Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191125_104557.jpg
Ijumaa hii tarehe 29/11/2019 Yanga Sc itashuka dimbani(CCM Kirumba) kucheza na Alliance katika muendelezo wa mechi za ligi ku
 
Leo Jumatano, Novemba 27 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli, amesema timu inaelekea Mwanza ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo "Wachezaji wamerejea mazoezi leo baada ya mapumziko ya siku nne. Mwalimu alitoa mapumziko kwa sababu awali ratiba yetu haikuwa ikionyesha kuwa tunapaswa kucheza Novemba 29," alisema "Pamoja na kuwa wametushtukiza lakini tumejipanga vizuri kushinda mchezo huo jijini Mwanza"

Baada ya mchezo huo, Yanga itashuka tena dimbani Disemba 02 kuikabili KMC ukiwa pia ni mchezo wa kiporo.

@Yangafulldozz
 
20191127_062219.jpg
BALAMA KUIKOSA ALLIANCE FC

Kiungo Mapinduzi Balama hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachosafiri leo kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa Ijumaa, Novemba 29

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kiungo huyo hajapona majeraha ya nyonga aliyopata kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania siku ya Ijumaa "Balama ameshindwa kufanya mazoezi kutokana na maumivu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania" "Tutamuacha jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa majeraha yanayomsumbua," amesema

Balama atakosa mchezo huo dhidi ya waajiri wake wa zamani, klabu ya Alliance Fc

Kwenye mchezo huo Yanga pia huenda ikawakosa viungo wake watatu Feisal Salum, Mohammed Issa 'Banka' na Abdulaziz Makame ambao walirejea Zanzibar kujiunga na timu ya Taifa kuelekea michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Uganda kuanzia Disemba 07

@Yangafulldozz
 
20191127_065637.jpg
YANGA YAKANUSHA KUTOWEKA KWA SADNEY

Gazeti moja la michezo leo imeripoti kuwa mshambuliaji wa Yanga Sadney Urikhob ametoweka katika klabu hiyo

Uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hiyo na kuthibitisha kuwa mchezaji huyo leo ameshiriki mazoezi ya asubuhi ambayo yamefanyika uwanja wa Uhuru "Sadney ameshiriki mazoezi ya Yanga yaliyofanyika uwanja wa Uhuru leo, yuko ‘fit’ na hajawahi kukosa mazoezi ya timu tangu Novemba 5, 2019," imesema taarifa ya Yanga

@Yangadaima
 
20191127_070140.jpg
Kikosi cha Yanga SC kitakacho ondoka leo 27/11/2019 kuelekea Jijini Mwanza kwenye mchezo wa tarehe 29/11/2019 wa #VPL dhidi ya @alliancefootballclub2011 ni :

Farouk Shikhalo,
Ramadhani Kabwili,
Juma Abdul,
Jafary Mohammed,
Ally Mtoni,
Kelvin Yondani,
Mustafa Selemani,
Lamine,
Papy Tshishimbi,
Mrisho Ngassa,
David Molinga,
Raphael Daud,
Sadney Urikhob,
Deus Kaseke,
Juma Balinya,
Said Juma,
Patrick Sibomana,
Adam Kiondo(u20)

Pamoja na Benchi la ufundi lenye viongozi saba likiongozwa na Kocha Charles Boniface Mkwasa
 
20191127_071655.jpg

MAKAME APANIA KUFANYA MAKUBWA MSIMU HUU.

Kiungo wa Yanga, Abdulaziz Makame amesema hana hofu ya kukosa namba ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha Boniface Mkwasa na kwamba anampa nafasi kila mtu kuonyesha uwezo wake.

Makame amesema hajaona wa kumkalisha benchi ila anachokiamini ni kujituma kwa bidii ili uwezo wake uwe na faida kwenye timu. "Sijaona ushindani wa aina yoyote ndani ya kikosi cha Yanga kikubwa ni mimi mwenyewe kuongeza bidii ya mazoezi, ninachokiamini hakuna kocha ambaye anaweza kumuweka benchi mchezaji anayeweza kusaidia timu," Makame aliliambia Mwanaspoti "Nipo Yanga kwa ajili ya kucheza hivyo siwezi kuilaza akili yangu kwamba mimi nitakuwa nakaa benchi, isitoshe umri wangu ni mdogo hivyo nina nafasi ya kufanya makubwa zaidi"

Nje na kikosi cha Yanga, amesema anatamani awe na namba ya kudumu ndani ya kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' akiamini kwa mchezaji aliye na ndoto za kufika mbali lazima asaidie taifa lake. "Msimu huu lazima nitafanya mambo makubwa, nimejipanga uwezo utaongea zaidi uwanjani"

@Yangadaima
 
YANGA KUONGEZA UMAKINI KWENYE USAJILI

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wataongeza umakini katika michakato yao ya usajili ili kuhakikisha wachezaji wanaosajili wanakuwa na viwango vya kucheza timu hiyo

Mkwasa amesema Yanga ina mifumo ya kutengeneza wachezaji wake wa ndani lakini kwa wale wanaotoka nje lazima wawe na uwezo "Tutaweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha wachezaji tunaowasajili wana ubora. Hapa sisi kwetu hatuleti mchezaji kwa ajili ya kujifunza au kujiendeleza," amesema "Tunahitaji wachezaji wenye uwezo ambao wakija hapa wanakuja kufanya kazi moja kwa moja" "Tunajipanga kwa kushirikiana na Kamati ya Usajili na uongozi wa juu kuandaa utaratibu ambao utasaidia kusajili wachezaji ambao tunadhani watatusaidia katika nafasi ambazo tuna mapungufu"

Msimu huu Yanga imesajili nyota tisa wapya wa kigeni lakini miongoni mwao ni beki Lamine Moro, mlinda lango Farouk Shikhalo na Patrick Sibomana ambao wameonyesha uwezo unaoridhisha

Nyota wengine kama David Molinga, Sadney Urikhob na Juma Balinya wamekuwa wakiimarika taratibu huku kukiwa na uwezekano kwa Mustafa Suleyman, Issa Bigirimana na Maybin Kalengo kupewa mkono wa kwaheri wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa Disemba 16.

@Yangadaima
 
20191127_072958.jpg

WATAKAOSAJILIWA DIRISHA DOGO KUJUMUISHWA KIKOSINI MAPEMA
Baada ya mchezo dhidi ya Alliance Fc, ligi itasimama kupisha michuano ya CECAFA Chalenji ambayo itafanyika nchini Uganda kuanzia Disemba Mosi

Kulingana na ratiba ya Bodi ya Ligi, baada ya michuano ya CECAFA Chalenji kumalizika, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba January 04 2020

Lakini mwishoni mwa wiki ijayo, Yanga itaifuata Alliance Fc Novemba 29 jijini Mwanza kucheza moja ya mechi zake za viporo kabla ya baadhi ya wachezaji wake kwenda kujiunga na timu za Taifa kushiriki michuano hiyo

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema timu itaendelea na mazoezi kipindi chote cha mapumziko hayo

Aidha amesema watawajumisha kwenye kikosi baadhi ya nyota ambao wanataka kuwasajili dirisha dogo kujiridhisha na uwezo wao.

@Yangadaima
 
VIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Abdulaziz Makame na Mohamed Issa ‘Banka’ hawakuungana na wenzao katika mazoezi ya kujiandaa na Alliance Ijumaa.

Viungo hao wamekosa mazoezi ya leo na jana kutokana na kwenda Zanzibar kujiunga na timu yao ya Taifa ‘Zanzibar Herros’ kwa ajili ya mashindano ya Chalenji yanayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Akizungumza na Mwanasporti, msomaji wa Yanga News ,Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema Makame na Fei wamepewa ruhusa maalumu na uongozi.

“Bodi ya ligi imetubadilishia ratiba tukiwa tayari tumeshatoa mapumziko kwa wachezaji na Makame na Fei Toto tumeshindwa kuwarudisha kwa kuwa, wamejiunga na kambi ya Zanzibar Heroes moja kwa moja.

”Awali, ratiba ilionyesha hatutakuwa na mchezo ligi hadi Januari 4 dhidi ya Simba, lakini sasa tumepewa ratiba nyingine,” alisema Bumbuli.

Bumbuli aliongeza, hivyo wachezaji hao hawatakuwa sehemu ya kikosi kinachotarajia kusafiri alfajiri ya leo kwenda Mwanza.

@Yangafulldozz
 
Back
Top Bottom