Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

afadhali wameshinda maana wangetoka sare hapo uwanjani pasingetosha, wananchi wa mbagala wangevunja viti huku mabondia wa jangwani wakimalizana na waamuzi na wachezaji wa villa kama kawa
Tushawazoea nyie waosha vinywa.....

Tunakuja kuwashika....
 
Yanga bad tuna tatizo la umaliziaji na hili ni tatizo la upangaji timu unaofanywa na kocha Kostadin Papic.....Mwape na Asamoah ni mzigo mkubwa sana kwa Yanga na wanatughaarimu sana.....

Sijui ni kwa nini anambania huyu bwana mdogo Pius Kisambale na Idrissa Rashid.....Hawa vijana ni wazuri kuliko Mwape na Asamoah

Mwape na Asamoah wanaigharimu timu si kwa kulamba mishahara minono tu lakini pia kwa kushindwa kufunga magoli pale timu inapokuwa inayahitaji kwa udi na uvumba.

Msimu ujao tupa kule hao wote foreigners wabaki Kiiza na Niyonzima. Pale mbele wachezeshwe wabongo mbona wana uwezo mkubwa? Yule dogo Idrisa, Kisambale, Tegete na Chidi wana uwezo wa kuiletea timu mafanikio kuliko hayo magarasa Mwape na Asamoah!
 
Hapa tupo pamoja sana Muraa....

Hao Mwape na Asamoah wote waliletwa na Papic so anawapanga kwa utashi wake mwenyewe.....Pia mwingine anayepaswa kubaki ni Golikipa Yaw Berko japo kuna magolikipa wazalendo wanakuja juu...Said Mohamed na Shaaban Kado
 
Yeah Yaw Berko naye bado anahitajika. Nasikia kapigwa misumari ndo maana haponi!
Niliwahi kusikia kwamba papic huwa anajipatia ''commission'' kila anaponunua hawa mapro, sasa analazimika kuwapanga tu hata kama hawana viwango ili kutekeleza makubaliano na kujustify ununuzi wao.
 
Berko anasumbuliwa na goti Muraa.....Hakuna cha Misumari wala nini....

Ukiangalia sasa hivi golini anakaa Said Mohamed.....Kado anakaa benchi......Utaratibu ambao nimeupenda kimsingi

Hilo suala la Papic kupata 10% hata mimi nimelisikia....
 
m.jpg

Dah....Huyu jamaa bado yupo wakuu...

Mshambuliaji+wa+Yanga+Hamis+Kiiza+akimtoka+beke+wa+Villa+Squad.JPG

Muuaji Diego....

Mshambuliaji+wa+Yanga,+Hamis+Kiiza+akiwatoka+mabeki+wa+Villa.JPG

Diego katika move....
 
Berko anasumbuliwa na goti Muraa.....Hakuna cha Misumari wala nini....

Ukiangalia sasa hivi golini anakaa Said Mohamed.....Kado anakaa benchi......Utaratibu ambao nimeupenda kimsingi

Hilo suala la Papic kupata 10% hata mimi nimelisikia....
Shabani Kado aliyataka mwenyewe.....atakaa benchi mpaka aote nakozi za ******: alikimbia Mtibwa akifikili Yanga kuna mtelemko..............duh!
 
Shabani Kado aliyataka mwenyewe.....atakaa benchi mpaka aote nakozi za ******: alikimbia Mtibwa akifikili Yanga kuna mtelemko..............duh!
Mbona Kado anachezeshwa mkuu?........Amecheza mechi nyingi tu akiwa Yanga na binafsi nimeupenda sana utaratibu wa Yanga kuwachezesha magolikipa wote watatu badala ya kumtegemea kipa mmoja....Said Mohamed na Kado wote wanachezeshwa kwa zamu tofauti na Timu zingine.....
 
Mkuu Bala leo yanga mna mechi? nataka nianze kuwaombea njaa lol
 
WACHEZAJI WA YANGA WALIOFUNGIWA WAACHIWA HURU

Kamati ya Nidhamu ya TFF – imewachia huru wachezaji watano wa klabu ya Yanga waliokuwa wamefungiwa kutokucheza mpira kwa vipindi tofauti na kamati ya ligi ya TFF, baada ya kamati ya nidhamu kuridhika na maelezo ya utetezi wa klabu ya Yanga juu ya adhabu hizo zilizotolewa wiki mbili zilizopita.

Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu – TFF Mh.Afred Tibaigana alisema kwa mujibu wa taratibu za shirikisho la mpira wa miguu nchini – TFF kamati ya ligi haina mamlaka ya kumfungia mchezaji yoyote wala kutoa adhabu kwa mchezaji yoyote isipokuwa kamati ya nidhamu ndo yenye mamlaka hayo, hivyo maamuzi yaliyofanywa na kamati ya ligi sio halali, na kama bado wanataka kuwashitaki tena wachezaji hao inabidi wapeleke malalamiko yao upya kwa kamati ya Nidhamu.

Awali kamati ya ligi ya mashindano iliyokutana tarehe 12.03.2012 chini ya mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu ilitoa adhabu kwa wachezaji watano (5) wa Yanga kutokana na kile walichokiita utovu wa nidhamu kwa wachezaji wa yanga katika mchezo dhidi ya Azam fc, mchezo uliochezwa machi 10 mwaka huu.

Kamati hiyo ya ligi ilitoa adhabu ya kumfungia mchezaji Stephano Mwasika mwaka mmoja kutocheza mpira na faini ya tsh milioni moja, Jeryson Tegete alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa miezi sita (6) na faini ya sh.500,000, Nadir Haroub Cannavaro alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa mechi sita (6) na faini ya sh.500,000, Nurdin Bakari alifungiwa kutocheza mechi tatu (3 )za ligi kuu na faini ya sh.500,000 na Omega Seme alifungiwa kutocheza mechi tatu (3) za ligi kuu na faini ya sh.500,000.

Kutokana na maamuzi ya kamati ya nidhamu – TFF wachezaji hawa watano (5) waliokuwa wamefungiwa kwa sasa wapo huru na wanaruhusiwa kucheza michezo inayofuata katika ligi kuu mpaka hapo TFF itakapopeleka malalamiko mapya juu ya wachezaji hao kwa kamati ya nidhamu.

Klabu ya Yanga itawatumia wachezaji wake hao katika mchezo dhidi ya timu ya Coastal Union ya Tanga jumamosi ijayo katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika jijini tanga machi 31-2012
Katika hatua nyingine kesi iliyokuwa inawakabili Louis Sendeu Afisa Habari wa klabu ya Yanga na Ismail Aden Rege mwenyekiti wa klabu ya Simba, juu ya kutishia kutopeleka timu uwanjani katika mchezo wa Ngao wa Hisani ulofanyika august mwaka 2011, kamati hiyo ya Nidhamu imewapa onyo kutorudia kitendo hicho, kwani kufanya vile ni kuchochea uvunjani wa amani katika michezo.

WACHEZAJI WA YANGA WALIOFUNGIWA, WAACHIWA HURU. « Millard Ayo
 
mkuu Balatanda ya kweli hayo!! Hata Mwasika kacholopoka!!!!! Niruhusu nikate rufaa aiseee. Mwasika havumiliki kwa kitendo alichokifanya aiseee.
 
mkuu Balatanda ya kweli hayo!! Hata Mwasika kacholopoka!!!!! Niruhusu nikate rufaa aiseee. Mwasika havumiliki kwa kitendo alichokifanya aiseee.
Ni ya kweli kabisa....Mwasyika yupo huru kucheza dhidi ya Coastal Union,pia Nadir Haroub, Tegete, Omega Seme na Nurudin Bakari.........TFF na Kamati yake ya ligi(inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu) walikurupuka katika kutoa adhabu...Kamati ya Ligi haina mamlaka ya kutoa adhabu,hiyo kazi ilitakiwa ifanywe na kamati ya Nidhamu ya TFF....Kwa ujumla TFF ni watu wa hovyo kabisa(samahani kwa kulisema hili),wao wamekali kuangalia mapato tu na hawaangalii kanuni zinasemaje,wangekuwa makini sidhani kama hiyo kamati ya Ligi ingekurupuka kutoa hukumu hizo ilhali kamati ya Nidhamu ipo...Cha ajabu ni kwamba baada ya Kamati ya akina Tibaigana kutoa maamuzi haya TFF wameanza kuweweseka na kusema watakutana katikati ya wiki kujadili maamuzi haya ya Kamati ya Nidhamu......What a shame kwa Leodgar Tenga na TFF yake....
 
Back
Top Bottom