Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

[emoji736][emoji736][emoji736]
 
Nadhani kila mtu anamuono wake lakini ukweli ni kwamba, ukiachana na hiyo pasi, nafasi nyingi sana kazipoteza kwa kutaka kulazimisha kufunga yeye, laiti kama akili hiyo aliyofanya angekuwa anafanyaga hivyo basi Yanga tungekuwa na magoli mengi sana. Alichokifanya mwishoni ndio alichotakiwa kukifanya kila mara, ukiwa na mpira aangalie aliyepo nafasi nzuri zaidi yake kuliko kutaka kufunga yeye.
 
Wanainchi mnauona moto wa Yacouba huko Ihefu?
Binafsi mimi haijanistua kabisa kwasababu Yacouba kaonesha kiwango bora sana alipokuwa Yanga kabla hajaumia. Na aliporudi tena uwanjani kwa dakika chache alizocheza Mapinduzi nikaona jamaa bado ni mtu sana. Viongozi walishindwa kufikiria ni maamuzi ya busara kufanyika ili Yacouba awe sehemu ya timu. Au pengine nilichokiona mimi juu ya kiwango chake kimeonwa tofauti na benchi la ufundi na viongozi pia
 
Kule yupo kwa mkopo shida nini?
 
[emoji599] YANGA imemtambulisha mchambuzi wa video, Khalil Ben Youssef raia wa Tunisia [emoji1249] kuwa mkufunzi mpya anaeungana na kikosi cha Kocha Nabi akiwa na CV nzuri kwenye eneo hilo, Kafanya kazi kwenye vilabu vikubwa barani Afrika kama Club Africain, Esperance De Tunis na Al Ahli Tripoli.
 
Kila la kheri Timu ya Wananchi.

Kama kawaida Timu ya Wananchi tuna jambo letu jioni ya leo.

#DaimaMbeleNyumaMwiko.
 
Majukumu yake technical team yanakuwa yapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…