DROO YA MTOANO KOMBE LA SHIRIKISHO KUFANYIKA KESHO JUMATANO
.
Droo ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na hatua ya mtoano kombe la Shirikisho itafanyika kesho Jumatano, Cairo Misri
Jioni ya kesho, macho na masikio ya Wanayanga yataelekezwa huko Misri kwani baada ya droo hiyo Yanga itamfahamu mpinzani wake wa hatua hiyo kusaka nafasi ya kucheza makundi kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne
Aidha kwa upande wa ligi ya mabingwa, timu 16 tayari zimeshapatikana hivyo kutakuwa na zoezi la kupanga makundi manne ya timu nne nne
Hizi hapa timu 16 zilizofuzu shirikisho ambazo zitaungana na timu nyingine 16 zilizotolewa raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa
Mpinzani wa Yanga atatoka miongoni mwa timu hizi
1.RS Berkane (Morroco)
2.Al Masry(Egypt)
3.Hassania Agadir (Morroco)
4.Zanaco (Zambia)
5.Enugu Rangers (Nigeria)
6.Djoliba (Mali)
7.Esae(Benin)
8.DC Motema PEMBE (DRC)
9.FC San Pedro(Ivory Coast)
10.Bandari (Kenya)
11.Bidvest Witts(South Africa)
12.Ts Galaxy (South Africa)
13.Ploline (Uganda)
14.Triangle (Zimbabwe)
15.Pyramids (Egypt)
16.Paradou (Algeria)
Yanga ina uwezekano mkubwa wa kupangwa na moja ya timu kati ya namba 07 mpaka 16 kulingana na marks zinazotolewa na CAF kwa kuangalia mafanikio ya timu kwenye michuano iliyopita
Yangafulldozz