MAFANIKIO NJE YA MIPAKA.
Yanga kama yanga ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA. itakumbukwa tu yanga waliwafunga express ya uganda kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC villa.
yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa afrika mashariki na kati na kupelekea serikali ya tanzania kutuma ndege mpaka katika uwanja wa ndege wa entebe kwenda kuwachukua waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso yaani yanga.
hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau yanga maishani mwao.
yanga katika mechi hiyo iliwakilishwa na:
1) steven nemes
2) mwanamtwa kihwelu
3) keneth mkapa
4) willy mtendamema
5) issa athuman
6) method mogella
7) steven mussa
8) hamis thobias gagarino
9) said mwamba kizota
10) mohamed husein chinga one
11) edibily jonas lunyamila
pia yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama willy martin, rifat said, aboubakar salum "sure boy" david mwakalebela "MP" na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda.
katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahili wa villa na timu ya taifa ya uganda marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba winga wa yanga edibily lunyamila, lakini alilazimishwa na kocha wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili.
kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na yanga na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama "lunyamila trans" "kizota trans" au hata wengine walifuta majina ya salon zao na kuandika "gagarino hair salon" na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka tanzania inakwenda huko wanauliza "je ni yanga?".
na baada ya ushindi huo mwanamuziki nguli wa afrika marehemu kabasele yampanya al maarufu kama peppe kalle alitunga wimbo wa kuisifia timu hiyo baada ya kuonyesha dhahili kiwango cha juu na kuvutia washabiki wengi wa soka kitu ambacho hakijawahi kufanywa na klabu yoyote nyingine hapa nchini.
.