Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Daaa haka ka trip ka Mbeya kana ugumu flani hivi,ila kwa morali watayokuwanayo wachezaji hasa kutokana na sajili mbili tatu zilizofanyika naamini tutatoka na sita zetu huko
 
Kuna video niliiona muda wa asubuhi nikajikuta nacheka sana yaani lol.

Haijawahi kutokea watu wakalala chini namna ile aisee. Halafu yule sijui ni sonso au Moro alisimama wacha wamfuate akabakia kujikung'uta tu.

#amakwelisimbasiwatuwazuri. Teh teh
Simba wanachanganyikiwaga haraka sana. Yaani usajili Wa hapa na pale tu ulofanywa na wananchi umewachanganya hadi wanatutumia na nyuki
 
Na kama alikuwa hivo huko mikiani basi naamini hawezi rudia kosa, Japo ninaamini mikia ni waongo. Inaonyesha ni wanunuzi wazuri Wa mechi kwa hyo mpunga mwingi walikuwa wanatoa ukawauma wakawa wanaona kama Mwl hana mchango Mkubwa ktk ushindi walokuwa wanapata kitu ambacho si sahihi. Sema nnachompendeya yule kocha alikuwa anafundisha mpira Wa kushambulia sana
 
Shadeeya unaangalia mpira lakiniiiii? Sisi hatujaleta nyuki lakini habari ndio kama ulivyosikia
 
Daaa haka ka trip ka Mbeya kana ugumu flani hivi,ila kwa morali watayokuwanayo wachezaji hasa kutokana na sajili mbili tatu zilizofanyika naamini tutatoka na sita zetu huko
Hakika Mkuu tuna mechi ngumu sana kule.

Ila naamini tutafanikiwa japo mechi na Prison ndio inanipa hofu kubwa kuitoboa mana msimu huu iko vizuri.
 
Na kama alikuwa hivo huko mikiani basi naamini hawezi rudia kosa
Hakika Mkuu
Japo ninaamini mikia ni waongo
😅😅
Inaonyesha ni wanunuzi wazuri Wa mechi kwa hyo mpunga mwingi walikuwa wanatoa ukawauma wakawa wanaona kama Mwl hana mchango Mkubwa ktk ushindi walokuwa wanapata kitu ambacho si sahihi.
Hivyo wamemwonea tu mzee wa watu. Daah.
Sema nnachompendeya yule kocha alikuwa anafundisha mpira Wa kushambulia sana
Huo kwetu utatufaa
 
SIMBA NI TIMU YA KAWAIDA - MKWASA
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema hawana hofu kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa January 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa.

Mkwasa aliyewahi kuwa dimbani kwenye mchezo wa watani akiwa mchezaji na baadae kocha, amesema Simba ni timu ya kawaida.

Mkwasa amesema kwa sasa wameweka nguvu kwenye mechi za viporo ambazo watacheza kabla ya mchezo huo "Ni mapema sana kuzungumzia mchezo dhidi ya Simba Januari 04 kwani tuna mechi nyingine kabla ya mchezo huo" "Lakini kwa ufupi niseme kuwa Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu nyingine ambazo tayari tumecheza nazo," alisema Mkwasa

KIKOSI KIMEIVA

Katika hatua nyingine, Mkwasa amesema vijana wake wameanza kufanyia kazi mafunzo ambayo amekuwa akiwapa mazoezi na hivyo kuiongezea timu makali hasa katika ushambuliaji "Kwa sasa vijana wanaelekea vizuri kwani wanayafanyia kazi yale ambayo tumekuwa tukiyafanya mazoezini. Unaona sasa wanatengeneza nafasi nyingi na kuzitumia baadhi kufunga mabao. Mwanzoni hali ilikuwa tofauti" "Ni mwelekea mzuri na inatoa picha nzuri kwani naamini kwenye mechi zijazo tutaweza kufanya vizuri zaidi kuliko sasa," alisema

Katika mchezo wa kombe la FA uliopigwa jana dhidi ya Iringa United, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Kwenye mchezo huo Mkwasa aliwakosa nyota saba waliokuwa timu za Taifa za Zanzibar na Tanzania Bara ambao wamerejea hivi karibuni kutoka nchini Uganda walikokwenda kushiriki michuano ya Chalenji.

Lakini pia aliwakosa nyota wake wapya Tariq Seif, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima na Adeyum Saleh ambao mchakato wa usajili wao haukuwa umekamilika.

@Yangadaima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…