika hiyo paragraph ya mwisho.

Lakini pia mawazo mengi ambayo yanaelea kichwani mwa mtu kwa muda mrefu mengi huwa ni hakika na ndio maana ukiweka sumaku sehemu fulani utaona vile vitu ambavyo vinaweza kuvutwa na sumaku na vipo kwenye umbali fulani huwa vinakua na mtindo wa kusogea taratibu taratibu kuelekea usawa wa sumaku na vikifika kwenye umbali unaotosha kuvutwa basi vinavutwa.

Kwahiyo wewe hupangi nini cha kuwaza na nini si chakuwaza ila mawazo yanakuja kwa namna mbili labda au tatu, ya kwanza ni kutokana na uzoefu wako wa kwenye maisha na pili ni hakika yako na tatu ambayo inaweza kuingia kwenye ya kwanza ni umekua triggered na kitu fulani ambacho hukuwahi kutegemea kama kingetokea ila kikatokea, hapa sasa ndio unakuta watu wanakua na mawazo ya huzuni unapoenda msibani, kuna watu wanakua na huzuni hadi wanazimia na mostly maeneo haya ndio frequency za watu zinakua sana down na ndio maana wale wataalam wa kucheza na hizo vitu wanatumiaga sana nafasi hiyo kuchange hatima halisi za watu (hapa kaka yangu Mshana nadhani ndio anaweza kupaelezea vizuri😅)
 
Habari wadau wa JF,

Unavuta Kile Unachowaza na Kuamini: Akili Yako Ni Adui Au Nguvu Yako Kubwa?

Nimekuwa nikijiuliza sana hivi karibuni;

Kwa nini watu wawili wakipitia changamoto ile ile, mmoja anaona fursa na mwingine anaona mwisho wa dunia?

Nimegundua kitu kimoja Life does not give you what you WANT, it gives you what you BELIEVE.

Ukiamini pesa ni ngumu, utaona ni ngumu kweli. Ukiamini hakuna kazi Dar, hutapata. Ukiwaza kila siku "nimezimiwa, naonewa, sitaweza" ubongo wako utatafuta ushahidi wa kukuthibitishia kuwa uko sahihi.

Mifano
•Ukianza siku ukisema "leo itakuwa mbaya", hata daladala ikichelewa kidogo unasema "nilijua tu".
•Ukiamini "watu hawapendi kununua online", hautajitahidi kuuza vizuri.

Swali langu kwenu wadau;

1. Je, umewahi kubadilisha mawazo yako na maisha yakabadilika kweli? Toa mfano.
2. Unafanyaje ku-control mawazo hasi hasa ukiwa kwenye pressure ya pesa/kazi?
3. Unadhani ni kweli "Positive thinking" inafanya kazi au ni porojo za motivational speakers?

Natoa mwaliko tujadili kwa hekima,

Karibuni.
You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

Haya Madini Niliyopata....🙏🙏🙏 Endeleen Seran Thecoder Andromeda Galaxy Na Wengine SaidAlly
 
Attachments

  • downloadfile-6.png
    downloadfile-6.png
    1.6 MB · Views: 9
Sumaku inaweza kuattract baadhi ya vitu ila lazima kuwe na vitu kadhaa vilivyozingatiwa cha kwanza ni distance kutoka hapo sumaku ilipo na kile kitu kinachotakiwa kuvutwa na cha pili lazima hiko kitu kinachotaka kuvutwa kiwe ni miongoni mwa vitu ambavyo sumaku inayouwezo wa kukivuta.

Sasa hapo kwenye distance ndio kiini cha mada yetu, ya kwamba mawazo utakayoyakaribisha kichwani mwako yanaposibility kubwa ya kwenda kutokea lakini ukiweka udongo karibu na sumaku au mbao karibu na sumaku sikweki ya kwamba itavutwa ndio maana Mimi nikaandika hiyo paragraph ya mwisho.

Lakini pia mawazo mengi ambayo yanaelea kichwani mwa mtu kwa muda mrefu mengi huwa ni hakika na ndio maana ukiweka sumaku sehemu fulani utaona vile vitu ambavyo vinaweza kuvutwa na sumaku na vipo kwenye umbali fulani huwa vinakua na mtindo wa kusogea taratibu taratibu kuelekea usawa wa sumaku na vikifika kwenye umbali unaotosha kuvutwa basi vinavutwa.

Kwahiyo wewe hupangi nini cha kuwaza na nini si chakuwaza ila mawazo yanakuja kwa namna mbili labda au tatu, ya kwanza ni kutokana na uzoefu wako wa kwenye maisha na pili ni hakika yako na tatu ambayo inaweza kuingia kwenye ya kwanza ni umekua triggered na kitu fulani ambacho hukuwahi kutegemea kama kingetokea ila kikatokea, hapa sasa ndio unakuta watu wanakua na mawazo ya huzuni unapoenda msibani, kuna watu wanakua na huzuni hadi wanazimia na mostly maeneo haya ndio frequency za watu zinakua sana down na ndio maana wale wataalam wa kucheza na hizo vitu wanatumiaga sana nafasi hiyo kuchange hatima halisi za watu (hapa kaka yangu Mshana nadhani ndio anaweza kupaelezea vizuri😅)
Asante sana!
Acha nikubali kuwa imetosha maana natamani uendelee kuelezea zaidi na zaidi haichoshi kusoma na kila unavyoeleza vinaibuka vitu vingine vipya vizuri zaidi.
Hatutamaliza.
 
Asante sana!
Acha nikubali kuwa imetosha maana natamani uendelee kuelezea zaidi na zaidi haichoshi kusoma na kila unavyoeleza vinaibuka vitu vingine vipya vizuri zaidi.
Hatutamaliza.
Usiogope kuuliza mkuu, Uzi bado upo sana huu na wadau ni wengi pia so uulizaji wako ndio utamuibua mtu mmoja somewhere ili atupe kitu cha kuendelea kujifunza zaidi na zaidi.
 
Umeniacha hapa mwishoni! Kama kuna anguko linaniumiza nitafute mzizi wake, unaweza kueleza kwa undani?
Mara nyingi tatizo hutokea ndani zaidi.

Labda unajilinganisha na watu waliokuzunguka. Labda wakubwa zako wanakushinikiza ufanye jambo fulani. Labda una changamoto flani za kiakili.

Ukiona kitu kinakuumiza sana ujue kuna sehemu ndani yako imeguswa.
 
Labda hatuelewani, mfano kila nikifanya biashara yangu haifiki sehemu fulani niliyokusudia mzunguko unakuwa mdogo biashara haitanuki na nimjeribu kubadilisha mtazamo wa kibiashara nina miaka zaidi ya mitano matokeo ni yale yale!

Au ninaomba kazi fulani kila mwaka naikosa napata nisizo na matarajio nazo!

Hapo sielewi pa kuzichomeka hizo points ukiangalia ninafanya juhudi kubwa kufanikisha jambo langu ili kufikia malengo.

Kuumiza kichwa juu ya kupata mafanikio sidhani kama inahusiana na shinikizo la mzazi au mtu, kujilinganisha na watu au matatizo ya kiakili.
 
Labda hatuelewani, mfano kimi kila nikifanya biashara yangu haifiki sehemu fulani niliyokusudia mzunguko unakuwa mdogo biashara haitanuki na nimjeribu kubadilisha mtazamo wa kibiashara nina miaka zaidi ya mitano matokeo ni yale yale!

Au ninaomba kazi fulani kila mwaka naikosa napata nisizo na matarajio nazo!

Hapo sielewi pa kuzichomeka hizo points ukiangalia ninafanya juhudi kubwa kufanikisha jambo langu ili kufikia malengo.

Kuumiza kichwa juu ya kupata mafanikio sidhani kama inahusiana na shinikizo la mzazi au mtu, kujilinganisha na watu au matatizo ya kiakili.
Nilikuwa nazungumzia kuhusu kukabiliana na kufeli.

Juhudi zinaweza kuwa kubwa lakini zisiwe sahihi. Chamsingi ni kutafuta njia mpya na kuzijaribu, pia kujiweka karibu na waliofika unapotaka.

Kuumizwa kichwa kunahusiana mno na makuzi yako, uzoefu na mazingira. Hakuna mtu anazaliwa akiwaza mafanikio, tunafundishwa na jamii. Tunapaswa kujichunguza mara kwa mara, na kukosoa dhana za mafanikio tulizo nazo.
 
Back
Top Bottom