Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Wajitafakari aiseee. Wajue hatupendi furaha za vipindi sisi kama tunaweza kumfunga Simba hawa vidagaa wanatufungaje?

Tusubiri leo tuone huko Lindi napo.
Uwezo uwanjani hamna Shadeeya, kwenye ile mechi na Simba kamati yenu ya "ufundi" ilifanya mambo. Mlichoharibu baada ya kuwabeba hamkuwalipa, sasa wamewaachia muonyeshe hicho kiwango chenu mnachodhani mnacho
 
Yaani wacha tuitwage Utoporo tu, mi mwenyewe walinikera mbaya wenzao tulitaka tuendeleze furaha wao wanaleta masikhara. 😔

Kama Molinga kuna nafasi ya wazi aliipoteza kizembe sa sijui mawazo yake yalikuwa wapi sababu yale maamuzi ya haraka aliyakosa kabisa.
Yaani umeona goli alilokosa Molinga tu? Na nyie mlikoswakoswa pia ukumbuke. Ilikua mpapaswe viwili safi kabisa
 
"Nimekuja na wachezaji wachache lakini nna imani tutafanya vizuri na kupata matokeo dhidi ya timu bora Namungo FC, Ni kama Simba SC baada ya kupoteza mchezo waliinuka na kushinda mchezo unaofuata 8-0 hii ni ishara ya timu bora. . naamini vijana wangu pia watathibitisha hilo leo jioni kuwa Yanga SC ni kubwa na timu bora. . Kuhusu wachezaji ambao hawajasafiri pamoja na timu nadhani ni vema nikaliweka wazi hili. . nimesikitishwa sana kwangu mimi ni kukosa uweledi wengine ni majeruhi kama Adeyun , Kelvin Yondani ana matatizo ya kifamilia na Niyonzima Haruna amesimamishwa . . wengine nasikia imewahi kutokea huko nyuma, hili sikubaliani nao na sio kariba ya klabu kubwa kama Yanga . . kuna wachezaji wanachagua mechi za kucheza yaani Sadio Mane ama Mohamed Salah aseme hataki kwenda kucheza huko?. . OOOOOPs ni nini hicho? kuna wachezaji wanadhani wao ni Ronaldo au Messi? hata hao hawafanyi hivo . . hii sio heshima kwa klabu, hii sio heshima kwa nembo ya Yanga SC. . sio heshima kwa wachezaji wenzao na wafanyakazi wote wa Yanga na mashabiki wake"

-Luc Eymael.

NIMESIKITIKA SANA NIMEONA KOCHA KAONGEA KWA MASIKITIKO SANA. SIJUI KUNA KITU GANI KINAENDELEA SISI HATUJUI
Wazungu hua ni wakweli sana. Katamka mwenyewe kua ushindi wa Simba wa bao 8 kwa sifuri baada ya kutoka kupoteza mechi ni alama ya timu bora
 
Back
Top Bottom