Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mkuu kyata

Nakubaliana na wewe tena kama huyo Nugaz tusipopata matokeo huwa neno lake kubwa eti tunatengeneza brand mmxieeew brand gani hiyo wakati sisi mashabiki tunahitaji matokeo.

Itakuwa wanaona raha tunavyochekwa kila kona.

Kuhusu huyo Yikpe lile ni jipu na hata Nchimbi mwenyewe namuona kichefu chefu tu naye.

Kusema ukweli timu yetu inasikitisha sana, yaani kila match ni kama wanaenda uwanjani kukamilisha ratiba tu. Morali ya wachezaji wote hiko chini mno, nadhani kuna tatizo somewhere si Bure na viongozi wapo tu wala hakuna juhudi zozote za kujikwamua, kazi ni kina Nugaz kujimwambafy tu kwenye vyombo vya habari eti wape salaam, na salaam tumezipata kweli. USHAURI: Viongozi na bench LA ufundi mjitafakari, ninahisi viatu hivi vimewapwaya. Huyo NUGAZ aache mbwembwe na tambo za mitandaoni anajichoresha tu. Mnabowa sana, nakaribisha wa kunikosoa kakini huo ndiyo ukweli. Halafu hivi aliyemsajili Yikpe ni nani? Mungu anakuona aisee, hivi mlikosa washambuliaji hadi Yikpe anatufaa? Mbona kuna vijana wa hapahapa tu na ni wazuri tuu ambao tungewapata hata kwa gharama ndogo tu na matokeo tungepataa? Yanga tunakwama wapi?
 
20200224_061129.jpg

KWA HALI HII ETI MTU ANAKWAMBIA TUNAEZA PATA UBINGWA LOL.
 
S
Tatizo nyie wazee wa Miamala sana.

Kwa gape hiyo mnadhani mwaeza achia tupate ubingwa kirahisi lazima tu wapewaji wa Ist 😛waongezeke mana tumeshawapa matumaini makubwa.
Hivi hizo "sare" za harusi hazijatimia kwani Shadeeya🤣🤣🤣?
 
Back
Top Bottom