Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191012_142444.jpg
 
CCM KIRUMBA ITATURAHISISHIA MAANDALIZI

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wameuchagua uwanja wa CCM Kirumba kuutumia mechi dhidi ya Pyramids Fc baada ya kujiridhisha unakidhi vigezo

Aidha Mwakalebela amesema Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu mkoani Mwanza dhidi ya Mbao Fc hivyo wanaamini watakuwa na muda wa kujiandaa mkoani pamoja na kuzoea uwanja "Tutakuwa Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi, hivyo Kamati ya Utendaji ikaona ni vyema mchezo dhidi ya Pyramids Fc tuupeleke huko kwani itaturahisishia maandalizi yetu," amesema "Lakini tutakuwa na muda wa kutosha kuutumia na kuuzoea uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuwakabili Pyramids Oktoba 27" "Muhimu zaidi tunawapa nafasi wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa ya jirani kushuhudia mchezo wa Kimataifa baada ya kukosa burudani hiyo kwa miaka kadhaa"

Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya wiki moja jijini Mwanza kabla ya mchezo huo

Aidha, mabingwa hao wa kihistoria watautumia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Oktoba 24 kama sehemu ya maandalizi yao
 
MOLINGA AONGEZA NGUVU, KUWAVAA PYRAMIDS FC
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mshambuliaji wa timu hiyo David Molinga ataweza kucheza mchezo wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc Oktoba 27

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Molinga na Mustafa Suleyman hawakuwa na vibali vya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua za mwanzo kwa kuwa walipaswa kupata vibali baada ya Septemba 30

Bumbuli amesema wana uhakika vibali vyao vitawasili wakati wowte na wataweza kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Pyramids itakayopigwa Oktoba 27 uwanja wa Taifa

Kuongezeka kwa Molinga kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga ni habari njema kuelekea mchezo huo kwani Mcongomani huyo kwa sasa ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga
 
Back
Top Bottom