Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

MAFANIKIO NJE YA MIPAKA.
Yanga kama yanga ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA. itakumbukwa tu yanga waliwafunga express ya uganda kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC villa.
€€€Huu nao ni uandishi kanjanja mwanzoni mwa karne ya 21 . Ati Yanga ndiyo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe . Mwandishi unamaana gani hasa kutulisha matango pori kama haya . Dunia simama Yanga atuelezee
 
Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema wachezaji wa timu hiyo wana ari kubwa na wamepania kuwapa furaha mashabiki katika michezo iliyobaki

Yanga imerejea mazoezini wiki iliyopita, nyota hao wakiendelea kujifua chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa 'Master'

Abdul amesema wamepania kufanya vizuri katika michezo yote iliyobaki akitamba kuwa hawafikirii kama kuna mchezo watapoteza "Wachezaji wako tayari, we mwenyewe si unaona namna tulivyo na ari kubwa katika mazoezi, tunajiandaa kikamilifu na michezo iliyobaki ya ligi na ile ya FA "Hatutegemei kupoteza mchezo wowote tupo tayari kuikabili timu yoyote na tutapata matokeo chanya na sio kupoteza," amesema Abdul

Kipimo cha kwanza kwa mabingwa hao wa kihistoria ni siku ya Jumapili, Juni 07 ambapo wataumana na KMC katika mchezo wa kirafiki ambao utapigwa uwanja wa Uhuru

Baadae timu itaelekea mkoani Shinyanga ambapo Juni 13 itafungua rasmi ligi katika uwanja wa CCM Kambarage, kwa kuikabili Mwadui Fc.
 
Wanaendaje shinyanga tena,kwani ule muongozo wa kuwa ligi itachezewa dar tu upoje??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…