You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

You Attract What You Think and Believe - Is Your Mind Your Biggest Enemy or Power?

Tatizo tumesahulishwa na mifumo kuwa katika hii sinema inayoitwa maisha mchezaji ni ( Mimi na wewe na muangaliaji ni Mimi na wewe) tumekaririshwa zaidi kuangalia sinema na kusahau kuwa sisi ndiyo wachezaji wenyewe.

Tunajiona kama wahanga" victim" wa maisha badala ya mashujas wake. Ndiyo maana linapokuja kicheko cha ulimwengu (kifo) au kwa kusukuma "cosmic joke" tunaona tumepoteza.
Una madini sana mkuu.. endelea kutema👏🏾
 
You can prove me wrong,
Matatizo mengi leo Duniani ni zao la mawazo yetu, ni kama tumemuumba Mungu wetu mwingine na kimuabudu na sasa tunajitoa wenyewe kuwa sadaka kwake, Angalia mfano wa Akili unde (AI) leo tunaambiana inatoroka na kuvuka mipaka, itachukua ajira za watu...mara ooooh...wakati akili hiyo tuliiunda sisi wenyewe

Matatizo yako au yangu ni Mimi au wewe tumeyapa nguvu kwa kujua au kutojua.
 
Watu hawaoni na hawataki kuona mapambano yako ya ndani " inner struggle" wanataka matokeo yako. Kuonesha huruma na unyonge siyo njia sahihi hata kidogo. That is why kuna wakati hatupaswi kuioneshea Dunia unyonge, show it that you can.
DC28C779-AF59-4E66-8448-305FD5A2D0D5.jpeg
 
So true! Am so glad.. tuendelee kujifunza zaidi!
Ok.. ngoja nitoe mfano huu wa kuhuzunisha, tafakari juu ya mtu mwenye jeraha linalovuja damu usoni anayejiangalia kwenye kioo kisha anaamua kuchukua kitambaa na kufuta damu inayoonekana kwenye kioo kwa kufuta kioo na kupaka dawa kwenye kioo. Haya ndiyo maisha yetu
 
Ok.. ngoja nitoe mfano huu wa kuhuzunisha, tafakari juu ya mtu mwenye jeraha linalovuja damu usoni anayejiangalia kwenye kioo kisha anaamua kuchukua kitambaa na kufuta damu inayoonekana kwenye kioo kwa kufuta kioo na kupaka dawa kwenye kioo. Haya ndiyo maisha yetu
This hurts way more..💔
 
This hurts way more..💔
Ndiyo maana hata ule msemo wa "kufikiri nje ya boksi" nao unakosa maana kwa sababu uwepo wa boksi hata kama ukitoka nje ya boksi Kuna athari za boksi.

Tunapaswa kufikiri kwa uhuru bila ya uwepo wa boksi, tubaki wenyewe asilia. Haya maboksi (mifumo ya elimu, Siasa, Jamii, Familia, Dini) ni maboksi yanayotuumiza sana.
 
Ndiyo maana hata ule msemo wa "kufikiri nje ya boksi" nao unakosa maana kwa sababu uwepo wa boksi hata kama ukitoka nje ya boksi Kuna athari za boksi.

Tunapaswa kufikiri kwa kuru bila ya uwepo wa boksi, tubaki wenyewe asilia. Haya maboksi (mifumo ya elimu, Jamii, Familia, Dini) ni maboksi yaliyotuumiza sana.
Hayo maboksi yote sijaona michango yao katika maisha yangu, michango yao ni ambayo kila mtu anaipata bila hata kuomba wala kutegemea!
 
Hayo maboksi yote sijaona michango yao katika maisha yangu, michango yao ni ambayo kila mtu anaipata bila hata kuomba wala kutegemea!
Yanatufanya tufanane wote, tuishi maisha yaleyale yasiyokuwa na ladha ya upekee. Haya ndiyo gereza la mtu wa ndani tangu kuzaliwa mpaka kufa.
 
Habari wadau wa JF,

Unavuta Kile Unachowaza na Kuamini: Akili Yako Ni Adui Au Nguvu Yako Kubwa?

Nimekuwa nikijiuliza sana hivi karibuni;

Kwa nini watu wawili wakipitia changamoto ile ile, mmoja anaona fursa na mwingine anaona mwisho wa dunia?

Nimegundua kitu kimoja Life does not give you what you WANT, it gives you what you BELIEVE.

Ukiamini pesa ni ngumu, utaona ni ngumu kweli. Ukiamini hakuna kazi Dar, hutapata. Ukiwaza kila siku "nimezimiwa, naonewa, sitaweza" ubongo wako utatafuta ushahidi wa kukuthibitishia kuwa uko sahihi.

Mifano
•Ukianza siku ukisema "leo itakuwa mbaya", hata daladala ikichelewa kidogo unasema "nilijua tu".
•Ukiamini "watu hawapendi kununua online", hautajitahidi kuuza vizuri.

Swali langu kwenu wadau;

1. Je, umewahi kubadilisha mawazo yako na maisha yakabadilika kweli? Toa mfano.
2. Unafanyaje ku-control mawazo hasi hasa ukiwa kwenye pressure ya pesa/kazi?
3. Unadhani ni kweli "Positive thinking" inafanya kazi au ni porojo za motivational speakers?

Natoa mwaliko tujadili kwa hekima,

Karibuni.
Uzi huu umenigusa pia. Positive thinking siyo uchawi, lakini namna tunavyofikiri inaweza kubadili namna tunavyoona tatizo, kufanya maamuzi na kuchukua hatua. Ukiamini umefeli, unaweza kukata tamaa; ukiamini bado unaweza kuanza upya, unatafuta njia.
Mimi naamini akili inaweza kuwa nguvu au kikwazo—kutegemea tunavyoitumia. 💯
 
Hawa mabinti zetu wanaadika vizuri. Nakuwa msomaji maana sina content tena🤪
Haya ukimaliza kusoma nijibu haya maswali yangu mawili..

-Je, umewahi kubadilisha mawazo yako na maisha yakabadilika kweli?

-Unadhani ni kweli "Positive thinking" inafanya kazi au ni porojo za motivational speakers?
 
Haya ukimaliza kusoma nijibu haya maswali yangu mawili..

-Je, umewahi kubadilisha mawazo yako na maisha yakabadilika kweli?

-Unadhani ni kweli "Positive thinking" inafanya kazi au ni porojo za motivational speakers?
Sina content mjukuu, mnaandika kila kitu, kinachobaki ni kusoma na kumeza kama vilivyo.

Ndio, si kila kitu kinaanzia kwenye ubongo, nikiwaza kufeli ni kweli nitafeli. Katika kuishi kuna nyakati mtu anapitia kukata tamaa, kuhisi lengo halitatimia, ila kama binadamu nawaza kama nisipofanya nani atanifanyia. Unaamua kubadilisha mtazamo na kuanza tena. Eventually mambo yanaenda.

Motivational speakers wamekuja hivi karibuni, zamani contents za motivation zilipatikana kwenye vitabu na tulihimizwa sana kuvisoma, so positive thinking ndio kila kitu kwenye maisha, motivation inapatikana kwa njia nyingi, sio lazima kwenda seminars na warsha, kuona wenzako wanavyopambana na kufanikiwa tu ni motivation hasa kama utaiangalia in a positive way.
 
Ni kweli kila kitu huanzia ulimwengu wa rohon.

Yaan unavojiwazia ndicho unachovutia kwako, zinabaki juhud tu za kukipata.

Mim nikipitia changamoto za uchumi au mahusiano huwa najipa matumain na ninaamini kesho itabadilika na sitokua hvohvo.
naikataa kabsa roho ya kushindwa kamwe najinenea mema.
 
Back
Top Bottom