Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191221_162110.jpg
 
Mi naona sio mbaya labda shida ni ile waliyosema mikia (sina hakika huenda walimsingizia pia) kwamba ameshindwa kusimamia discipline ndani ya timu. Mana akishashindwa kuisimamia basi hakutakuwa na timu tena kwani kila mchezaji ataamua afanye kile akitakacho akitegemea amepata kocha poa.

Kama vp wampe nafasi tuone.
A
Mchukueni tu Shadeeya ila akishindwa kusimamia nidhamu ndio mtajua kwanini sumu haijaribiwi kwa kuionja. Na ukizingatia pale Chura FC kuna wachezaji watumiaji wazuri wa Jamaican Vegetable basi itakua mambo ni moto hasaa
 
Kuna video niliiona muda wa asubuhi nikajikuta nacheka sana yaani lol.

Haijawahi kutokea watu wakalala chini namna ile aisee. Halafu yule sijui ni sonso au Moro alisimama wacha wamfuate akabakia kujikung'uta tu.

#amakwelisimbasiwatuwazuri. Teh teh
Hata mimi nilicheka sana kwakweli, nikasema hawa wadudu hawana adabu kabisa! Yaani wanawalaza watu chini bila kupenda! Ila ukijifanya mjuaji wanaondoka na roho yako, nyuki si wakuchezea Shadeeya
 
Umoto utaletwa na huyo mwalimu asiweza kusimamia nidhamu za wachezaji wake na huku kwenye kikosi cha wachezaji kuna wanaotumia cha Arusha au wengine wanaita mboga ya Jamaica, si patawaka moto hapo mamii?
Hakuna cha kuuwasha moto bwana.

Kila mmoja atasimamia nafasi yake na kwa kuwa tumeshaijua shida aliyonayo mwalimu ninaamini uongozi utamuweka wazi ili na yeye ajue namna ya kulisimamia hilo.
 
Hata mimi nilicheka sana kwakweli, nikasema hawa wadudu hawana adabu kabisa! Yaani wanawalaza watu chini bila kupenda! Ila ukijifanya mjuaji wanaondoka na roho yako, nyuki si wakuchezea Shadeeya
Nyuki hawafai kabisa Ses nakumbuka nikiwa la kwanza waliwahi kumng'ata mwanafunzi mwenzetu mpaka akafariki.

Hivyo nyuki sio wa kuchezea kabisa mana ukiwa mbishi hata manundu yanakuhusu. 😅😅😅
 
Nyuki hawafai kabisa Ses nakumbuka nikiwa la kwanza waliwahi kumng'ata mwanafunzi mwenzetu mpaka akafariki.

Hivyo nyuki sio wa kuchezea kabisa mana ukiwa mbishi hata manundu yanakuhusu. 😅😅😅
Poleni sana japo imepita miaka mingi toka afariki huyo mwenzenu wa darasa la kwanza

Ila pamoja na ukali wake wooote asali yake taaamu🤪🤪🤪
 
Hahahaaa. Leo hii mnajifanya weeema. 😎😎🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️ Kumbe hamna lolote.
Lunyasi sisi ni wema sana, tunataka mje uwanjani mkiwa hamna kisingizio sijui cha hatuna kocha, hatuna mazoezi mara tumeng'atwa na nyuki ili kichapo kiwe cha halali na kiwaingie barabara mkiwa na akili zenu timamu na bila kushawishiwa wala kulazimishwa na mtu yeyote
 
Back
Top Bottom