CCM KIRUMBA ITATURAHISISHIA MAANDALIZI
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wameuchagua uwanja wa CCM Kirumba kuutumia mechi dhidi ya Pyramids Fc baada ya kujiridhisha unakidhi vigezo
Aidha Mwakalebela amesema Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu mkoani Mwanza dhidi ya Mbao Fc hivyo wanaamini watakuwa na muda wa kujiandaa mkoani pamoja na kuzoea uwanja "Tutakuwa Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi, hivyo Kamati ya Utendaji ikaona ni vyema mchezo dhidi ya Pyramids Fc tuupeleke huko kwani itaturahisishia maandalizi yetu," amesema "Lakini tutakuwa na muda wa kutosha kuutumia na kuuzoea uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuwakabili Pyramids Oktoba 27" "Muhimu zaidi tunawapa nafasi wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa ya jirani kushuhudia mchezo wa Kimataifa baada ya kukosa burudani hiyo kwa miaka kadhaa"
Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya wiki moja jijini Mwanza kabla ya mchezo huo
Aidha, mabingwa hao wa kihistoria watautumia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Oktoba 24 kama sehemu ya maandalizi yao