Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

we acha mechi ya tatu mfululizo tunatoa sare tena sisi ndio tunarudisha kwa mbinde haya mateso ndugu zangu hayo mabadiliko yaje haraka
Poleni sana mkuu, ndio ukubwa huo lakini. Wakati mwingine changamoto kama hizo ndio zinawapa fundisho la kuchagua viongozi wenye maono na uwezo wa kuwapitisha na kuwavusha kwenye nyakati ngumu kama hizi
 
Mashabaki wapigwa STOP .

Serikali imepiga marufuku mashabiki wa soka katika mikoa nje ya Dar es Salaam, kuingia viwanjani kutazama mechi za Ligi Kuu zitakazohusisha timu za Simba na Yanga kuanzia Jana hadi pale itakapojiridhisha .

Agizo hilo limetolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufuatia kukiukwa kwa miongozo iliyowekwa ya kukabiliana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika juzi katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, baina ya Mbeya City na Simba .

Katika taarifa yake iliyotolewa jana jioni, serikali imesema imechukua hatua hiyo baada ya kubaini kutofuatwa kwa miongozo iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na virusi hivyo .
 
Mbona nyie mnapitisha miamala kwa wahusika mpira uchezwe dakika 100 ili msawazishe goli hatusemiii😂😂😂
Mpira hata ukiongezwa dakika 1000 huwezi kulalamika kwa sababu inakuwa nafasi ya kufunga kwa timu zote. Kwa mfano ingekuwa 3-1
 
20200627_055149.jpg

Kiungo Mshambuliaji, Mapinduzi Balama atakosekana kwenye Kikosi cha timu ya Wananchi kwa takribani wiki tatu baada ya kuumia mazoezini jana.

Get Well Soon

#DaimaMbeleNyumaMwiko.

@YangaSc
 
Back
Top Bottom