Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya wachezaji watanzania wanaocheza soka nje ya nchi kwa sasa. Orodha inaonyesha mchezaji, nchi anayocheza na jina la club yake ya mwisho kuchezea kabla 'hajatimkia' nje ya nchi kucheza soka la kulipwa.

1. Muharami Mohamed - Msumbiji , former Simba player
2. Haruna Moshi " Boban" - Sweden, former Simba Player
3. Henry Joseph Shindika– Norway, former Simba player
4. Victor Costa " Nyumba" – Msumbiji , former Simba player
5. Renatus Njohole – Switzerland,former Simba Player
6. Athuman Machupa - Sweden, former Simba Player
7. Said Maulid – Angola – former Yanga player
8. Credo Mwaipopo - Sweden – former Yana Player
9. Nizar Khalfan – Canada, former Mtibwa player
10. Kalimangonga Remmy Mtoro Ongala –Sweden,former Kajumulo FC

Idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza nje utaona wanatokea club ya Simba SC " Wekundu wa Msimbazi"; najiuliza maswali yafuatayo
1. Je, wachezaji wa Simba wana vipaji zaidi kuliko wa Yanga ndo mana wengi wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi?

2. Je, wachezaji wa Yanga hawana mwamko wa kucheza nje ya nchi,kwa maana ingine wameridhika na "soka la bongo" ndo sababu ya idadi yao kuwa ndogo?

3. Je, viongozi wa Yanga wanawabania wachezaji wao kucheza nje ya nchi kwa maslahi yao binafsi?

Nini maoni yenu wana JF

Hatuna maGod father wakutupeleka kwa wazungu.

Madalali wote wanao peleka wachezaji ulaya ni Simba damu au uzao wa Simba.
 
Yanga longo longo sana si mliona eti tegete aje acheze mechi ya watani wa jadi sasa Yanga Tumevuna nini pale, sana sana kumlostisha tuu tegete wa watu.
 
1. Muharami Mohamed - Msumbiji , former Simba player
2. Haruna Moshi “ Boban” - Sweden, former Simba Player
3. Henry Joseph Shindika– Norway, former Simba player
4. Victor Costa “ Nyumba” – Msumbiji , former Simba player
5. Renatus Njohole – Switzerland,former Simba Player
6. Athuman Machupa - Sweden, former Simba Player
7. Said Maulid – Angola – former Yanga player
8. Credo Mwaipopo - Sweden – former Yana Player
9. Nizar Khalfan – Canada, former Mtibwa player
10. Kalimangonga Remmy Mtoro Ongala –Sweden,former Kajumulo FC
Umemsahau huyu:

11. Dany Mrwanda - Vietnam, former Simba Player
 
Wana kabumbu naomba mnijuze ni kinanani hao wamechaguliwa kuiongoza klabu yenye nembo ya YEBOYEBO sijui ndala, watani wangu?
 
Naona Michuzi ametuwekea, ingawa hakumalizia kutupa orodha ya wajumbe waliochaguliwa
 
Hata mwimbaji wa taarabu ndani!mambo makubwa jangwani tukishindwa mpira tunaweka alamba alamba aaaam
 
Kama hiyo ilikuwa ni timu bora definately ilifanya vizuri....

swali kwani yanga ya miaka hii haitishi? na kama haitishi tatizo ni nini? ni kocha ama wachezaji wabovu?
 
NI hadithi ya washambuliaji wawili walioichezea klabu ya Yanga katikati ya miaka ya 1990. Mmoja aliitwa James Tungaraza maarufu kama Boli Zozo na mwingine alijulikana kama Nonda Shaaban.

Huyu wa kwanza alisajiliwa kutoka Sigara ya jijini Dar es Salaam na mwingine alikuwa amekimbia vita vya kwao Burundi.

Tungaraza alikuwa staa sana. Kocha wao alihitaji washambuliaji wawili waanze katika kila mechi na alipendelea kuwatumia Watanzania wawili, Mohamed Hussein na Tungaraza. Lakini Nonda aliishia kukalia benchi tu na kuingia katika kipindi cha pili au wakati mwingine asicheze kabisa.

Sahau Kuhusu Mohamed Hussein, huyu alikuwa mfalme wa mabao na kila mtu analifahamu hilo. Lakini Tungaraza alikuwa mjanja uwanjani, mwepesi kuwatoka walinzi, miguu yake ilikuwa ina kasi ya kuwatungua makipa. Alikuwa kipenzi cha Yanga na ni nani angemkumbuka Nonda wakati huo.

Nonda alikuwa anaishi uswahilini kwetu Mwananyamala nyumbani kwa jamaa mmoja �maskini� mwenzake anaitwa Mtambo. Tungaraza alikuwa anakula kuku kutoka kwa matajiri wa klabu ya Yanga kwa sababu alikuwa staa.

Sasa sikia mwisho wa hadithi wa hii. Miaka michache baadaye Nonda alikuwa akihamishwa kwa uhamisho wa dola milioni tisa kutoka klabu ya FC Zurich ya Uswisi kwenda Rennes ya Ufaransa, uhamisho uliovunja rekodi ya uhamisho pale Ufaransa.

Lakini hapa nyumbani, Tungaraza alikuwa anakabiliwa na kesi ya kumpiga Mama muuza Chapati ambaye alikuwa anamdai fedha zake pale Magomeni. Alikuwa anadaiwa sh. 200.
Baadaye Tungaraza aliugua sana na kufariki, lakini kabla hajafariki, wakati huo akiugua, rafiki yake kipenzi Bakari Malima alikuwa akitembeza bakuli la michango ili atibiwe.

Wakati Malima alitembeza bakuli hilo, Nonda alikuwa akihamishwa kutoka Rennes kwenda Monaco kwa kiasi cha dola milioni 25 ambacho kiliweka rekodi ya uhamisho pale Ufaransa. Huu ni mwisho wa simulizi na Mungu ailaze pema peponi roho ya James Tungaraza.

Mara nyingi huu ndiyo mwisho wa simulizi ya mchezaji wa Kitanzania na mchezaji wa nchi nyingine. Na inasikitisha kila ninapokumbuka kuwa Haruna Moshi Boban amerudi nchini baada ya kushindwa kucheza soka Ulaya kwa sababu zisizoeleweka.

Nimesoma habari nyingi na makala tofauti kuhusu kurudi kwa Boban nyumbani. Wengi wanamlaumu Boban, lakini nadhani tunashindwa kugusa tatizo la msingi ambalo liko wazi kabisa.
Ukweli unabakia pale pale kwamba wachezaji wa Tanzania wana vipaji sana, pengine kuliko wa nje, lakini hawajaandaliwa kucheza wala kutamba Ulaya. Hawajaandaliwa kucheza hata Afrika Kusini.

Hata wakati anaondoka nilifahamu kuwa Haruna asingeweza kucheza Ulaya. Na kuna wachezaji wengi wa Kitanzania kuanzia enzi za akina Athumani China mpaka zama hizi za akina Boban na Mrisho Ngassa bado hawajaandaliwa kucheza Ulaya.
Kucheza Ulaya hakuihitaji kipaji peke yake. Kunahitaji uvumilivu, kujituma na kujitoa. Kutamba Ulaya ni vita ya machozi, jasho na damu. Hawa akina Didier Drogba wamepitia katika vipindi hivi.
Kina Drogba wamebaguliwa, wametupiwa ndizi wakifananishwa na nyani, wamepigwa na baridi kali kupindukia, kula chakula wasichokiweza na mikataba yao ya kwanza ilikuwa ni aibu na si ajabu Boban ameanzia mkataba wa kitajiri. Lakini walijua wanachokitaka.
Wachezaji wa Tanzania hawawezi vita hivi kwa sababu hawaandaliwi kisaikolojia kukabiliana na vitu hivi. Akili zao zinaishia katika kununua seti ya Televisheni (Siku hizi wananunua magari), kununua jeans za kisasa na kuchukua senti za haraka zilizopo mbele ya macho yao.
Wachezaji wa Afrika Magharibi wanaandaliwa kiakili kucheza Ulaya. Kwanza tayari wameona kwa macho yao namna kaka zao akina John Fashanu, Abeid Pele na wengineo walivyovuna fedha nyingi barani Ulaya. Hili ni somo tosha kwao na kwa bahati nzuri wanajua namna ambavyo akina Abeid Pele walicheza soka kwa tabu sana. Mama yake alikuwa anauza mkaa ili Pele apate nauli ya kwenda mazoezini.
Sisi hatuna wakongwe (legends) wa kutupa masomo haya. Lakini bahati mbaya pia hatuwafundishi wachezaji wetu angali wakiwa watoto namna mwanasoka wa kulipwa wa kiafrika anavyopitia shida.
Tunachojua ni kumkatia tiketi mchezaji na kumpeleka Ulaya eti kwa sababu ana kipaji. Nyuma yake hajui lolote kuhusu soka la kulipwa na ugumu wake. Na wala hajui mikataba ya Ulaya inavyokwenda. Mbaya zaidi tunawadekeza wafikiri kuwa Tanzania kunalipa kuliko Ulaya kwa sababu ya fedha za kuwaomba wanachama matajiri.
Kuna watu wasio na uelewa ambao wanamuunga mkono Boban. Lakini pitia malalamiko yake utagundua kweli itatuchukua miaka 100 kumpata Nonda wa Tanzania. Boban alikuwa analipwa kiasi cha dola 5,000 kwa mwezi lakini alikuwa anakatwa dola 1,000 kwa mwezi.
Hii ina maana kwamba alikuwa anakwenda nyumbani na dola 4,000. Na tunaweza kufanya alikuwa anakatwa zaidi ya hapo. Lakini jaribu kufikiri, kama kweli Boban angeitumia Sweden kama njia huku akitoa machozi, jasho na damu basi ni wazi kwamba baada ya miaka miwili ya mkataba wake angeweza kuuzwa timu bora zaidi kama vile CSKA ya Moscow na kulipwa kiasi cha dola 18,000 kwa mwezi.
Sawa, unaweza kumuona wakala wako Damas Ndumbaro ni mjinga, lakini kama umefika Sweden, unacheza timu ya Ligi Kuu, haulali nje, haukosi chakula, unapangwa kikosini, Pasipoti yako inaonyesha una miaka 21, maisha yanataka nini zaidi ya kuutafuta mkataba wa Bayern Leverkusen ulipo?
Sawa Boban anaweza kupata shilingi milioni moja kwa mwezi akiwa nchini, lakini kati ya hizo laki nane zinaweza kuwa za kupewa tu kwa hisani ukiwatembelea ofisini akina Hans Pope, Geofrey Nyange Kaburu na rafiki yake Islam. Mshahara halisi ni laki mbili tu.

Anaweza kujiuliza, mbona akina Abuubakar Salum hawapewi? Anathaminiwa kwa sababu anacheza, lakini mpira ukiondoka miguuni atajua tu kuwa fedha hizi ni danganya toto. Hata akina Edibily Lunyamila walikuwa wanapewa sana, mbona sasa hawapewi?

Laiti kama angetoa machozi, jasho na damu ndani ya miaka mitano angeweza kwenda Everton na kupewa kiasi cha shilingi milioni 120 kwa wiki na kujikuta akiwa tajiri kuliko hawa wanaompatia visenti kwa sasa.

Yeye anaitazama dola 5,000 kuwa ndogo lakini ajiulize tu, Nonda alikuwa analipwa kiasi gani na Vaal Professional. Ajiulize Obi Mikel alikuwa anapewa kiasi gani akiwa anacheza Norway katika mkataba wake wa kwanza. Alikuwa analipwa dola 1,000 tu.

Sina haja ya kumlaumu Boban�ndipo akili yake ilipoishia. Huu ni wakati wa kuwatibu wachezaji wetu kisaikolojia angali wakiwa na umri mdogo sana kabla hawajafikia umri wa Boban, Athuman Idd au Mrisho Ngassa.
 
Inasikitisha sana na wakati mwingine huwa nahisi tumelaaniwa; hatuna muda wa kufikiri! Sio katika nyanja hiyo tu hata huko kwingine sis vijana tuna mawazo finyu ya kumaliza zile tuzionazo ni shida kwa sasa bila kutafakari in 20 yrs nini tutafanya.
 
Ebwana mkuu nimekusoma sana, despite story hiyo nilishaisoma kwenye gazeti la mwanasport-HISIA ZANGU (Edo Kumwembe)

kifupi haruna hana cha kutuambia watanzania,mibangi yake ndo inamponza,mwache aje acheze kwenye klabu zake alizozoea ambazo hata fedha za usajili mpaka watu wachangishane.sasa sijui za kumlipa yeye vizuri zitatoka wapi,labda asubiri kuifunga yanga apate ufadha mtaani mana ndo akili za wachezaji wetu zilipoishia.
 
Juzi kakipiga mchangani, pale kwenye viwanja vya Muhimbili. Sijui kama bima yake inamkinga hata akicheza kwenye mazingira yasiyo salama kwake.
Ebwana mkuu nimekusoma sana, despite story hiyo nilishaisoma kwenye gazeti la mwanasport-HISIA ZANGU (Edo Kumwembe)

kifupi haruna hana cha kutuambia watanzania,mibangi yake ndo inamponza,mwache aje acheze kwenye klabu zake alizozoea ambazo hata fedha za usajili mpaka watu wachangishane.sasa sijui za kumlipa yeye vizuri zitatoka wapi,labda asubiri kuifunga yanga apate ufadha mtaani mana ndo akili za wachezaji wetu zilipoishia.
 
Back
Top Bottom