Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Inamana Zambia nzima mchezaji ni Bwalya? Au ndio unawalisha viongozi wetu maneno?
 
Mtani ni wiki sasa hujapost kitu humu, natumaini kwamba unaendelea vizuri.

Hizi taarifa za Simba kumtangaza mchezaji mliyemfata Zambia nadhani utakuwa nazo, vipi unasemaje kuhusu hili?
Hahahaaa. Mie Alhamdulillah Mtani.

Ninazo ila nirudie tu ile kauli ya Bumbuli kwamba nyie mnasajili kwa tetesi mnazozisikia mitandaoni na magazetini kuhusu Yanga na kiukweli hatukuwa tukimuhitaji huyo Bwalya. Teh teh
 
Nyie Utopolo kama mnavyojua Simba sc ndio Bayern Munichen ya hapa Tanzania, hivyo nitoe rai kwenu kuwa tunataka kufanya kile kilichomkuta Barcelona hivyo mjiandae kisaikolojia.

Simba nguvu moja
Simba bingwa CCL 2020/2021
Shadeeya
Hahahaaa. Baada ya kupigwa goli nane naona mnajikataa. Lol

"Sisi simba ni level za Barcelona" (in Ropo ropo Voice) Teh
 
Hahahaaa. Mie Alhamdulillah Mtani.

Ninazo ila nirudie tu ile kauli ya Bumbuli kwamba nyie mnasajili kwa tetesi mnazozisikia mitandaoni na magazetini kuhusu Yanga na kiukweli hatukuwa tukimuhitaji huyo Bwalya. Teh teh

Afadhali umerudi utupe update za kesi ya Morrison huko FIFA.

Bwalya tumeshamalizana naye.
 
Utazipata Mtani japo kwa sasa anga limetulia hivyo mjiandae mana tunaanza kuwashusha mmoja mmoja. lol

Hongereni kwa kukusanya Mtani.

Nimekuelewa hapo kwa Bwalya.

Hongereni kwa usajili mwingine, nimesikia mmemsajili aliyekuwa dreva wa Senzo.
 
Hahahaaa. Kwa sasa kejeli zenu zote tunazipokea Mtani.

Mtani hiyo taarifa nimesikia ni kweli, Senzo alihitaji aje na watu wake. Na huyo dreva ndiye mtu wake muhimu imebidi mmchukue.

Tunasubiri kuyaona majina mnayosajili mtani, sisi tunaendeleza kufanya yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…