Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Juzi kakipiga mchangani, pale kwenye viwanja vya Muhimbili. Sijui kama bima yake inamkinga hata akicheza kwenye mazingira yasiyo salama kwake.


maximo alikadhania nidhamu watu wakamuona mjinga,matokeo yake ndiyo hayo sasa
 
Heshima kwako Bujibuji,

Nimesoma andiko lako kidogo machozi yanitoke,Inasikitisha sana kuona Tanzania mpaka leo bado hatujaweza kutoa wachezaji aina ya kina Nonda, Adebayor na Drogba.

Nimeshuhudia wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu sana lakini pia wenye nidhamu mbovu kupita maelezo yoyote unayoweza kuyatoa.

Namkumbuka Hamisi Gaga enzi zake akichezea Ndovu ya Arusha alikuwa ana kiwango kuliko wachezaji wengi tunaowatazama kwenye lunga leo.

Hamis Gaga alikuwa mlevi wa kupindukia kiasi kwamba ata nguo za kuvaa yeye mwenyewe alikuwa hana. Kifupi alitumia kipaji chake vibaya na kama bado yuko hai nina hakika atakuwa anabangaiza maisha.

Hamis Gaga ni aina ya wachezaji wengi wa kitazania wasiotambua jinsi ya kutumia vipaji vyao kwa faida yao,ndugu zao na taifa kwaujumla.
 
Ahaaaa....wabongooo ndo tulivyooo bwanaa..wewe sisi na tabuuu wapi na wapi!!!!!!!

yule Nonda shida ya vita kwao ilimfanyaa akawa na nidhamu, kujituma na uvumilivuuuuu
 
Watu hatambui nini wajibu wao, kwao wenyewe na nafsi zao.
Ulevi na soka haviendani.
Ona Gazza, ile namba nane ya Uingereza.
Tunahitaji shule za soka, wacvhezaji tangu wakiwa wadogo wafundishwe kujitambua kuwa wao ni masupa staa wajao.
Wakilitambua hilo hawatazuzuzliwa na mafanikio watakayo yapata kwa kuwa ni kitu ambacho kiko kwenye matarajio yao.
Haya mambo ya kutokea mchangani halafu ghafla unajikuta supa staa ndio yanapelekea watu kufanya mambo ya ajabu.
 
Bange +No Education at all + Malezi ya Uswahilini Tabora Relini + kulijua jiji mixa kulishobokea + ulimbukeni=Haruna Moshi Boban a.k.a Chandumu.
 
wapo vijana wa Kitanzania kwenye UK football academies, huenda pia Denmark, Sweden, Norway na Germany. Ipo siku, hivi karibuni nimesoma maendeleo ya ADAM NDITI kwenye club ya Chelsea.

Hawa vijana wanaolelewa nje watakuja kutukomboa, pengine dual nationality zao zikatusaidia.
 

haya yota ni shida ya majanii nafikiri swala muhimu kwa ndumbaro ni kujifunza asikimbilie umaarufu akimbilie na wenye nidhamu huyu boban tangu akiwa tstars alipewa live na upuuzi wake mpaka maximo akasema labda awe anapanda pipa ndio atamrudisha na kweli jamaa anaondoka boban anarudi....

nidhamu jamani nidhamu muhumi sana kweli haya majani yameumbwa na mungu lakini mungu ajatuelekeza kuyatumia viabaya hivi
 
Nimekugongea " thanks " mkuu bujibuji. Hii stort yako imenigusa kweli!

Serikali inabidi itengeneze mazingira bora ya kielimu na kimichezo toka ngazi ya chini ya vijana ( mashuleni )

Kwa sasa itakua ngumu - " Samaki mkunje angali mbichi "
 
Hivi mtu anaposema wachezaji wetu wana vipaji lakini hawajaandaliwa kucheza ulaya huwa anamaanisha nini?
 
Hivi mtu anaposema wachezaji wetu wana vipaji lakini hawajaandaliwa kucheza ulaya huwa anamaanisha nini?

Anamaanisha wawe wana nidhamu akiambiwa zunguka uwanja mara mia kweli azunguke, aheshimu, ajibidilishe, ajitume, awe mvumilivu n.k
 

Hamis Thobias Gaga 'Gagarino' hatunaye tena. Alifariki miaka kadhaa iliyopita. Hii habari iliandikwa vizuri na Edo Kumwembe katika gazeti la Mwanaspoti.
 
Papic alifaa kuwa kocha wa Stars hana mchezo.
 
Salamu tumetuma Msimbazi
Tutatoa kipigo cha mbwa mwizi
Hatuogopi hizo zenu hirizi
Asamoah anawangoja kichizi!

Mwaka huu mtakoma na Papic
Kama mlivyolizwa na Kondic
Hata kama hatuna kipa Cuckovic
Tunao mabeki bomba kuliko Vidic

Tumewapa muda ili Phiri aje
Tutaona mkifungwa mtasemaje
Kichapo palepale hata mkifanyaje
Sijua Msimbazi mtarudije!!
 
Msimbazi unapenda sana kujifariji!
Mwalala asuswe wakati alitikisa jiji!
Kuwafunga Simba ni kama kunywa uji!
Ni kazi rahisi kwetu haiihitaji mtaji

Asamoah katoka Ghana
Uwanjani masihara hana
Akipata mpira mnapotezana
Sipati picha mtakavyonuniana!

Yondani anamkumbuka Ngasa
Asamoah ni zaidi ya Ngasa
Tutawaonyesha mpira sio siasa
Ukimchezea chatu ushindi utaukosa!

Kumlinganisha Del Bosque na Phiri
Ni sawa na kufananisha kisima na bahari
Mserbia mmemtelekeza kwa wenu ubahiri
Kwanza Phiri hamkuti Papic kwa umahiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…