Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Juzi kakipiga mchangani, pale kwenye viwanja vya Muhimbili. Sijui kama bima yake inamkinga hata akicheza kwenye mazingira yasiyo salama kwake.


maximo alikadhania nidhamu watu wakamuona mjinga,matokeo yake ndiyo hayo sasa
 
Heshima kwako Bujibuji,

Nimesoma andiko lako kidogo machozi yanitoke,Inasikitisha sana kuona Tanzania mpaka leo bado hatujaweza kutoa wachezaji aina ya kina Nonda, Adebayor na Drogba.

Nimeshuhudia wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu sana lakini pia wenye nidhamu mbovu kupita maelezo yoyote unayoweza kuyatoa.

Namkumbuka Hamisi Gaga enzi zake akichezea Ndovu ya Arusha alikuwa ana kiwango kuliko wachezaji wengi tunaowatazama kwenye lunga leo.

Hamis Gaga alikuwa mlevi wa kupindukia kiasi kwamba ata nguo za kuvaa yeye mwenyewe alikuwa hana. Kifupi alitumia kipaji chake vibaya na kama bado yuko hai nina hakika atakuwa anabangaiza maisha.

Hamis Gaga ni aina ya wachezaji wengi wa kitazania wasiotambua jinsi ya kutumia vipaji vyao kwa faida yao,ndugu zao na taifa kwaujumla.
 
Ahaaaa....wabongooo ndo tulivyooo bwanaa..wewe sisi na tabuuu wapi na wapi!!!!!!!

yule Nonda shida ya vita kwao ilimfanyaa akawa na nidhamu, kujituma na uvumilivuuuuu
 
Watu hatambui nini wajibu wao, kwao wenyewe na nafsi zao.
Ulevi na soka haviendani.
Ona Gazza, ile namba nane ya Uingereza.
Tunahitaji shule za soka, wacvhezaji tangu wakiwa wadogo wafundishwe kujitambua kuwa wao ni masupa staa wajao.
Wakilitambua hilo hawatazuzuzliwa na mafanikio watakayo yapata kwa kuwa ni kitu ambacho kiko kwenye matarajio yao.
Haya mambo ya kutokea mchangani halafu ghafla unajikuta supa staa ndio yanapelekea watu kufanya mambo ya ajabu.
Heshima kwako Bujibuji,

Nimesoma andiko lako kidogo machozi yanitoke,Inasikitisha sana kuona Tanzania mpaka leo bado hatujaweza kutoa wachezaji aina ya kina Nonda,Adebayor na Drogba.Nimeshuhudia wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu sana lakini pia wenye nidhamu mbovu kupita maelezo yoyote unayoweza kuyatoa.Namkumbuka Hamisi Gaga enzi zake akichezea Ndovu ya Arusha alikuwa ana kiwango kuliko wachezaji wengi tunaowatazama kwenye lunga leo.Hamis Gaga alikuwa mlevi wa kupindukia kiasi kwamba ata nguo za kuvaa yeye mwenyewe alikuwa hana.Kifupi alitumia kipaji chake vibaya na kama bado yuko hai nina hakika atakuwa anabangaiza maisha.Hamis Gaga ni aina ya wachezaji wengi wa kitazania wasiotambua jinsi ya kutumia vipaji vyao kwa faida yao,ndugu zao na taifa kwaujumla.

 
Bange +No Education at all + Malezi ya Uswahilini Tabora Relini + kulijua jiji mixa kulishobokea + ulimbukeni=Haruna Moshi Boban a.k.a Chandumu.
 
wapo vijana wa Kitanzania kwenye UK football academies, huenda pia Denmark, Sweden, Norway na Germany. Ipo siku, hivi karibuni nimesoma maendeleo ya ADAM NDITI kwenye club ya Chelsea.

Hawa vijana wanaolelewa nje watakuja kutukomboa, pengine dual nationality zao zikatusaidia.
 
ni hadithi ya washambuliaji wawili walioichezea klabu ya yanga katikati ya miaka ya 1990. Mmoja aliitwa james tungaraza maarufu kama boli zozo na mwingine alijulikana kama nonda shaaban.

Huyu wa kwanza alisajiliwa kutoka sigara ya jijini dar es salaam na mwingine alikuwa amekimbia vita vya kwao burundi.

Tungaraza alikuwa staa sana. Kocha wao alihitaji washambuliaji wawili waanze katika kila mechi na alipendelea kuwatumia watanzania wawili, mohamed hussein na tungaraza. Lakini nonda aliishia kukalia benchi tu na kuingia katika kipindi cha pili au wakati mwingine asicheze kabisa.

Sahau kuhusu mohamed hussein, huyu alikuwa mfalme wa mabao na kila mtu analifahamu hilo. Lakini tungaraza alikuwa mjanja uwanjani, mwepesi kuwatoka walinzi, miguu yake ilikuwa ina kasi ya kuwatungua makipa. Alikuwa kipenzi cha yanga na ni nani angemkumbuka nonda wakati huo.

Nonda alikuwa anaishi uswahilini kwetu mwananyamala nyumbani kwa jamaa mmoja �maskini� mwenzake anaitwa mtambo. Tungaraza alikuwa anakula kuku kutoka kwa matajiri wa klabu ya yanga kwa sababu alikuwa staa.

Sasa sikia mwisho wa hadithi wa hii. Miaka michache baadaye nonda alikuwa akihamishwa kwa uhamisho wa dola milioni tisa kutoka klabu ya fc zurich ya uswisi kwenda rennes ya ufaransa, uhamisho uliovunja rekodi ya uhamisho pale ufaransa.

Lakini hapa nyumbani, tungaraza alikuwa anakabiliwa na kesi ya kumpiga mama muuza chapati ambaye alikuwa anamdai fedha zake pale magomeni. Alikuwa anadaiwa sh. 200.
Baadaye tungaraza aliugua sana na kufariki, lakini kabla hajafariki, wakati huo akiugua, rafiki yake kipenzi bakari malima alikuwa akitembeza bakuli la michango ili atibiwe.

Wakati malima alitembeza bakuli hilo, nonda alikuwa akihamishwa kutoka rennes kwenda monaco kwa kiasi cha dola milioni 25 ambacho kiliweka rekodi ya uhamisho pale ufaransa. Huu ni mwisho wa simulizi na mungu ailaze pema peponi roho ya james tungaraza.

Mara nyingi huu ndiyo mwisho wa simulizi ya mchezaji wa kitanzania na mchezaji wa nchi nyingine. Na inasikitisha kila ninapokumbuka kuwa haruna moshi boban amerudi nchini baada ya kushindwa kucheza soka ulaya kwa sababu zisizoeleweka.

Nimesoma habari nyingi na makala tofauti kuhusu kurudi kwa boban nyumbani. Wengi wanamlaumu boban, lakini nadhani tunashindwa kugusa tatizo la msingi ambalo liko wazi kabisa.
Ukweli unabakia pale pale kwamba wachezaji wa tanzania wana vipaji sana, pengine kuliko wa nje, lakini hawajaandaliwa kucheza wala kutamba ulaya. Hawajaandaliwa kucheza hata afrika kusini.

Hata wakati anaondoka nilifahamu kuwa haruna asingeweza kucheza ulaya. Na kuna wachezaji wengi wa kitanzania kuanzia enzi za akina athumani china mpaka zama hizi za akina boban na mrisho ngassa bado hawajaandaliwa kucheza ulaya.
Kucheza ulaya hakuihitaji kipaji peke yake. Kunahitaji uvumilivu, kujituma na kujitoa. Kutamba ulaya ni vita ya machozi, jasho na damu. Hawa akina didier drogba wamepitia katika vipindi hivi.
Kina drogba wamebaguliwa, wametupiwa ndizi wakifananishwa na nyani, wamepigwa na baridi kali kupindukia, kula chakula wasichokiweza na mikataba yao ya kwanza ilikuwa ni aibu na si ajabu boban ameanzia mkataba wa kitajiri. Lakini walijua wanachokitaka.
Wachezaji wa tanzania hawawezi vita hivi kwa sababu hawaandaliwi kisaikolojia kukabiliana na vitu hivi. Akili zao zinaishia katika kununua seti ya televisheni (siku hizi wananunua magari), kununua jeans za kisasa na kuchukua senti za haraka zilizopo mbele ya macho yao.
Wachezaji wa afrika magharibi wanaandaliwa kiakili kucheza ulaya. Kwanza tayari wameona kwa macho yao namna kaka zao akina john fashanu, abeid pele na wengineo walivyovuna fedha nyingi barani ulaya. Hili ni somo tosha kwao na kwa bahati nzuri wanajua namna ambavyo akina abeid pele walicheza soka kwa tabu sana. Mama yake alikuwa anauza mkaa ili pele apate nauli ya kwenda mazoezini.
Sisi hatuna wakongwe (legends) wa kutupa masomo haya. Lakini bahati mbaya pia hatuwafundishi wachezaji wetu angali wakiwa watoto namna mwanasoka wa kulipwa wa kiafrika anavyopitia shida.
Tunachojua ni kumkatia tiketi mchezaji na kumpeleka ulaya eti kwa sababu ana kipaji. Nyuma yake hajui lolote kuhusu soka la kulipwa na ugumu wake. Na wala hajui mikataba ya ulaya inavyokwenda. Mbaya zaidi tunawadekeza wafikiri kuwa tanzania kunalipa kuliko ulaya kwa sababu ya fedha za kuwaomba wanachama matajiri.
Kuna watu wasio na uelewa ambao wanamuunga mkono boban. Lakini pitia malalamiko yake utagundua kweli itatuchukua miaka 100 kumpata nonda wa tanzania. Boban alikuwa analipwa kiasi cha dola 5,000 kwa mwezi lakini alikuwa anakatwa dola 1,000 kwa mwezi.
Hii ina maana kwamba alikuwa anakwenda nyumbani na dola 4,000. Na tunaweza kufanya alikuwa anakatwa zaidi ya hapo. Lakini jaribu kufikiri, kama kweli boban angeitumia sweden kama njia huku akitoa machozi, jasho na damu basi ni wazi kwamba baada ya miaka miwili ya mkataba wake angeweza kuuzwa timu bora zaidi kama vile cska ya moscow na kulipwa kiasi cha dola 18,000 kwa mwezi.
Sawa, unaweza kumuona wakala wako damas ndumbaro ni mjinga, lakini kama umefika sweden, unacheza timu ya ligi kuu, haulali nje, haukosi chakula, unapangwa kikosini, pasipoti yako inaonyesha una miaka 21, maisha yanataka nini zaidi ya kuutafuta mkataba wa bayern leverkusen ulipo?
Sawa boban anaweza kupata shilingi milioni moja kwa mwezi akiwa nchini, lakini kati ya hizo laki nane zinaweza kuwa za kupewa tu kwa hisani ukiwatembelea ofisini akina hans pope, geofrey nyange kaburu na rafiki yake islam. Mshahara halisi ni laki mbili tu.

Anaweza kujiuliza, mbona akina abuubakar salum hawapewi? Anathaminiwa kwa sababu anacheza, lakini mpira ukiondoka miguuni atajua tu kuwa fedha hizi ni danganya toto. Hata akina edibily lunyamila walikuwa wanapewa sana, mbona sasa hawapewi?

Laiti kama angetoa machozi, jasho na damu ndani ya miaka mitano angeweza kwenda everton na kupewa kiasi cha shilingi milioni 120 kwa wiki na kujikuta akiwa tajiri kuliko hawa wanaompatia visenti kwa sasa.

Yeye anaitazama dola 5,000 kuwa ndogo lakini ajiulize tu, nonda alikuwa analipwa kiasi gani na vaal professional. Ajiulize obi mikel alikuwa anapewa kiasi gani akiwa anacheza norway katika mkataba wake wa kwanza. Alikuwa analipwa dola 1,000 tu.

Sina haja ya kumlaumu boban�ndipo akili yake ilipoishia. Huu ni wakati wa kuwatibu wachezaji wetu kisaikolojia angali wakiwa na umri mdogo sana kabla hawajafikia umri wa boban, athuman idd au mrisho ngassa.

haya yota ni shida ya majanii nafikiri swala muhimu kwa ndumbaro ni kujifunza asikimbilie umaarufu akimbilie na wenye nidhamu huyu boban tangu akiwa tstars alipewa live na upuuzi wake mpaka maximo akasema labda awe anapanda pipa ndio atamrudisha na kweli jamaa anaondoka boban anarudi....

nidhamu jamani nidhamu muhumi sana kweli haya majani yameumbwa na mungu lakini mungu ajatuelekeza kuyatumia viabaya hivi
 
Nimekugongea " thanks " mkuu bujibuji. Hii stort yako imenigusa kweli!

Serikali inabidi itengeneze mazingira bora ya kielimu na kimichezo toka ngazi ya chini ya vijana ( mashuleni )

Kwa sasa itakua ngumu - " Samaki mkunje angali mbichi "
 
Hivi mtu anaposema wachezaji wetu wana vipaji lakini hawajaandaliwa kucheza ulaya huwa anamaanisha nini?
 
Hivi mtu anaposema wachezaji wetu wana vipaji lakini hawajaandaliwa kucheza ulaya huwa anamaanisha nini?

Anamaanisha wawe wana nidhamu akiambiwa zunguka uwanja mara mia kweli azunguke, aheshimu, ajibidilishe, ajitume, awe mvumilivu n.k
 
Heshima kwako Bujibuji,

Nimesoma andiko lako kidogo machozi yanitoke,Inasikitisha sana kuona Tanzania mpaka leo bado hatujaweza kutoa wachezaji aina ya kina Nonda,Adebayor na Drogba.Nimeshuhudia wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu sana lakini pia wenye nidhamu mbovu kupita maelezo yoyote unayoweza kuyatoa.Namkumbuka Hamisi Gaga enzi zake akichezea Ndovu ya Arusha alikuwa ana kiwango kuliko wachezaji wengi tunaowatazama kwenye lunga leo.Hamis Gaga alikuwa mlevi wa kupindukia kiasi kwamba ata nguo za kuvaa yeye mwenyewe alikuwa hana.Kifupi alitumia kipaji chake vibaya na kama bado yuko hai nina hakika atakuwa anabangaiza maisha.Hamis Gaga ni aina ya wachezaji wengi wa kitazania wasiotambua jinsi ya kutumia vipaji vyao kwa faida yao,ndugu zao na taifa kwaujumla.


Hamis Thobias Gaga 'Gagarino' hatunaye tena. Alifariki miaka kadhaa iliyopita. Hii habari iliandikwa vizuri na Edo Kumwembe katika gazeti la Mwanaspoti.
 
KKDKDK.JPG
 
Salamu tumetuma Msimbazi
Tutatoa kipigo cha mbwa mwizi
Hatuogopi hizo zenu hirizi
Asamoah anawangoja kichizi!

Mwaka huu mtakoma na Papic
Kama mlivyolizwa na Kondic
Hata kama hatuna kipa Cuckovic
Tunao mabeki bomba kuliko Vidic

Tumewapa muda ili Phiri aje
Tutaona mkifungwa mtasemaje
Kichapo palepale hata mkifanyaje
Sijua Msimbazi mtarudije!!
 
Msimbazi unapenda sana kujifariji!
Mwalala asuswe wakati alitikisa jiji!
Kuwafunga Simba ni kama kunywa uji!
Ni kazi rahisi kwetu haiihitaji mtaji

Asamoah katoka Ghana
Uwanjani masihara hana
Akipata mpira mnapotezana
Sipati picha mtakavyonuniana!

Yondani anamkumbuka Ngasa
Asamoah ni zaidi ya Ngasa
Tutawaonyesha mpira sio siasa
Ukimchezea chatu ushindi utaukosa!

Kumlinganisha Del Bosque na Phiri
Ni sawa na kufananisha kisima na bahari
Mserbia mmemtelekeza kwa wenu ubahiri
Kwanza Phiri hamkuti Papic kwa umahiri
 
Back
Top Bottom