Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mkuu ungejua jinsi Yanga na UKONWE wake ilivyotia aibu juzi kwenye mechi yake na JKT hii thread ungeimeza na uilete siku nyingine! Nilikuwemo Jamhuri ile juzi wakat maafande walipowapelekesha kikwelikweli mbele ya waziri Mwakyembe na wabunge kibao! Hata lile goli refa angekuwa makini halikuwa halali! Sasa cha kushangaza badala ya kucheza soka mnaanzisha masumbwi, tena wachezaji wa kimataifa, nikajiuliza hivi hii ni Yanga au ni zile timu za ndondo Cup! Pia uzi wako umeegemea zaidi kwenye mihemko ya kishabiki, sentensi zako nyingi zinazoitaja yanga kama ndio klabu pekee sio za kweli! Huwezisifia Yanga kwa ubingwa Afrika mashariki leo hii wakati hadi Azam walishabeba kombe hilo achilia mbali Simba ambayo ilirudisha kombe hilo nchini likiwa limepotea kwa miaka zaidi ya 20! Huwezisifia Yanga kwa uwanja wa Karume leo hii wakati Azam wana Chamazi Comlex na Msimbazi kuna MO Arena!...Kwa upande wa kombe la ligi, lakini kwa upande wa medani ya kimataifa tuache Ushabiki Simba ni bora zaidi kuliko timu yoyote Tanzania rejea hata takwimu za ubora zilizotolewa mara ya mwisho na FIFA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…