Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

simba anataka nyama(njaaaaa)
IMG_20200305_141746.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto akikua muache nae aitwe baba ila baba siku zote atabaki kuwa baba, historia hazifutiki na hesabu hazidanganyi
dcb04374bc5ed8e4580afc1c91edb7be.jpg
 
Kwa mujibu wa vitabu vya dini Biblia, Torah na Quran, mwenyezi Mungu alimuumba Adam na baada ya Adam kuwa na upweke mwingi, mwenyezi Mungu alimshushia usingizi mzito na akazinyofoa mbavu zake za kushoto na kumuumba Hawa, ili amuondolee Adam upweke. Wawili hawa wakazaa watoto na vizazi vyao vikasambaa Dunia nzima.

Nadharia hii inauhusiano mkubwa na mambo mbali mbali duniani ikiwemo hapa kwetu Tanzania. Miaka 17 baada ya kutamatika kwa WW1 nikimaanisha mwaka 1935, enzi hizo ukoloni umeshamiri katika viunga vya Tanganyika na visiwani, iliundwa timu ya wananchi, timu ambayo iliundwa ili kuwaunganisha, kuwakutanisha, kuwaletea furaha na kuwaondolea adha na mateso ya ukoloni watanganyika, timu ya Young Africans.

Muda mfupi baada ya kuundwa timu ya Kwanza kabisa Tanganyika bara na visiwani, watanganyika sambamba na baadhi ya waarabu waligundua Young Africans inapitia kipindi kingi cha UPWEKE Kama kile alichokipita Adam baada ya kuumbwa. Ndio hapo likafanyika Jambo ili kumfurahisha Young Africans kwa kumletea mwenza (Hawa) ili amuondolee upweke mwingi aliokuwa nao. Mwaka 1936, baada ya mwaka mmoja wa shida,upweke na kulala kwa kukumbatia mito kila siku, hatimae muda ulifika na Young Africans akaketewa HAWA wake, kwa kuundwa timu ya Sunderland enzi hizo.

Hakika ilikuwa ni furaha ya ajabu, nderemo na vifijo vilitawala viunga vyote vya tanganyika, manamba mashambani, walimu mashuleni, wafanyakazi wa migodi,viwandani,Askari wa KAR, maakida na Liwali, wahindi na watu wote waliokuwepo enzi hizo hakika walifurahi baada ya Adam kuletewa Hawa wake.

Historia inaonyesha Hawa hana cha kusema mbele ya Adam, kwani Hawa kachapwa mara nyingi zaidi.

timu ya wananchi inakutana na timu iliyoundwa kuiondolea upweke, Adam anakutana na Hawa wake. Najua wakubwa mnaelewa Adam akikutana na Hawa nini kinatokea.

Tukutane Taifa..😁
 
Tukutane Taifa..[emoji16]
Ujumbe wa karne huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom