Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Villa Squad 0-1 Yangamatokeo vip waungwana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Villa Squad 0-1 Yangamatokeo vip waungwana
Tushawazoea nyie waosha vinywa.....afadhali wameshinda maana wangetoka sare hapo uwanjani pasingetosha, wananchi wa mbagala wangevunja viti huku mabondia wa jangwani wakimalizana na waamuzi na wachezaji wa villa kama kawa
Yanga bad tuna tatizo la umaliziaji na hili ni tatizo la upangaji timu unaofanywa na kocha Kostadin Papic.....Mwape na Asamoah ni mzigo mkubwa sana kwa Yanga na wanatughaarimu sana.....
Sijui ni kwa nini anambania huyu bwana mdogo Pius Kisambale na Idrissa Rashid.....Hawa vijana ni wazuri kuliko Mwape na Asamoah
Hapa tupo pamoja sana Muraa....Mwape na Asamoah wanaigharimu timu si kwa kulamba mishahara minono tu lakini pia kwa kushindwa kufunga magoli pale timu inapokuwa inayahitaji kwa udi na uvumba.
Msimu ujao tupa kule hao wote foreigners wabaki Kiiza na Niyonzima. Pale mbele wachezeshwe wabongo mbona wana uwezo mkubwa? Yule dogo Idrisa, Kisambale, Tegete na Chidi wana uwezo wa kuiletea timu mafanikio kuliko hayo magarasa Mwape na Asamoah!
Full Time
Villa Squad 0-1 Yanga
Hongereni sana wana Yanga wenzangu.......
Hapa tupo pamoja sana Muraa....
Hao Mwape na Asamoah wote waliletwa na Papic so anawapanga kwa utashi wake mwenyewe.....Pia mwingine anayepaswa kubaki ni Golikipa Yaw Berko japo kuna magolikipa wazalendo wanakuja juu...Said Mohamed na Shaaban Kado
Berko anasumbuliwa na goti Muraa.....Hakuna cha Misumari wala nini....Yeah Yaw Berko naye bado anahitajika. Nasikia kapigwa misumari ndo maana haponi!
Niliwahi kusikia kwamba papic huwa anajipatia ''commission'' kila anaponunua hawa mapro, sasa analazimika kuwapanga tu hata kama hawana viwango ili kutekeleza makubaliano na kujustify ununuzi wao.
Shabani Kado aliyataka mwenyewe.....atakaa benchi mpaka aote nakozi za ******: alikimbia Mtibwa akifikili Yanga kuna mtelemko..............duh!Berko anasumbuliwa na goti Muraa.....Hakuna cha Misumari wala nini....
Ukiangalia sasa hivi golini anakaa Said Mohamed.....Kado anakaa benchi......Utaratibu ambao nimeupenda kimsingi
Hilo suala la Papic kupata 10% hata mimi nimelisikia....
Mbona Kado anachezeshwa mkuu?........Amecheza mechi nyingi tu akiwa Yanga na binafsi nimeupenda sana utaratibu wa Yanga kuwachezesha magolikipa wote watatu badala ya kumtegemea kipa mmoja....Said Mohamed na Kado wote wanachezeshwa kwa zamu tofauti na Timu zingine.....Shabani Kado aliyataka mwenyewe.....atakaa benchi mpaka aote nakozi za ******: alikimbia Mtibwa akifikili Yanga kuna mtelemko..............duh!
hongera sana nawe mkuu bala.....
Mtaa wa pili wamepiga kimya ghafla......
Ni ya kweli kabisa....Mwasyika yupo huru kucheza dhidi ya Coastal Union,pia Nadir Haroub, Tegete, Omega Seme na Nurudin Bakari.........TFF na Kamati yake ya ligi(inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu) walikurupuka katika kutoa adhabu...Kamati ya Ligi haina mamlaka ya kutoa adhabu,hiyo kazi ilitakiwa ifanywe na kamati ya Nidhamu ya TFF....Kwa ujumla TFF ni watu wa hovyo kabisa(samahani kwa kulisema hili),wao wamekali kuangalia mapato tu na hawaangalii kanuni zinasemaje,wangekuwa makini sidhani kama hiyo kamati ya Ligi ingekurupuka kutoa hukumu hizo ilhali kamati ya Nidhamu ipo...Cha ajabu ni kwamba baada ya Kamati ya akina Tibaigana kutoa maamuzi haya TFF wameanza kuweweseka na kusema watakutana katikati ya wiki kujadili maamuzi haya ya Kamati ya Nidhamu......What a shame kwa Leodgar Tenga na TFF yake....mkuu Balatanda ya kweli hayo!! Hata Mwasika kacholopoka!!!!! Niruhusu nikate rufaa aiseee. Mwasika havumiliki kwa kitendo alichokifanya aiseee.