Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

KALENGO APATA MAJERAHA

Mshambuliaji Maybin Kalengo amerudi 'ubaoni' baada ya kupata majeraha ambayo yanaweza kumuweka nje kwa wiki 12

Mshambuliaji huyo kinda aliyesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya Zesco ya Zambia, amepata majeraha kwenye mguu wake wa kushoto wakati akiitumikia Yanga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Fc

Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa nje kati ya miezi miwili mpaka mitatu

Kalengo ndio kwanza alikuwa ameanza kuingia kwenye kikosi cha Zahera, majeraha hayo ni pigo kwake na kwa Yanga

Alipata majeraha kama hayo wakati wa maandalizi ya msimu mpya mkoani Morogoro na kukaa nje kwa takribani wiki tatu
 
MASHABIKI WA YANGA DAR KUONGEZA NGUVU MWANZA
.
Msafara wa mashabiki wa Yanga wa jijini Dar es salaam, unaondoka leo kuelekea Mwanza kuongeza nguvu kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc

Mashabiki hao wanatarajiwa kuondoka na basi la klabu ya Yanga

Mjumbe wa Kamati ya Hamasa, Jimmy Kindoki anaongoza msafara huo

Aidha Wanayanga kutoka mikoa jirani na Mwanza kama Geita, Tabora, Shinyanga na Mara pia watakuwepo kwa wingi Jumapili
 

MASHABIKI WASHAURIWA KUCHANGAMKIA TIKETI MAPEMA
Mashabiki wa klabu ya Yanga jijini Mwanza wametakiwa kuchangamkia kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza Jumapili ambayo ni siku ya mchezo dhidi ya Pyramids Fc

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema tiketi zinaanzwa kuuzwa leo kupitia vituo vilivyoainishwa na klabu hiyo jana

Viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa saa 10 jioni ni Royal Tsh 50,000/-, VIP Tsh 20,000/- na Mzunguuko Tsh 7,000/- "Mashabiki wachangamke mapema kununua tiketi ili siku ya Jumapili wawe na zoezi moja tu, kwenda uwanjani kuishangilia timu yao," amesema "Hii itawaepusha na changamoto zinazoweza kujitokeza siku ya mchezo. Tutafunga zoezi la kuuza tiketi Jumapili mchana lakini inaweza kuwa mapema zaidi kama tiketi zitamalizika"

Vituo vinavyouza tiketi

1. Nyamagana

2. Kituo cha mabasi Nyegezi

3. Kituo cha mabasi Buzuruga

4. Kituo cha mabasi Igoma

5. Shule ya Msingi Buhongwa

6. Uwanja wa CCM Kirumba

7. Lenana Hotel Pasiasi

8. Posta Pamba Road

9. Kituo cha mabasi Mkolani

10. Kituo cha mafuta Buswelu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…