Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Safi sana Niyonzima na Kisambale........Kazi nzuri


Mfungaji Hamis Kiiza 'Diego'
 
Full Time

Villa Squad 0-1 Yanga

Hongereni sana wana Yanga wenzangu.......
 
Hamisi Kiiza,tunajikongoja kama Man U
Sasa hivi tunashika nafasi ya 2 kwa kuwa na point 43 tunatofautiana na Simba kwa point 1 wao wanaongoza kwa point 44, Azam wanashika nafasi ya 3 kwa kuwa na point 41......
 
viva yanga mbele kwa mbele kama simba alivyo mbele daima
 
Kwa mwendo huu lazima turudia tulichofanya msimu uliopita.....

Sasa hivi tunalingana idadi ya mechi na tuna tofauti ya point moja tu....
Pointi 1 ni kubwa kaka; bila Simba kupoteza mchezo hiyo kuipata ni ngumu.
 
afadhali wameshinda maana wangetoka sare hapo uwanjani pasingetosha, wananchi wa mbagala wangevunja viti huku mabondia wa jangwani wakimalizana na waamuzi na wachezaji wa villa kama kawa
 
Yanga bad tuna tatizo la umaliziaji na hili ni tatizo la upangaji timu unaofanywa na kocha Kostadin Papic.....Mwape na Asamoah ni mzigo mkubwa sana kwa Yanga na wanatughaarimu sana.....

Sijui ni kwa nini anambania huyu bwana mdogo Pius Kisambale na Idrissa Rashid.....Hawa vijana ni wazuri kuliko Mwape na Asamoah
 
Pointi 1 ni kubwa kaka; bila Simba kupoteza mchezo hiyo kuipata ni ngumu.
Ni kweli kama Ligi itaisha kwa Simba kushinda mechi zote ama kutotoka sare....

Kumbuka baada ya wachezaji wetu 6 kufungiwa kuna waosha vinywa wa mtaa wa pili walishaanza kusema Yanga kwishne.....Kwamba itakuwa ni vipigo tu sasa,lakini imekuwa tofauti maana mechi zote mbili tulizocheza baada ya adhabu hiyo tumeshinda na kupata point 6 saaaaaaaaaaaaaafi....

Nilikuwa naonesha mfano wa msimu uliopita mkuu ambao mwenendo wa ligi ulikuwa kama huu.....

Kesho mnakipiga na Mtibwa Jamhuri........Tawi lenu lile lol...
 
Hongera Bala. Mtibwa Vs Simba tena Jamhuri stadium imekaa kimtego kweli..

Asante sana mkuu....

Mtibwa kwa Simba hakohoi......Hata Simba wawe wabovu wakikutana na Mtibwa lazima wajipigie...

Hili hutufanya wengine tudhani Mtibwa ni Simba B......Kama ilivyo kwa Coastal na Azam FC, hawa wakikutana na Yanga wanakaza mpaka basi ila wakikutana na Simba wanakuwa Urojooooooooo

So Simba kesho wajihesabie ushindi
 
Back
Top Bottom