Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Ameandika Yericko Nyerere.

"Ukiambiwa kuwa hili ni kombe la Ligi Kuu Tanzania unaweza kuonekana kama chizi hivi hasa ukikaa na watu wa mpira duniani huko... Hili kombe atakuelewa Haji S. Manara tu ukimwambia hili ni kombe la ligi kuu.

Hii aibu laana zote zimwendee Karia na @tanfootball yote. Hili ni yale masufuria ya Kariakoo Gerezani yamegongwagongwa na kupigwa libeti kisha yakapelekwa kwa Kimario Tabata Dampo yakapuliziwa rangi tu? Naamini gharama za kutengeneza hili karai la gerezani haidizi elfu sabini (70,000/=).

Hivi tuko serious kweli Ligi ya thamani ya Milioni mia tano kombe lake ndio hili? Ligi ambayo inashirikisha Klabu ya Simba yenye bajeti yake kwa mwaka zaidi ya bilioni 5, Hivi kombe la ligi ndio hili? Nafikiriki masihara katika soka letu yamevuka mipaka, sheria za nchi zinatakiwa kuchukua mkondo wake. Ndugu zetu Nbc Bank HQ mnaodhamini Ligi hii, hilo ndio kombe mmeleta?

Ndugu zetu Uto kwakuwa walikuwa desperate na ubingwa basi hawajui la mwadhini wala mnadi sala, lakini wangekuwa na uelewa hata nusu tu, wangesusia kabisa, hii ni aibu kwa ligi yenye klabu bora kama ya Simba SC Tanzania ambayo iko kwenye 10 bora Afrika halafu ligi yake kombe ni hili sufuria."

Toa maoni yako

#tujuzeView attachment 2276039
Kumbe ni maumivu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hivi ndo Mabingwa tulimaliza ligi kuu NBC 2021/2022 jana.
20220630_053308.jpg
 
Hongereni sana kwa ubingwa UTOPOLO PRO MAX wazee wa bahasha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Japo kombe bayaaaaaaaaaaa ila tuwalaumu tiefuefu.....

Hongereni machampion

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nipo mtani.....twende tukapambane ktk nchi za watu ila ujikaze sasa safari hii,nmechoka kukubeba.....View attachment 2277110

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
Nzuri hiyo Mtani. 🤝

Sisi nia tunayo na Kikosi bora pia tunacho nadhani ni marekebisho machache tu ya Kikosi ambayo soon tutayafanya.

Hivyo Kimataifa mjiandae kutoka mashindanoni huku Mabingwa wa Kihistoria mkituacha.
 
Back
Top Bottom